Ushauri wako, nini kifanyike? Vijana wanapukutika

Ushauri wako, nini kifanyike? Vijana wanapukutika

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2010
Posts
15,145
Reaction score
5,574
Sikilizeni vijana wanapukutika sana,
Vifo vingi ni vya vijana below 40 years,
Shida ni nini, tatizo ni nini?

Kwanini vijana wanakwisha hivyo,
Magonjwa yanamaliza vijana,
Ajali zinamaliza vijana,
Msongo wa mawazo unamaliza vijana,

Wengine wanaacha wake/waume zao wabichi kabisa,
Wengine wanaacha watoto wao wadogo hata hawajawatambua,
Nenda makaburini kasome zile namba kwenye makaburi, utalia

Vijana wamekosea wapi, wamekengeuka wapi?
Najua hapa MMU wengi ni vijana, tushauriane,

Tuonyane kama ni kuonyana, tushauriane kama ni ndio inafaa

Mokoyo
 
Ni topic pana sana kuijadili ila kwa kifupi niseme kuwa imefikia wakati sasa vijana wanatakiwa kujitambua na kuthamini maisha yao. Hii ni pamoja na
  • Kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kukuingiza kwenya magonjwa yasiyo na tiba kama UKIMWI
  • Kujitunza kiafya ikiwemo kula vizuri, kuepuka vyakula hatarishi au vilivyoandaliwa kihatarishi vyenye mafuta mengi au viungo kupita kiasi, kufanya mazoezi nk vitasaidia kuepuka magonjwa kama kisukari, BP, Magonjwa ya moyo nk
  • Kuepuka na kujiepusha na ulevi kupindukia ambao kimsingi huchangia kuleta ajali na matatizo yasiyo ya lazima
  • Kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabaunifu ili kuiongezea kipato na kupunguza mawazo na tabia hatarishi kama wizi ambao waweza kusababishi kifo
  • Vijana wanaoendesha vyombo vya moto (Magari, pikipiki nk) wawe makini kama marubani wa ndege na kufuata sheria za barabarani kupunguza vifo kwa njia ya ajali
  • Kupata muda wa kupumzika na kufurahi ili kuondoa stress
  • Kumuomba Mungu aendelee kutulinda na pia kujiapesha na kushawishiwa viabaya ili pia tusiingie kwenye balaa la vita vya kidini maana hivyo ndo vitawamaliza vijana wote kabisa ...
  • .....

Nawasilisha,

HP
 
Mkuu epukana na hizi kauli tata, ni kweli hali inatisha, ushauri wako?

Kwa kuongezea ni kwamba vijana mna tabia mbaya za kimaisha katika vitu hivi :-
1. Kutokunywa maji ya kutosha kiasi kwamba haja ndogo inatoka ikiwa njano na haikawii kuoza mara tu ikitua chini, hii ni dalili ya madhala mengi yatokanayo
2. Kutosinzia masaa ya kutosha vijana siku hizi wanakesha kwenye burudani hawana muda wa kuutumia vizuri usiku kwa kulala
3. Ulaji nalo ni eneo lingine linalowapa ubovu wa afya kutokula mlo uliokamilika limekuwa tatizo sugu kwa vijana wengi.
4. Kuoga kikamilifu hakufanyiki zaidi ya kujimwagia maji na wengine kutooga kwa muda wa hata week!
5. Kutofanya/kutopenda Kufanya kazi kunafanya ubongo kudumaa na hivyo kuharibu mfumo wa ukuaji chembe hai mwilini
Naishia hapa kwanza wadau
 
Ni tatizo kubwa, many are committed to sex!...vijana!...from morning to evening are warming for sex, no way, he who doesnt fear God..let him/her go way..
 
Kila nafsi itaonja umauti.


Kila umri ni sahihi kwa kufa.
 
Si kweli. Aslimia 65% ya population ni vijana.
Ndo maana unaona wanakufa wengi.
Kama una research data tupatie.
 
Cha kufanya vijana wamrudie Mungu. Maana huko ndiko kuliko na msaada, pia wajifunze kutawala hisia zao
 
vijana wengi hawana maadili, hawana maadili ya chakula, mapenzi , vinywaji. maadili ni kufuata sheria za jamii husika kama , kutokunywa pombe, kutokuzini, kutokutumia pesa vibaya n.k. kama vijana watafuata madili mema basi na vivyo vitapungua
 
Kweli vijana wengi! Tuko kwenye kundi la kifo kuzidi hata! Wazee! Mi nashauri tumurudie mwenyezi Mungu! Tumuombe Mungu atuepushe na hizi balaa za dunia Mara Wizi,Ujambazi,Pombe kupindukia(viroba sana),Uzinzi!Utapeli,, naamini tukiyaepuka haya na siku zetu za kuishi zitasogea!
 
Mitikasi haikamatiki...wanga wanazidi kubana....ndo maana vijana tunaona bora tujiripue na mjani angalau tupunguze STRESS...si unajua ile kitu inavyokimbiza stimu..?
 
Si kweli. Aslimia 65% ya population ni vijana.
Ndo maana unaona wanakufa wengi.
Kama una research data tupatie.

Big Lady kuwa asilimia kubwa sio tafsiri sahihi ya kutokea vifo vingi kwenye age ya ujana
 
ulevi,uasherati,tamaa ya pesa ya haraka kwa njia za mkato na madawa ya kulevya yanafupisha maisha ya vijana
 
Well sayed

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom