Ushauri wako ni muhimu

Ushauri wako ni muhimu

Aiseee sijawahi kutoa comment huku ila Leo inanibidi kwanza nikuulize swali unampenda mkeo au huyo mzazi mwenzio?Hapo cha muhimu kaa chini uongee na mkeo umwambie kila kitu,yeye ndo ataamua nini cha kufanya ni bora umwambie mapema kuliko aje kusikia kwa mtu mwingine
 
Mimi naitwa Fred ... Ni baba wa familia ya Mke na watoto wawili, naipenda familia yangu na tunaishi vizuri. Kikubwa nilipata promotion kazini Hali iliyolazimu niiache familia yangu pale tulipojenga Makazi yetu ili nikajenge Mazingira ya kuwarudia au kuachana na kazi hiyo kama ikinishinda. Kufika kazini nilikutana na binti mrembo na mzuri, sikubabaika sana nilimuona wa kawaida..... Siku zilipokwenda tukaanza kuwa na hisia za mapenzi juu yetu.... Aliniambia ana mchumba wake amemuacha Bukoba na Mimi nilimwelekeza familia yangu iko Songea.... Wakati huo tuko Arusha kikazi...... Kweli tukawa wapenzi kwa Siri na Ikifika Likizo kila mtu anaheshim mahusiano ya mwenzake.... Baada ya miez mitatu mdada alinijuza kwa busara sana anahisi ni mjamzito.... Nilivuta pumzi.... Tukakubaliana tukapime.. Kweli alikuwa ni mjamzito.... Lahaula... Ikiwa imebaki miezi sita tu ili akafunge ndoa na mchumba wake Huyo wa Bukoba..... Tukajadili tuitoe mimba hiyo ili kuzinusuru ndoa zetu, Japo tulijua ni dhambi kwa Mungu na jamii .... Japo alisisitiza yeye kabaki na mama pekee na mama alimuasa "ukipata ujauzito bila kutarajia... Chonde Chonde usitoe yatakukuta makubwa"... Kwa msaada wa mtaalam wa afya tukakubaliana tujaribu... Kwel tukafanya.... Kuja kucheki ultra sounds..... Mimba haikutoka na binti akaugua pomoni... Zaidi kumbe alikuwa na Maralia iliyojificha na pia upungufu wa damu... Hivyo vyote vikawa juu.. Damu Ilikuwa 5 ya 11 na Maralia... Takriban 11... Lahaula... Mimi ndo pekee niliyekaribu nae hapa Arusha.... Nikamuuguza hospital ya Mkoa kwa muda wa wiki na nyumbani wiki hadi akapona kabisa.. Nikiwa hoi hadi kitambi kuisha.... Yeye alinambia neno moja tu "Nimeamini unanipenda"..... Uzuri Ilikuwa kipindi cha Likizo Hivyo wote tulichelewa kwenda kwenye familia zetu.... Inshu ikawa ujauzito una miezi minne... Atamwambia nini mama yake ambae ni mjane na mboni yake ni yeye pekee... .. Koo za mchumba wake na za binti zimeshaanza kuwa Karibu kwa sababu ya vijana wao.... . Mipango ya harusi inaendelea.... Nikamsihi.. Aende Bukoba akamwambie Ukweli mpenzi wake kuwa alichepuka na ni mjamzito, pia aliugua muda mrefu, na hatua atakazo chukua basi Itakuwa imepangwa....... Kila hatua alinijuza kuwa kamweleza mchumba wake yote...... Ila mchumba wake alilia sana kwa nini alimsaliti!.... Baadae akampa sherti moja kuwa wafunge ndoa haraka sana kabla hajajifungua. Kweli ndoa iliandikishwa.... Kadi na kamati vikatengenezwa.. Mipango ya harusi ikafanyika.... Ulikuwa ni usiku wa kiza.... Totoro..... Mida ya Saa nane na robo usiku .... Binti Alinipigia simu akiwa analia..... Kuwa tumbo linamuuma.... Na anapelekwa Hospital... Kweli alipelekwa na kupewa kitanda. .. Kufika asubuhi Saa nne Alinipigia simu akinieleza.. Chupa ya uzazi imepasuka... Na kufika Saa saba na nusu mchana akajifungua kwa operation..... Saa kumi jioni alinipigia simu kwa furaha akasema amejifungua mtoto wa kiume..... Nikampa pole na Hongera..... Usiku wake alinijuza nitoe jina la mtoto nami Nilifanya Hivyo kwa kumpa jina la Baba yangu mzazi... Kumbuka Yuko hospital na zimebaki siku Tatu ifike siku ya ndoa na Ndugu wa mbali wameshaanza kusogea.... Ukoo ulipokaa wakaamua... Binti ajikaze na ndoa ifungwe maadam amejifungua tayar..... Kweli kesho yake wakaomba ruhusa na kutoka hospital.... Ndoa ikafungwa.... Nami Nilimuagiza best friend japo ni mbali Bukoba...... Hadi Arusha, nae akashiriki Maelezo ya jamaa yangu ni kuwa ... Aliia sana binti.. Hasa alipokuwa akimuona yeye.... Kama mtu ambae hakufurahia ndoa hiyo... .. Zoezi likaisha... Kikubwa nilichokiona ni kuwa ndoa yake haikumbadili kitu.. Bado alipenda sana mawasiliano nami..... Nilijitahidi kumzuia.... Lakini wapi.... Kwangu niliacha kabisa kumpigia ila yeye ni lazima moja mara tatu.... Kwamba asubuhi lazima apige, mchana apige na jion hata message.... Ilibidi nimpokee kwa kuwa sasa ni mzazi mwenzangu..... Japo nilimuomba Mungu tusifanye tena mapenzi nae kwani ni mke wa Mtu sasa..... Baada ya muda wakaja na mumewe Arusha mimi nikiwa Likizo .... Kuna jiran yangu alikuwa akimtaka sana kimapenzi binti yule nami binti alinambia..... Akamkuta mumewe na kumpa A -Z juu ya mahusiano yangu na binti Huyo ... Kwani kabla tulikuwa tunafanya kazi ofisi moja na ofisi ilitupa nyumba moja...... Kwa kugawana vyumba.... Kiukweli Ilikuwa nyumba kubwa ya vyumba vinne na Sebule.... Japo iliachanishwa na kuta flani ila geti moja.. Tulikuwa tunaishi watatu.... Mimi, Binti na Mfanyakaz mwenzetu...... Hivyo kwa mgeni lazima angejua lazima ni mke wa jamaa yangu au wangu...... Tulikula na kupika pamoja....... Alipopata Habari mumewe Alianza kunitumia message za vitisho..... Nilikauka sikujibu.... Baada ya muda niliona nikikaa kimya haita nisaidia.... Siku moja nilimpigia na kumuomba tuzungumze kwa kirefu..... Na ikawa....... Kweli.. Tuliongea mengi kwa muda wa masaa matatu na yeye aliridhika ila nilimueleza mimi ni binadamu na niliteleza kuwa na mahusiano na binti Huyo kabla hajaoa... Hivyo ni Marafiki tu kwa sasa na ni mfanyakazi mwenzake.... Jamaa akadai.... Tusaidiane kumtafutia binti uhamisho Aende Bukoba..... Tukaweka mipango..... Japo nikamtahadharisha...... Kuwa aliyempa taarifa ni mtu mzuri ila nae alikuwa anamhitaji binti..... Tukapanga kukutana.. Pia akanipa condition nimjibu yule ni mtoto wangu au Vipi.... Nikamwambia mtoto mwenye Siri ni mama.. Hivyo ambane mkewe Atamwambia, japo hitimisho ikawa nimbane mkewe pia akinijibu nae nimwambie ... Wakati Nataka nianze safari.... Baba yangu mzazi akafariki ikabidi niahirishe safari ya kwenda kazini na niende msibani..... Iliniuma kwa kuwa mamangu mzazi alitangulia nikiwa primary....... Tulizika na nikaona ni mwaka wa mkosi Kwangu........ Why always me..... Kabla sijarud kazini ikatoka barua nyingine ya kwenda kuripoti katika ofisi zetu mjini Moshi...... Nikaenda kuripoti..... Na kupanga mipango ya kazi..... Nikiwa njian kufuata familia yangu ambayo mambo Haya Bado hawana taarifa nayo....... Ninavyomfahamu mke wangu akisikia naongea na simu ya Mwanamke hata Dada yangu anaumwa.... Akigundua Nina mtoto na mke wa Mtu Itakuwaje.... Najitajidi sana kumsisitiza binti ampende mumewe pia nikagundua.... Mume anaendeshwa na mke mana message za mwanzo nilimfowardia na kumueleza aache kunitafuta kila mara labda kwa shida za mtoto au kubwa.... Kumbe ikawa Kesi tena jamaa akaomba msamaha kuwa hatanipigia tena..... KIBAYA ZAIDI....... Juzi jamaa Ameanza kunitumia message za vitisho tena ..... Nataman kufanya mengi.... Ila nashindwa Nianzie wapi..... Mbele giza.... Nilipo giza..... Naithamini damu yangu... Ya jina la Baba yangu mzazi aliyetangulia mbele yake hivi punde ....... Siwez itupa kwani nikifanya Hivyo napo kwa binti ni kilio kingine.... Mana inaonesha jamaa hampendi hata kidogo mtoto Huyo .... MAWAZO YENU WADAU.......

jamani sijaelewa mbona kama.umebambikiwa hiyo mimba wewe mara mimba inmkez minne so alijifungua njiti
 
Mgiriki.... Nashkur kwa ushauri wako......... Mkuu. .... Ila mimi najiona shujaa kushare TATIZO langu na jamii..... Ni wachache ambao wanauwezo huu... Wengi wanakaa kimya na wanaumia Zaidi.. Pili... Kumbuka tulipokutana nae first time Sio kwamba alikuwa amehalalishwa..... Hata pete ya uchumba hakunionesha.... Ila walikuwa ni wapenzi wenye malengo. .... Tatu Bado tunaishi Ninaamini wewe umekosa mengi kuliko mimi sema umejua mapema yangu kwa kuwa mimi ni mwepesi wa kutubu mbele ya jamii..... Amina

mkuu ungekuwa muungwana ungeomba ushaur kabla ya kuanza mahusiano na huyo bint lakn ww leo unajifanya muungwana kwa kusema kuwa unashare mawazo ni baada ya maji kukufika shingon...
Na kumbuka kila aangamizaye kwa upanga ataangamia kwa upanga na muosha huoshwa.. Ila mm nakushaur tu mshukur sanna mungu na usiache kumwomba kwasababu ungekutana na mtu mwenye akili kama yangu adhabu yako ilikuwa risasi tatu kifuan
 
duuuh,,,hii ni hadith au mkasa!,,,kusoma inabd miwan,,,,any way pole kwa yote ila uyo binti atasumbuka sana na ww coz anaonekana kukupenda ww na sio uyo mme wake,,,jitahd ku-keep distance itasaidia angalau

Magombe...... Nashkur.. Ntajitajidi zaid ya hapa.. I will try for my next level
 
Aiseee sijawahi kutoa comment huku ila Leo inanibidi kwanza nikuulize swali unampenda mkeo au huyo mzazi mwenzio?Hapo cha muhimu kaa chini uongee na mkeo umwambie kila kitu,yeye ndo ataamua nini cha kufanya ni bora umwambie mapema kuliko aje kusikia kwa mtu mwingine

Naipenda familia yangu........ Sintosita kumwambia...... Ngoja nijipange nimwambie......
 
jamani sijaelewa mbona kama.umebambikiwa hiyo mimba wewe mara mimba inmkez minne so alijifungua njiti

Naithibitisha ni ya Kwangu kwa namna tarehe zilivyooana..... Pia ktk kila hatua alinijuza....... Meanwhile alikuwa mkweli kwenye baadh ya mambo.... Inanipa iman......
 
mkuu ungekuwa muungwana ungeomba ushaur kabla ya kuanza mahusiano na huyo bint lakn ww leo unajifanya muungwana kwa kusema kuwa unashare mawazo ni baada ya maji kukufika shingon...
Na kumbuka kila aangamizaye kwa upanga ataangamia kwa upanga na muosha huoshwa.. Ila mm nakushaur tu mshukur sanna mungu na usiache kumwomba kwasababu ungekutana na mtu mwenye akili kama yangu adhabu yako ilikuwa risasi tatu kifuan

Sawa mkuu...... Nimeishi na watu wengi sana mpaka nimefika umri huu...... "As people are equal but not the same "....... Be blessed
 
Wewe achana nao tu ilitokea kama ajari basi usilazimishe kutoa matumizi ya mtoto akati dada wa watu wameoana badilisha namba ya simu na udil na mambo yako mkiendelea kuwasiliana jamaa anaweza kmudhuru mtoto, au mama na hata wewe pia
 
Shamkware...... Nashukuru kwa ushauri wako........ Nitaufanyia kazi......
 
Naipenda familia yangu........ Sintosita kumwambia...... Ngoja nijipange nimwambie......

Ukisema umejimaliza mi naona piga kimya tu maana uzuri umehamishwa kazi kutoka Arusha kwenda moshi. Na binti si karudi bukoba? Wewe kausha tu maana ukiendelea kuongea na huyo binti jamaa anajaa sumu na atakuja kuwafanyia kitu kibaya wote watatu wewe mwanao na mkeo
 
Tafuta muda mzuri umweleze mkeo kwa upole kbsa naamini atakusikia, kama mfuko unaruhusu nendeni mbali mahali ambapo mtakuwa wawili TUBU KWA MUNGU NA KWA MKEO, jitahidi kwa nmna zote kukata mawasiliano na huyo bidada!! angalia namna nzuri ambayo itamfikia huyo mtoto lakini pia haitakuwa kikwazo kwa pande zote mbili!
 
Poa mkuu mi Nakuelewa............. Nashkur kwa ushauri
 
Tafuta muda mzuri umweleze mkeo kwa upole kbsa naamini atakusikia, kama mfuko unaruhusu nendeni mbali mahali ambapo mtakuwa wawili TUBU KWA MUNGU NA KWA MKEO, jitahidi kwa nmna zote kukata mawasiliano na huyo bidada!! angalia namna nzuri ambayo itamfikia huyo mtoto lakini pia haitakuwa kikwazo kwa pande zote mbili!

Nashkur kwa ushauri....... Kuntu.......
 
una uhakika gani

Kwel ni ngumu mwanamama ..... Lakini hili suala mara nyingi.... Ni kuaminiana..... Coz Ukisema Hivyo.... Inawezekana hata wa ndoa unakuta mtu Sio wako...... Na plan ya DNA ni mapema sana.....
 
Ayse nashindwa kushauri maana watumishi wengi wa umma ndo maisha yetu ukihamishwa mkoa unaacha familia ili ukatengeneze njia halafu tunakumbana na majaribu kama hayo. Ila kaka ulipopuuza condom ndo ulikaribusha tatizo. Siku zote mbwana weka condom kwenye begi kwa dharura kama silaha hasa ukiona kuna mazingira kama hayo maana wakati mwingine kichupa kikijaa na binti mzuri naye akijilengesha tunashindwa. Ila kosa lingine ulilofanya ni kukubali kutoa jina la baba yako kuwa la mtoto. Hiyo itaendelea kukuuma. Pia shukuru umehamishwa ofisi ili uwe mbali na huyo binti. Kuhusu vitisho zungumza na huyo binti ujue jamaa anawasiwadi gani kuhusu mtoto pia muwe na jibu 1 kwa jamaa wewe na huyo binti. Kama binti ataridhia kumuweka jamaa wazi basi uwe tayari kulea mtoto kwa uwazi umjulishe wife maana utaficha hadi lini wakati unataka mtoto na huku unatishiwa? Mfano kesho ukiuawa na huyo jamaa wife atawaeleza nini watoto wenu na hata ndugu zako?
 
Jenerali...... That's why ure General........ Hizi kazi. .... Itabidi niongeze umakini..... Nashkur kwa ushauri mkuu....
 
namba 1. wewe ndo ulikuwa na hisia nae na sio kwamba mlikuwa na hisia tengua kauli hapo!!
namba 2. jela ilikuwa inakuita ila ukakata rufaa bahati yako!!!
namba 3 . hv ungekuwa ni wewe mke wako umemgharamia vya kutosha halafu anakuletea mimba ukireflect mtoto alivyotengenezwa ungejisikiaje!!!?
namba 4. nakushauri nenda polis kajihami na huyo mtu kuwa anakuletea vitisho atakutumia watu wakuharibie ni hayo tu!!!

Tena huyo jmaa ni mpole sana,,mm ningeshakufanya kitu mbaya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom