Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Mh. Mnyika,nilikufahamu tangu ulipogombea Ubunge wa Ubungo kwa mara ya kwanza mwaka 2005 dhidi ya Charles Keenja. Wakati huo nilikuwa mwanachuo wa mwaka wa kwanza UDSM nikichukua Sheria. Ingawa sikuwa mpigakura wako kwakuwa nilijiandikisha Kibaha,nilikuunga mkono. Ukiwa kijana na mwanafunzi mwenzetu UDSM,tulijivunia uwepo na ugombea wako.
Mh. Mnyika,mwaka 2010 nilihamisha kituo changu cha kupígia kura kwa ajili yako. Nikahamisha toka Kibaha hadi Ubungo. Nikakupigia kura Nkrumah Hall UDSM nikitambua uwezo,nia na sababu zako za kuwa Mbunge wa Ubungo. Safari hii nikiwa mwajiriwa wa UDSM. Ukamshinda Hawa Ng'umbi wa CCM na kuwa Mbunge.
Tangu kuwa Mbunge,hukuwahi kutuangusha kama vijana katika hoja na msimamo wa kitaifa. Umekuwa ukiongozwa na kauli zithibitikazo kwa nyaraka na tafiti mbalimbali. Hakika vijana wa Tanzania unatuwakilisha vyema na tunajivunia kukuchagua kuwa Mbunge wa Ubungo.
Nakushauri mambo mawili. Mosi,uanze upya au umalizie elimu ya juu yako. Tunahitaji ubongo wako ulioimarika zaidi kielimu. Elimu ya juu kwa nafasi na uwezo wako wa kiuongozi haiepukiki. Pili,endelea kuwatumikia wananchi wako wa Ubungo na Tanzania kwa ujumla kwa weledi,uwezo na bidii uliyojaaliwa. Asante