Ushauri wa wazi kwa J. J. Mnyika (Mb)

Ushauri wa wazi kwa J. J. Mnyika (Mb)

Msilete ujanja ujanja kama ana muda akamalizie shule yake, mwenzie Kafulila amemaliza licha ya kwamba alikuwa anahudhuria vikao vya bunge. Tulikuwa tunapiga kelele wabunge wz CCM walipoondoa kipengere cha elimu kama kigezo cha kuchaguliwa kuwa mbunge. Wengi hapa tunaamini JJ Mnyika ana uwezo wa kushika nyadhifa kubwa huko mbele kama Urais tunataka wakati huo ndio aanze kusoma? Au mwakani ikitokea Chadema na Ukawa wanaingia Ikulu hatuoni kwamba licha ya uwezo wake na akili ya kuzaliwa bado kiwango cha Elimu nacho kitakuwa kigezo kwenye uteuzi wa mawaziri e.t.c?
 
Madhara ya John Mnyika kukosa degree ni yeye mwenyewe kuanza kuwa mjanja mjanja. Ukiingia kwenye website ya bunge CV ya mnyika haina chochote kwa miaka kadhaa sasa. Watu wengi wanadhania mnyika ni graduate wa udsm. Ingawa ukweli ni kwamba Mnyika siyo graduate wa University.

Parliament of Tanzania
 
Elimu sio kigezo cha kuwa kiongozi wa CHADEMA. Ndio maana Mwenyekiti Mbowe ni Form six leaver with zero division.
 
Mnyika ana simu,email na blogu,,ungemtumia huko ingekuwa busara sana. Au ungeomba miadi nae kumweleza haya. Sawa atakuwa kakusikia kaka.
 
Kila kitabu na zama zake. Nakubaliana na wewe kuwa kuna watu wamefanya makuu bila elimu kubwa, lakini hizi si zama za kuenzi hilo suala kwani hakuna vikwazo vya kielimu kama zamani. Kwa umri wa Mnyika bado anayo nafasi ya kujiendeleza zaidi kielimu ili kuendeleza kipaji chake. Asiridhike na mawazo kuwa elimu sio lazima.No Mnyika Please! elimu ni muhimu sana kwa kizazi cha sasa usije kubweteka itakukosti baadae.


Sijakuelewa kabisa-Itamkosti kwenye lipi na baadaye ipi-kwani umesikia mwisho wa kusoma ni lini na umri gani?
Suala hapa ni malengo na kipaumbele na nini unatamani maishani kwako kabla huajafikia umri fualani uweumekifankisha au umekijaribu kukifanya kikakwama au kufikika hatua fualani kabla nguvu ya kufanya hivyo haijaisha/umri.



Naoungana na Petro, Mnyika sasa hivi nafasi za kujiendeleza kielimu ni nyingi mno. hata kama UDSM walikubania bado unayo nafasi kubwa kwenye vyuo nvingine ndani na nje ya nchi. Changamkia fursa uliyopata before it is too late!

Hakuna hoja kuhusiana na Nafasi au wapi akasomee na nini cha kusoma.
 
Tatizo nadhani hujamsikia wala kumuona mnyika akijenga hoja na ufahamu wake wa mambo. Ni zaidi ya graduate. Halafu webu fuatilia kijana aliyegundua facebook hakumaliza degree. Achana na vinjwa wewe . Angalia prof. TIBAIJUKA anavyojitetea na 1.6 biln vituko tu
 
Nilitoa chagizo kwamba maisha ya mnyika katika harakati za siasa hazitofautiani sana na hayati prof kighoma malima nadhani mtu ambaye amepitia historia ya mwanazuoni huyo hawezi kumbeza mnyika hata kidogo
 
Elimu sio kigezo cha kuwa kiongozi wa CHADEMA. Ndio maana Mwenyekiti Mbowe ni Form six leaver with zero division.

Mkuu MSALANI Mbowe ni form 4 leaver tuweke kumbukumbu sawa.Uenyekiti amepewa zawadi na baba mkwe.
 
Last edited by a moderator:
Nilimwandikia Mh. Rais waraka wa kuleta maadili mema nchini ambapo ingekuwa mwanzo mpya kama utasoma kwa ukamili attachment katika habari zangu ndani ya JF yenye kichwa MH. KIKWETE MTIKISIKO WA 4 KULIKUMBA TAIFA.

Ndani ya waraka huo wa tarehe 27/10/2012 ushauri nilioshauri utangazwe na rais ni: (Nanukuu hapa chini)

1. NJIA YA KULETA AMANI NA UTENGAMANO WA TAIFA


Mungu wa Kweli Yehova anaagiza kuwa: “Ukiwa Rais na kabineti yako ya utawala na ushauri; kwa pamoja mpitishe azimio la kusamehe na kufuta kesi zote ambazo zinahusikana na migogoro ya kidini, kisiasa, uhujumu uchumi, ufisadi, migomo ya wafanyakazi, wanafunzi na hata kesi ambazo zinakabili watu ambao wamehusika katika migogoro ya kikabila na ardhi.” Mungu akimaanisha watu watakao husika katika zoezi hili la kusamehewa ni katika kesi ambazo zinasimamiwa na Jamhuri siyo katika kesi zinazohusisha mtu na mtu. Pia, msamaha utahusika kwa wale wote ambao tayari wanatumikia vifungo kwa sababu ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu, wanapaswa kufunguliwa na kuwekwa huru. Kisha, utoe tamko kwamba serikali itapitisha sheria kali hivi karibuni kwa wote watakaotenda au kusababisha matatizo mapya yaliyotajwa hapo juu.

MWAROBAINI WA KUKOMESHA MATATIZO HAYO HAPO JUU UNATOLEWA NA MIFANO MIWILI INAYOPATIKANA KATIKA BIBLIA:

i). Andiko la Luka 19:2-10 linalosema: “Sasa kulikuwa na mwanaume anayeitwa Zakayo; naye alikuwa mkuu wa wakusanya kodi, na alikuwa tajiri. Basi, alikuwa akitafuta kuona Yesu huyu ni nani, lakini hangeweza kwa sababu ya umati, kwa sababu alikuwa mfupi. Kwa hiyo akakimbia mbele na kupanda mforsadi-tini kusudi amwone, kwa sababu alikuwa karibu kupitia njia hiyo. Sasa Yesu alipofika hapo, akatizama juu na kumwambia: “Zakayo, shuka haraka, kwa maana leo lazima nikae katika nyumba yako.” Ndipo akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa shangwe. Lakini walipoona hilo, wote wakaanza kunung’unika, wakisema: “Ameingia apate kukaa pamoja na mwanamume mtenda-dhambi.” Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana: “Tazama! Nusu ya mali zangu, Bwana mimi nitawapa masikini, na chochote nilichomnyang’anya mtu yeyote kwa shitaka la uwongo nitarudisha mara nne.” Ndipo Yesu akamwambia: “Leo wokovu umekuja kwenye nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Abrahamu. Kwa maana Mwana wa Binadamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea.”

ii). Pia, andiko la 2Wafalme 6:15-23 linasema: “Wakati mhudumu wa yule mtu wa Mungu wa kweli (Elisha) alipoamka asubuhi na mapema, akaenda nje, na, tazama, hapo jeshi lilikuwa limelizunguka jiji kwa majeshi na magari ya vita. Mara moja mtumishi wake akamwambia: “Ole, bwana wangu! Tutafanya nini? Lakini yeye akasema: “usiogope, kwa maana wale walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.” Na Elisha akaanza kusali na kusema: “Ee Yehova, tafadhari fungua macho yake, ili aone.” Mara moja Yehova akafungua macho ya yule mtumishi, hivi kwamba akaona; na, tazama! Lile eneo lenye milima lilikuwa limejaa farasi na magari ya vita ya moto kumzunguka Elisha pande zote.”

Walipoanza kushuka kumwendea, Elisha akaendelea kusali kwa Yehova na kusema: “Tafadhali, lipige taifa hili kwa upofu.” Basi yeye akawapiga kwa upofu kulingana na neno la Elisha. Sasa Elisha akawaambia: “Hii siyo njia, na hili silo lile jiji. Nifuateni, na acheni niwaongoze kwa yule mtu mnayemtafuta.” Hata hivyo akawaongoza kwenda Samaria.

Na ikawa kwamba mara walipofika Samaria, ndipo Elisha akasema: “Ee Yehova, fungua macho yao waone.” Yehova akafungua macho yao mara moja, nao wakaona; na, tazama, walikuwa katikati ya Samaria. Sasa mfalme wa Israeli akamwambia Elisha mara alipowaona: “Je, niwapige, je, niwapige, baba yangu?” Lakini akasema usiwapige. Je, unawapiga wale ambao wewe umewachukua mateka kwa upanga wako na upinde wako? Weka mkate mbele yao ili wale na kunywa, waende kwa bwana wao.” Basi akawaandalia karamu kubwa; nao wakaanza kula na kunywa, kisha akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikundi vya waporaji vya Wasiria havikurudi tena hata mara moja katika nchi ya Israeli.”

Kwa hiyo maandiko yote mawili yana maana kubwa au mfano mkubwa kwa makundi yote ambayo yametajwa hapo juu ambayo yatapata msamaha wa serikali. Ni kwamba Yehova ametoa agizo la msamaha kwa sababu msamaha huo utawahukumu wahusika katika nafsi zao; kwa sababu watakapokuwa wakifikiria rehema walizotendewa, hawatarudia makosa yao ya zamani. Ndivyo alivyofanya Zakayo baada ya kumkaribisha Yesu alijisikia hatia juu ya ufisadi na rushwa alizokuwa akipokea naye akaahidi kuwalipa aliowadhurumu, kusaidia masikini n.k. Vivyo hivyo msamaha ambao serikali imetoa kwa watuhumiwa utawafanya wahusika kuwa watu wazuri katika jamii ili kulipia matendo waliyosababisha na itachochea jamii kuchukia matendo hayo. Na katika mfano wa pili, tunaona Wasiria waporaji baada ya kufanyiwa matendo mema badala ya mabaya; walipata somo kubwa sana na hawakurudi tena kuwasumbua Waisraeli, hii, ikiwa ni sehemu ya kulipia matendo mema waliyotendewa badala ya mabaya.

HITIMISHO: Ushauri huu ungefuatwa 2012 kusingekuwa na ufisadi wa Escrow au ufisadi mwingine

Mheshimiwa sasa unaboa inawezekana ukawa kweli nabii lakini unafosi kukubalika. Kila kwenye thread yenye comments nyingi unaingizia hii post yako. Siyo vizuri unatafuta watu wasio waamini kukuvunjia heshima ama kushawishi watu waanze kuamini kuwa wewe ni mchumia tumbo. Mimi sasa naanza kuamini.
NABII NENO LAKE NI MOJA TU. HUWA HABEMBELEZI.
 
Kama wananchi wanamhitaji kwa elimu hiyo hiyo aliyonayo ni vema akawatumikia wananchi hao. Akina Professor Muhongo, Tibaijuka mbona wanalikoroga na kuboronga ingawa wana usomi kuliko wa Mnyika?
 
Back
Top Bottom