Ushauri wa wazi kwa J. J. Mnyika (Mb)

Ushauri wa wazi kwa J. J. Mnyika (Mb)

Mkuu Mingoi,heshima ni kitu cha bure. Nimekuwa nikisema mara kwa mara kuwa mimi si huyo mnayeamini ni mimi. Mimi sina haja ya kuwa na ID bandia kwakuwa najiamini na nayaamini mawazo yangu.

Mkuu Invisible,tafadhali mpatie Mingoi haki yake kwa name calling na kwa uzushi.
Wapi amekutaja moja kwa moja? Acha kujistukia, Mchezo wenu wa kutumia ID mbili mbili umeshashtukiwa!
 
Kumbe ndio wale wale..

ImageUploadedByJamiiForums1419503626.994967.jpg
 
Wapi amekutaja moja kwa moja? Acha kujistukia, Mchezo wenu wa kutumia ID mbili mbili umeshashtukiwa!

Huyo kada wenu mtafuteni huko huko. Mlioko MSALANI ndio mnaopenda kutumia ID bandia. Mimi najiamini na ni jasiri sana.

Unajitafutia ban bure MSALANI kwa uzushi unaourukia. Mkuu Invisible husika hapa
 
Last edited by a moderator:
Mtuo mada tunaomba utupe cv ya John Mnyika mbunge wetu plz!!
 
Kweli mkuu, hata hapa kijiweni kwetu-jana watu walikuwa wanalijadili hilo jambo. Kama kweli UDSM walimdisco kwa sababu za kisiasa, walio husika walaaniwe.

Mm ningeomba asome nje ya nchi mf. USA au UK. Akisha graduate aweke vyeti vyake hapa. Maana mtu kama Nape Nauye anaweza kukurupuka tu na maneno mengi (Japo yeye ni mtu wa Four, Zero na Vicertificate vingi) wakati Mnyika kashahitimu kupitia Online/distance learning. Naunga mkono hoja.
 
Kwani Mnyika hana digrii? Binafsi naona uelewa wake na jinsi anavyochambua masuala mbalimbali ni kama ana Masters vile. Kama kweli hana ni bora asome aipate - lakini isiwe digrii fake kama ya akina Agustine Mrema na wengineo
 
Mh. Mnyika,nilikufahamu tangu ulipogombea Ubunge wa Ubungo kwa mara ya kwanza mwaka 2005 dhidi ya Charles Keenja. Wakati huo nilikuwa mwanachuo wa mwaka wa kwanza UDSM nikichukua Sheria. Ingawa sikuwa mpigakura wako kwakuwa nilijiandikisha Kibaha,nilikuunga mkono. Ukiwa kijana na mwanafunzi mwenzetu UDSM,tulijivunia uwepo na ugombea wako.

Mh. Mnyika,mwaka 2010 nilihamisha kituo changu cha kupígia kura kwa ajili yako. Nikahamisha toka Kibaha hadi Ubungo. Nikakupigia kura Nkrumah Hall UDSM nikitambua uwezo,nia na sababu zako za kuwa Mbunge wa Ubungo. Safari hii nikiwa mwajiriwa wa UDSM. Ukamshinda Hawa Ng'umbi wa CCM na kuwa Mbunge.

Tangu kuwa Mbunge,hukuwahi kutuangusha kama vijana katika hoja na msimamo wa kitaifa. Umekuwa ukiongozwa na kauli zithibitikazo kwa nyaraka na tafiti mbalimbali. Hakika vijana wa Tanzania unatuwakilisha vyema na tunajivunia kukuchagua kuwa Mbunge wa Ubungo.

Nakushauri mambo mawili. Mosi,uanze upya au umalizie elimu ya juu yako. Tunahitaji ubongo wako ulioimarika zaidi kielimu. Elimu ya juu kwa nafasi na uwezo wako wa kiuongozi haiepukiki. Pili,endelea kuwatumikia wananchi wako wa Ubungo na Tanzania kwa ujumla kwa weledi,uwezo na bidii uliyojaaliwa. Asante

Na bhange apunguze.. aache tilalila awasaidie wananchi wake wa ubungo kero ya maji ni moja kati ya ahadi alizotoa na kumpa ushindi.
 
Wewe jembe na yeye jembe,wote nyie majembe hakikisheni anabaki 2015.
 
Nilimwandikia Mh. Rais waraka wa kuleta maadili mema nchini ambapo ingekuwa mwanzo mpya kama utasoma kwa ukamili attachment katika habari zangu ndani ya JF yenye kichwa MH. KIKWETE MTIKISIKO WA 4 KULIKUMBA TAIFA.

Ndani ya waraka huo wa tarehe 27/10/2012 ushauri nilioshauri utangazwe na rais ni: (Nanukuu hapa chini)

1. NJIA YA KULETA AMANI NA UTENGAMANO WA TAIFA


Mungu wa Kweli Yehova anaagiza kuwa: “Ukiwa Rais na kabineti yako ya utawala na ushauri; kwa pamoja mpitishe azimio la kusamehe na kufuta kesi zote ambazo zinahusikana na migogoro ya kidini, kisiasa, uhujumu uchumi, ufisadi, migomo ya wafanyakazi, wanafunzi na hata kesi ambazo zinakabili watu ambao wamehusika katika migogoro ya kikabila na ardhi.” Mungu akimaanisha watu watakao husika katika zoezi hili la kusamehewa ni katika kesi ambazo zinasimamiwa na Jamhuri siyo katika kesi zinazohusisha mtu na mtu. Pia, msamaha utahusika kwa wale wote ambao tayari wanatumikia vifungo kwa sababu ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu, wanapaswa kufunguliwa na kuwekwa huru. Kisha, utoe tamko kwamba serikali itapitisha sheria kali hivi karibuni kwa wote watakaotenda au kusababisha matatizo mapya yaliyotajwa hapo juu.

MWAROBAINI WA KUKOMESHA MATATIZO HAYO HAPO JUU UNATOLEWA NA MIFANO MIWILI INAYOPATIKANA KATIKA BIBLIA:

i). Andiko la Luka 19:2-10 linalosema: “Sasa kulikuwa na mwanaume anayeitwa Zakayo; naye alikuwa mkuu wa wakusanya kodi, na alikuwa tajiri. Basi, alikuwa akitafuta kuona Yesu huyu ni nani, lakini hangeweza kwa sababu ya umati, kwa sababu alikuwa mfupi. Kwa hiyo akakimbia mbele na kupanda mforsadi-tini kusudi amwone, kwa sababu alikuwa karibu kupitia njia hiyo. Sasa Yesu alipofika hapo, akatizama juu na kumwambia: “Zakayo, shuka haraka, kwa maana leo lazima nikae katika nyumba yako.” Ndipo akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa shangwe. Lakini walipoona hilo, wote wakaanza kunung’unika, wakisema: “Ameingia apate kukaa pamoja na mwanamume mtenda-dhambi.” Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana: “Tazama! Nusu ya mali zangu, Bwana mimi nitawapa masikini, na chochote nilichomnyang’anya mtu yeyote kwa shitaka la uwongo nitarudisha mara nne.” Ndipo Yesu akamwambia: “Leo wokovu umekuja kwenye nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Abrahamu. Kwa maana Mwana wa Binadamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea.”

ii). Pia, andiko la 2Wafalme 6:15-23 linasema: “Wakati mhudumu wa yule mtu wa Mungu wa kweli (Elisha) alipoamka asubuhi na mapema, akaenda nje, na, tazama, hapo jeshi lilikuwa limelizunguka jiji kwa majeshi na magari ya vita. Mara moja mtumishi wake akamwambia: “Ole, bwana wangu! Tutafanya nini? Lakini yeye akasema: “usiogope, kwa maana wale walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.” Na Elisha akaanza kusali na kusema: “Ee Yehova, tafadhari fungua macho yake, ili aone.” Mara moja Yehova akafungua macho ya yule mtumishi, hivi kwamba akaona; na, tazama! Lile eneo lenye milima lilikuwa limejaa farasi na magari ya vita ya moto kumzunguka Elisha pande zote.”

Walipoanza kushuka kumwendea, Elisha akaendelea kusali kwa Yehova na kusema: “Tafadhali, lipige taifa hili kwa upofu.” Basi yeye akawapiga kwa upofu kulingana na neno la Elisha. Sasa Elisha akawaambia: “Hii siyo njia, na hili silo lile jiji. Nifuateni, na acheni niwaongoze kwa yule mtu mnayemtafuta.” Hata hivyo akawaongoza kwenda Samaria.

Na ikawa kwamba mara walipofika Samaria, ndipo Elisha akasema: “Ee Yehova, fungua macho yao waone.” Yehova akafungua macho yao mara moja, nao wakaona; na, tazama, walikuwa katikati ya Samaria. Sasa mfalme wa Israeli akamwambia Elisha mara alipowaona: “Je, niwapige, je, niwapige, baba yangu?” Lakini akasema usiwapige. Je, unawapiga wale ambao wewe umewachukua mateka kwa upanga wako na upinde wako? Weka mkate mbele yao ili wale na kunywa, waende kwa bwana wao.” Basi akawaandalia karamu kubwa; nao wakaanza kula na kunywa, kisha akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikundi vya waporaji vya Wasiria havikurudi tena hata mara moja katika nchi ya Israeli.”

Kwa hiyo maandiko yote mawili yana maana kubwa au mfano mkubwa kwa makundi yote ambayo yametajwa hapo juu ambayo yatapata msamaha wa serikali. Ni kwamba Yehova ametoa agizo la msamaha kwa sababu msamaha huo utawahukumu wahusika katika nafsi zao; kwa sababu watakapokuwa wakifikiria rehema walizotendewa, hawatarudia makosa yao ya zamani. Ndivyo alivyofanya Zakayo baada ya kumkaribisha Yesu alijisikia hatia juu ya ufisadi na rushwa alizokuwa akipokea naye akaahidi kuwalipa aliowadhurumu, kusaidia masikini n.k. Vivyo hivyo msamaha ambao serikali imetoa kwa watuhumiwa utawafanya wahusika kuwa watu wazuri katika jamii ili kulipia matendo waliyosababisha na itachochea jamii kuchukia matendo hayo. Na katika mfano wa pili, tunaona Wasiria waporaji baada ya kufanyiwa matendo mema badala ya mabaya; walipata somo kubwa sana na hawakurudi tena kuwasumbua Waisraeli, hii, ikiwa ni sehemu ya kulipia matendo mema waliyotendewa badala ya mabaya.

HITIMISHO: Ushauri huu ungefuatwa 2012 kusingekuwa na ufisadi wa Escrow au ufisadi mwingine

Aliyekufundisha kupost JamiiForums ametumaliza manake wewe unaingia popote pale na unabii wako, hata ambapo hoja ni tofauti wewe ni Unabii tu na Barua kwa Rais.

Jamani Joseph utakuwa kero muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom