Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za ghala (WRRB), yatoa mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi wa ghala

Apr 9, 2022
66
32
Mafunzo hayo yanayofanyika kila mwaka nchini yenye lengo la kuwajenga uwezo Watendaji wa Kampuni za waendesha ghala, Wasimamizi wa Ghala, Meneja Dhamana pamoja na washiriki binafsi yamefunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Ubungo Hashim Komba leo Tarehe 28 Agosti 2023, katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

IMG-20230828-WA0745.jpg

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mhe. Komba alieleza kuwa Mafunzo haya yanakwenda kuongeza heshima kwa watendaji wa ghala na kupelekea utoaji wa huduma bora kwa Wadau wote, vilevile ameitaka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utendaji ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Pia mafunzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu pamoja na Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji wa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Mary Fidelis.

IMG-20230828-WA0746.jpg

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye N. Bangu amesema kuwa lengo kubwa ni kuongeza tija katika ufanyaji kazi na matarajio ya mafunzo hayo ni kuhakikisha kazi zinafanywa kwa usahihi kwa kuzingatia sheria .

Aidha Mhe. Bangu ameongeza kuwa Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona ambavyo watatekeleza shughuli zao za kiserikali pia wamejitaidi kuingiza bidhaa mbalimbali kadiri sheria ilivyo waruhusu kufanya hivyo, Washiriki waliojitokeza kupata mafunzo haya watapatiwa cheti cha kufudhu usimamizi wa shughuli za uendeshaji Ghala ambacho kitatambuliwa na Bodi ya Stakabadhi za Ghala.

‘’Nilipofanya ukaguzi nilibaini changamoto mbalimbali kwenye maghala, anaeshikiliwa kwanza ni Meneja na Mkurugenzi anakuwa hayupo ukimuuliza Mkurugenzi anakuambia Meneja wangu ndio anaehusika, kwahiyo mda mwingine unakuta meneja hana Taharifa, hivyo natoa wito kwa Washiriki wote kuzingatia Mafunzo yanayotolewa ili kuwaongezea uwezo wa Kiutendaji. Alisema
 
Back
Top Bottom