Ushauri wa maisha utakaokufanya usikate tamaa

Vanlizerfx__

Senior Member
Jul 7, 2021
114
189
Habari wana Jamii forums

Kwenye maisha tunapitia changamoto nyingi ambazo kuna kuanguka na kukosa wa kukushika mkono, wa kukufariji hata wa kuona thamani yako hata kidogo.

Unakumbuka wakati ambao wewe ambaye ulikuwa unatoka kijijini kwenda mjini ni hali gani ambayo ulikuwa unajisikia? Unatamani japo ungekua wale wenye magari mazuri, maisha mazuri lakin unajipa moyo unajiona kama Elon musk wakati huna hata hela ya kula.

Weka uso wako kila wakati kuelekea jua na vivuli vitaanguka nyuma yako ni misemo inayotumika kuwapa moyo vijana wengi.

Wewe kama msomaji andika changamoto uliowahi kuipitia kwenye maisha ikataka kukufanya ukate tamaa lakini ukajipa moyo ukaishinda ili iwe fundisho kwa wengine.

Thread in a nutshell
 
Kuna vitu viwili unapaswa kuhakikisha viko sawa kabla ya kuanza harakati zako za utafutaji

1. Weka Mahusiano Mazuri Baina Yako na Mungu Wako
2. Hakikisha Uhusiano Wako Na Wazazi Wako Uko Vizuri na Kwamba Huwasahau Kwa Kila Hali.

Niamini Hakuna Nasema Hakuna Changamoto Itakujia Ukashindwa Kuivuka kwenye haya maisha.

Kuna kipindi niliachwa na Mwanamke nikapatwa na Stress Ila Namba 1 na 2 hapo Juu ndizo ziliniweka sawa sikutoka kwenye reli.

Baadae kuna mishe flani hivi nikaotea kwenye utafutaji wangu ilaniweka pazuri sana tu. Yule mwanamke akajuta sanaa baadae kwani alikua akisikia habari zangu. Ila ndio hivyo sijawahi rudia makombo / matapishi.

Niamini iko faida katika kuishi vizuri na watu...tabia na hulka yako ndio ina amua mwenendo wako wa maisha uwe vipi.

Thanks.
 
Bwana bwana...

Maisha ni kitu ingine kabisa asee.

Ngoja nisimulie kwa kifupi sana safari yangu ya maisha... Yaweza kuwatia moyo wengi wanaopitia haya niloyopitia / ninayopitia kwa sasa.

Bwana bwana asee... Ndoto yangu ilikuwa kuishi Arusha buana... Baada tu ya shule nikaanza safari ya kukamilisha ndoto yangu... Kwa bahati mbaya sikuwa na ndugu wala mtu ninayemfahamu Arusha...

Nilichofanya, kupitia kwa rafiki yangu mmoja nikaomba hifadhi kwa rafiki yake aliyekuwa anaishi ghetto yeye na mjomba wake...
Tulikuwa lika sawa kwa hiyo haikuwa tabu... Ingawa ilinishangaza kupokelewa na kuruhusiwa kuishi kwenye ghetto la mtu asiyenifahamu kabisa.

Nilipofika nilibahatika kupata ajira ya muda (maarufu kwa jina la "tempo" kwa tuliomaliza shule kusubiria nafasi ya kwenda chuo)... Mwenye ofisi aliniambia lazma nipige kazi kwa mwezi mmoja ili nijifunze kazi, akaahidi kunilipa pesa ya chakula kila siku... Kwa kuwa nilikwishajifunga mkanda wa safari, nikaanza ndoto katika nchi ya ugenini.

Nilipewa pesa ya chakula kwa takribani wiki moja na siku kadhaa... Baada ya hapo sikupewa tena ile 2,000/- niliyokuwa naipewa kwa ajili ya msosi... Nilimkumbusha boss wangu juu ya makubaliano yetu ambayo hayakuwa rasmi... Aliishia kusema atanipatia... Aliongeza kuwa ananisaidia tu kwani mimi ndo nilipaswa kumlipa kwani alikuwa ananipa 'exposure' (Katika kupitia madesa pale ofisini niliona fursa iliyokuwa imekaribia kuiva... Hivyo nikajipa moyo).

Kila siku niliyopewa ile buku 2 niliishia kununua mihogo ya mia 2 au mia tatu, nawekewa kwenye kimfuko 'transparent', nachanganyiwa humo pilipili nasepa zangu ofisini, nachota maji bombani nashiba ndiii... Hivyo baada ya boss mwenye ofisi kuanza kunikaushia kunipa ile buku 2 ya msosi, nilianza kutumia zile chenji kununulia ile mihogo kwa yule bibi pale jirani na ofisi.

Kwa ujumla maisha yalikuwa magumu sana... Namshukuru Mungu sana... kwani aliyekuwa ananihifadhi alikuwa mvumilivu na mwenye upendo sana... Hakuwahi nisimanga wala kuniona mzigo... Alinitia moyo na kunipa 'company' kubwa ajabu... Nilijihisi ni mwenye bahati... Ikanipa moyo wa kuzidi kupambania ndoto yangu.

Baada ya muda wa kufunzwa kazi kuisha nikaanza kulipwa laki moja kwa mwezi... Nilitumia ile pesa kununulia chakula pale ghetto na nyingine kuhifadhi kwani ndoto ya kwenda chuo ilikuwa imenikaba hasaaaa.

Baada ya kama miezi mitano ile fursa niliyoidesa ikaiva... Kutokana na uvumilivu mkubwa niliokuwa nao, boss akanipigia bonge la pande... Namshukuru Mungu nikapata pesa ya kutosha nauli ya kurudi home, nauli ya kwenda chuo na pesa ya kulipia 50% ya gharama za chuo... Kwani bodi ya mkopo walinipa 50% pekee... Maisha ya chuo yakaanza...

Kipindi chote cha chuo sikuweza kuhudhuria darasani kwa 100%... Nilinunua kibaskeli, kazi yangu ikawa kuzurura kwenye stationaries pale chuoni kuomba kazi ya kuchapa... Mungu ananipenda sana... Niliaminiwa haraka sana... Nikawa napewa assignment za wanafunzi walizopeleka kuchapiwa, nakwenda nazo ghetto, natumia laptop za ma-room mate, naweka kwenye flash, narudisha stationaries napewa pesa ya typing... Naitumia pesa kama pocket money na nyingine kutuma kwa mama angu mzee kule kijijini... Ilinilazimu kuishi hivi chuo kwani sikuwa na mjomba, baba, shangazi wala babu wa kunipatia pesa ya matumizi pale chuoni.

Stationary walinipenda sana maana kazi zote walizonipa nilizifanyia mpaka marekebisho ya lugha maana nipo vizuri kiasi kwenye lugha ya malkia ambayo ndo lugha kuu vyuoni kwetu. Kuna story ndefu katika kipengele hiki... Itoshe kuishia hapa.

Ilipofika mwaka wa pili sikuwa na pesa ya kulipia ile 50% iliyobaki... Niliandika mradi wa kununua 'toyo' ili inisaidie kujikusanyia pesa ninapokuwa free ili walau ipunguze makali ya gharama za pale chuo... Nilipambana kutafuta mtu wa kunifadhili kupitia ule mradi kwa mahangaiko sana... Sikukata tamaa... Mwisho nikabahatika kufadhiliwa na madam mmoja pale chuoni... Madam huyu alinilipia gharama zote za ile 50% iliyobaki... Alifanya hivi pia kwa mwaka wa tatu.

Baada ya chuo nikaja kitaa kuanza life after chuo... Nilipambana kufundisha shule moja wakati natafuta ajira... Mwaka mmoja baadaye nikabahatika kuajiriwa na kampuni moja hapa Arusha... Nilifanya kazi kwa bidii sana... Sijui nini kilitokea miaka minne baadaye... Kwani niliamshiwa vita vikali pale kampuni... Mwisho niliishia kuondolewa kazini kwa fedheha...

Nikajikusanya nikafungua kibiashara cha chakula... baadaye ile biashara ikadoda... Maisha yakaanza kuwa magumu balaa... Kula ikawa changamoto, marafiki wote wakakimbia, sikuweza hata kulipa kodi ya ghetto, nikatimuliwa, 'ka-kitanda' na 'ka-sofa' pale ndani nikauza ili nilipe kodi ya watu... Vifaa vya ule mgahawa navyo nikauza ili nilipe mkopo benki ambao waliniamini kunusuru dhamana ya kijumba ambacho hakijaisha wasije kukipiga mnada...

Nikaishia kuhifadhiwa tena na mmoja wa rafiki aliyeibuka baada ya kuona nadhalilika... Kuna rafiki mwingine mpya aliyekuwa dereva toyo naye aliibuka akawa anapambana na mimi kunitia moyo na kusaidizana na mimi ili nisimame tena... Naye akatekwa akapigwa visu akafariki...

Nikaona moja kati ya njia za kujikwamua ni kuanza kufanya online taxi, nikakodi gari la mtu, nalo baada ya wiki mbili likaungua injini... Nikawa kwenye shida mpya ya kutengeneza gari la watu tena... Acha kabisa asee...

Story ni ndefu... Ngoja niishie hapa ili kutokuwachosha... Ila mpaka sasa napambana kuweka mambo sawa katikati ya uchumi huu wa kati... Kamwe sitakata tamaa... Bidii za kujinasua na imani kwa Mungu ndo vinavyonipa nguvu... Kwa wenzangu na mimi mnaopitia changamoto kama hizi mjue hamko peke yenu... Tupo wengi tu.. tuongeze bidii ya kujinasua na kumuomba Mungu... Ipo siku yatabaki kuwa story.
 
Kuna mwamba mmoja aliwahi niambia

Mafanikio ni Kama Chupi Ficha Watu Wasijue.

HaHaHa
 
Usichokijua ni nyota zako zipo ovyo tunahangaika sana fanyia kazi hilo jambo itakuja kushukuru

Walifanikiwa wachoyo wa kutoa taarifa nzuri ya jins ya kufanikiwa.. watoto wa magomeni miaka fulani walienda sana China kufata bidhaa tofauti tofauti zikiwemo na nguo na wakirudi vijiweni wanazungumza na kujisifu nakusema.. yaani madogo tafuteni ml-5 mpaka 6 ukiwa nazo tutawapa diretion.. ukiwa umefanikisha kuzipata na ukiwatafuta na ukiwaambia wanakublock yaani watu waliofanikiwa wakoje? Sijui
 
Kuna vitu viwili unapaswa kuhakikisha viko sawa kabla ya kuanza harakati zako za utafutaji

1. Weka Mahusiano Mazuri Baina Yako na Mungu Wako
2. Hakikisha Uhusiano Wako Na Wazazi Wako Uko Vizuri na Kwamba Huwasahau Kwa Kila Hali.

Niamini Hakuna Nasema Hakuna Changamoto Itakujia Ukashindwa Kuivuka kwenye haya maisha.

Kuna kipindi niliachwa na Mwanamke nikapatwa na Stress Ila Namba 1 na 2 hapo Juu ndizo ziliniweka sawa sikutoka kwenye reli.

Baadae kuna mishe flani hivi nikaotea kwenye utafutaji wangu ilaniweka pazuri sana tu. Yule mwanamke akajuta sanaa baadae kwani alikua akisikia habari zangu. Ila ndio hivyo sijawahi rudia makombo / matapishi.

Niamini iko faida katika kuishi vizuri na watu...tabia na hulka yako ndio ina amua mwenendo wako wa maisha uwe vipi.

Thanks.
Point Sana umetoa
 
Kuna watu wanafanya hayo yote ila bado mshale unasoma vingine kabisa.
Iki kitu kinacho itwa maisha kiache tu.
 
Back
Top Bottom