Ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya fedha

faru john junior

JF-Expert Member
Dec 26, 2016
1,596
1,718
Husika na mada tajwa hapo juu,

Mimi ni mtumishi katika Secta Binafsi hapa nchini Tanzania.

Katika utumishi wangu nimefanikiwa kujichanga mpaka kufikia million 50. Hizi pesa ziko kwenye account bank lakini naona zimekaa tu nazidokoa dokoa ila kwa sasa natafuta taasisi gani ya Kifedha mfano hizi bank au yoyote ile ambayo naweza kuwapa waifanyie kazi lakini mwisho wa mwezi waweze kunizalishia angalau Milioni 1.2 kama riba.

Nafahamu nilipaswa kuanzisha biashara kwa kiwango hicho lakin nature ya majukumu niliyonayo kwa sasa siwezi kufanya biashara. So naombeni ushauri najua humu ndani kuna wataalam wengi sana wanaojua wapi naweza fanya hizi harakati.

Asanteni sana

Sent from my SM-N980F using JamiiForums mobile app
 
do!

Wakati wengine hawana cha kufanya na 50m wengine tunatafuta 4m tupindue meza ili baada ya miaka 3 niwe na mradi wa 30m.

wewe wekeza kwenye hati fungani za benki kuu na hasa ya miaka 20 ambayo itakuwezesha kuchukua mkopo na kuwekeza kwa nafasi na uelewa mkubwa.
 
do!
wakati wengine hawana cha kufanya na 50m wengine tunatafuta 4m tupindue meza ili baada ya miaka 3 niwe na mradi wa 30m.
wewe wekeza kwenye hati fungani za benki kuu na hasa ya miaka 20 ambayo itakuwezesha kuchukua mkopo na kuwekeza kwa nafasi na uelewa mkubwa.
Umeanza kimakasiriko, lakini asante kwa kumalizia vizuri kabisa..!!

By the way, hivi hizi za miaka 20, ukifa kabla ya miaka 20 kutimia nini kinatokea?
 
Umeanza kimakasiriko, lakini asante kwa kumalizia vizuri kabisa..!!

By the way, hivi hizi za miaka 20, ukifa kabla ya miaka 20 kutimia nini kinatokea?
nimekuandikia na kukuwekea Document kuhusiana na lilichokueleza kwenye pm
huku watu hawapendi kusoma vitu virefu sana.
 
Hakuna taasisi ya kifedha wanaweza kukupa riba ya 1.2 mln kwa mwezi kwa 50 mln

Mwaka huu BoT imeingia rasmi kwenye mfumo wa interest rate based monetary policy

BoT wamepanga benchmark rate set at 5.5% ambayo benki zote za biashara Tanzania zitatumia

Kwa hiyo kwa 50mln utapata riba ya 2.6 mln per year. Ambayo kwa mwezi ni 210,000

USHAURI: Wekeza kwenye assets
 
Chukua milioni 20 nunua bajaji toa fursa kwa vijana wa hapo mtaani kwako kila siku wanakupa 30 iyo 30m inabaki ndo tafuta izo bank za ku invest apo ni win win
 
Kama nimekuelewa Unahitaji Investment ambayo ni Low Risk ambayo ina return ya 1.2M Profit kwa Mwezi ambayo ni sawa na 14.4Mil per year ambayo ni sawa na 28% return.

Kwa kiwango hicho Cha RIBA na hutaki RISK Itakuwa ni Ngumu ila inawezekana kama Utatafuta Private Sector Ila SIO BANK.

Ila kama Tungeonana Last December.Ungeweza Kupata Fursa ya Kupata 500,000 kila Mwezi na Hela yako bado Ikiwa Salama Benki
 
Back
Top Bottom