Naomba ushauri wa biashara ya malori

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
852
1,158
Wakuu nawasalimu kwa Jina la JMT.

Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza. Nimekuja humu ndani kupata ushauri wa Biashara ya Malori haya ya kubeba mizigo iwe ya Local ama Transit.

Kutokana na Connection nilizonazo nadhani suala zima la kupata Mizigo ya Kusafirisha halitokuwa la kuumiza kichwa.
Changamoto inayonikabili ni funding pamoja na aina ya truck ambayo inapaswa ni nunue.

Kabla ya kuja humu ndani nilishaomba ushauri kwa watu kadhaa ambao wapo kwenye hii industry na wamenijuza truck nzuri ya kununua ni Mtumba SCANIA 124 420 iliyotumika Europe. Hawakunishauri kabisa kununua Truck Mpya ama Refurbished za Mchina, DAF na Volvo wakaniambia zitanitesa maana ndio kwanza naingia kwenye game. Hata nilipouliza SCANIA zilizotumika south Africa wakaniambia ni bora nichukue za europe zinakuwa bado zipo Bora na hazijatembea sana kwenye rough road kwa hizo za SOUTH japo hizo za south walikiri kwa gharama ya manunuzi zipo chini kiasi.

FUNDING
Kama nilivyoeleza awali mimi ni new comer kwenye hii industry hivyo nategemea kujichanga kama 50-60Mil then the rest nichukue mkopo maana nakopesheka vizuri sana. Baada ya kufanya window shopping nimegundua horse scania mtumba inaweza kunicost kati ya 75Mil - 85Mil hapa nitapata gari nzuri tu, Trailer nimeshauri kununua ya Mkononi ambayo imetumika hapa nchini ambapo zina range 25Mil - 30Mil kutokana na hali yake. Nimejaribu kuulizia. Mpya lakini naona bei imechangamka sana USD 28,500.00 flatbed Double tire

TECHNICAL
Nimeshauriwa hapo kwenye trailer kununua super single kwa maana inabeba Mzigo Mkubwa kulinganisha na trailer yenye double tire.
Kwenye Horse kama nilivyoeleza awali nimeshauriwa SCANIA 6x2 124L 420 Mtumba kutoka EUROPE

BUDGET
Ukiangalia makisio ya gharama zote Horse na Trailer budget yake inacheka kati ya 100Mil - 115Mil. 60% Nategemea kuitoa Mfukoni na 40% nichukue Mkopo. Nategemea kulipa Mkopo kwa kutumia Mshahara wangu pamoja na Mapato yatakayokuwa yanapatikana baada ya Truck kuanza kuoperate. Nimekuja kuomba ushauri kwa yeyote mwenye kuielewa biashara hii kwa undani, nimeweka mchanganuo wote hapa ili niweze kupata ushauri mzuri kulingana na information nilizopokea pamoja na uwezo wangu wa kifedha. Nategemea kuna wajuzi wengi humu na nitaambulia ushauri mzuri katika kukamilisha hili. Ahsanteni na niwakaribishe kwa Ushauri. Kejeli na dharau hapa si mahala pake.

UPDATE: Baada ya Ushauri wa Kina na kuchuja yote niliyoelezwa. Nimefikia uamuzi wa kuagiza Scania G420 kutoka Uingereza. Nimeachana na gari za kizamani 113, 124 kama wengi walivyoshauri. Wakati nikisubiria Gari ifike napambana na kutafuta trailer. Nimefuatilia Weight Limits za TANROAD naona Super Single na double tire trailers zote zimepewa uzito sawa wa 24MT kwa axle tatu za nyuma. Hii ina maana kuwa kwa kuwa super single ni nyepesi basi itabeba mzigo mwingi. Najua maybe nitakuwa sipo sawa kwenye hili, nipo tayari kurekebishwa kwa mwenye ujuzi zaidi.

Lingine linalonitatiza, trailer ya booster na ya spring ipi ni bora. booster inahitaji service nyingi kuliko spring. lakini pia booster ikiharibika ni lazima itengenezwe hapo hapo ndio safari ianze. Wajuzi naomba nimerudi tena kwenu kuomba ushauri mzuri kwenye trailers. Ahsanteni

UPDATE 2:

Nimefanikiwa kupata Trailer mtumba ya mkononi ambayo imerekebishwa. Najiandaa kupokea Scania Horse ambayo mpaka kufikia mwisho wa mwezi ujao itakuwa imefika na kutoka Bandarini.

Estimated Budget kwa Horse na Trailer hadi hapa ni 120m. Na hapo nimepambana sana. Kumbuka tela nimenunua mkononi ya double tire spring ambayo imekarabatiwa. Horse nimeagiza mtumba UK. Ahsanteni

UPDATE 3:

Gari ilianza kazi rasmi katikati ya mwezi October, 22. Nilianza Kwa trip chache za ndani ya nchi yaani local trips. Nilipata experience nzuri na mbaya. Most of worst experience ni kukutana na madalali waroho wasio waaminifu. Huwezi Siku zote kufanya hii kazi na Mteja mwenye mzigo Moja Kwa Moja, Ipo siku tu utanyanyua simu Kwa Dalali. Na ndicho kilichonikuta. Balance payment inakuwa shida kumaliziwa. Unapelekwa trip ya mbali Kwa malipo hafifu Ilhali address uliyoambiwa ilikuwa no fupi. Nilifanya hizi local trips Ili kuisoma gari performance yake kabla ya kwenda kupakia Transit.

November 11th , 2022 nilianza rasmi na trip ya kwanza ya Transit. Nilipata rates nzuri tu kutoka Kwa Wakala wa forodha kwenda Lubumbashi, Congo. Baada ya Siku mbili tulifika Tunduma. Baada ya Clearance ya gari safari iliendelea. Zambia mwisho wa kutembea ni saa tatu usiku Kwa mizigo ya container na loose cargo. Hivyo Kwa Siku hiyo muda ulipofika Dereva alilala kwenye Mji unaoitwa Mpika. Ni kama 350km kutoka Tunduma.

Kumi na Moja na upuuzi alfajiri gari iliendelea na safari. Baada ya kama dakika 30, niliona kupitia GPS gari imesimama. Ilisimama Kwa Muda Mrefu sana zaidi ya dakika 40. Muda mchache baadae nilipokea simu kutoka Kwa Namba ngeni Kwa njia ya WhatsApp.

Alijitambilisha kama dereva aliyekuwa nyuma ya gari yangu wakiongozana. Alinitaarifu juu ya Ajali iliyohusisha gari yangu. Gari imedondoka kama km 20 kutoka kwenye mizani ya Mpika.

Kiza kikatawala, mapigo ya Moyo yakaongezeka, Miguu ikakosa nguvu. Sikujua kilichoendelea tena. Nilizinduka baada ya kumwagiwa maji. Itaendelea......
 
Mimi binafsi ninge kushauri ungepata scania mende ya mchaga inarudisha pesa haraka na used ni 80-90m kwa Dar zipo, kwa wiki inaleta 1.8m, kuhusu mkopo kama kuna wezekano wa kununua mwenyewe subiri upate hiyo pesa au muelewane na mwenye gari umtangulizie tu, ila benki za hapa hazisaidie ila zinafilisi ndo zinapopata faida yao, biashara ya gari sio ya kuchukulia mkopo benki, risk analysis yake is above 50% don't risk mkopo
 
Mimi binafsi ninge kushauri ungepata scania mende ya mchaga inarudisha pesa haraka ya na used ni 80-90m kwa Dar zipo, kwa wiki inaleta 1.8m, kuhusu mkopo kama kunawezekano wa kununua mwenyewe subiri upate hiyo pesa au muelewane na mwenye gari umtangulizie tu, ila benki za hapa hazisaidie ila zinafilisi ndo zinapo pata faida yao, biashara ya gari sio ya kuchukulia mkopo benki risk analysis yake is above 50% don't risk mkopo
Mkuu nimeamua hivyo kwa sababu connection yangu ni kupata Mizigo ya kubeba kwenye flatbed sio Mende
 
Wakuu nawasalimu kwa Jina la JMT.

Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza. Nimekuja humu ndani kupata ushauri wa Biashara ya Malori haya ya kubeba mizigo iwe ya Local ama Transit.

Kutokana na Connection nilizonazo nadhani suala zima la kupata Mizigo ya Kusafirisha halitokuwa la kuumiza kichwa.
Changamoto inayonikabili ni funding pamoja na aina ya truck ambayo inapaswa ni nunue.

Kabla ya kuja humu ndani nilishaomba ushauri kwa watu kadhaa ambao wapo kwenye hii industry na wamenijuza truck nzuri ya kununua ni Mtumba SCANIA 124 420 iliyotumika Europe. Hawakunishauri kabisa kununua Truck Mpya ama Refurbished za Mchina, DAF na Volvo wakaniambia zitanitesa maana ndio kwanza naingia kwenye game. Hata nilipouliza SCANIA zilizotumika south Africa wakaniambia ni bora nichukue za europe zinakuwa bado zipo Bora na hazijatembea sana kwenye rough road kwa hizo za SOUTH japo hizo za south walikiri kwa gharama ya manunuzi zipo chini kiasi.

FUNDING
Kama nilivyoeleza awali mimi ni new comer kwenye hii industry hivyo nategemea kujichanga kama 50-60Mil then the rest nichukue mkopo maana nakopesheka vizuri sana. Baada ya kufanya window shopping nimegundua horse scania mtumba inaweza kunicost kati ya 75Mil - 85Mil hapa nitapata gari nzuri tu, Trailer nimeshauri kununua ya Mkononi ambayo imetumika hapa nchini ambapo zina range 25Mil - 30Mil kutokana na hali yake. Nimejaribu kuulizia. Mpya lakini naona bei imechangamka sana USD 28,500.00 flatbed Double tire

TECHNICAL
Nimeshauriwa hapo kwenye trailer kununua super single kwa maana inabeba Mzigo Mkubwa kulinganisha na trailer yenye double tire.
Kwenye Horse kama nilivyoeleza awali nimeshauriwa SCANIA 6x2 124L 420 Mtumba kutoka EUROPE

BUDGET
Ukiangalia makisio ya gharama zote Horse na Trailer budget yake inacheka kati ya 100Mil - 115Mil. 60% Nategemea kuitoa Mfukoni na 40% nichukue Mkopo. Nategemea kulipa Mkopo kwa kutumia Mshahara wangu pamoja na Mapato yatakayokuwa yanapatikana baada ya Truck kuanza kuoperate. Nimekuja kuomba ushauri kwa yeyote mwenye kuielewa biashara hii kwa undani, nimeweka mchanganuo wote hapa ili niweze kupata ushauri mzuri kulingana na information nilizopokea pamoja na uwezo wangu wa kifedha. Nategemea kuna wajuzi wengi humu na nitambulia ushauri mzuri katika kukamilisha hili. Ahsanteni na niwakaribishe kwa Ushauri. Kejeli na dharau hapa si mahala pake.
Achana na hiyo biashara!
Kama utaziweza hizi changamoto try!
1-Ale dereva!
2-Ale msaidizi!
3-Ile gari!
4-Ile serekali!
5-Ale dalali!
6-Ale Trafic
Kitakacho fika kwako sound!....

Wekeza kwenye kilimo cha Kitaalamu!
 
Kazi njema kwako kijana mwenzangu...mie bado sijafikia hatua hiyo ila mpaka hapa unapolileta hapa ilo wazo lako basi Mungu akusimamie na kukufanikishia wazo lako, umethubutu hongera yako.
 
Achana na hiyo biashara!
Kama utaziweza hizi changamoto try!
1-Ale dereva!
2-Ale msaidizi!
3-Ile gari!
4-Ile serekali!
5-Ale dalali!
6-Ale Trafic
Kitakacho fika kwako sound!....

Wekeza kwenye kilimo cha Kitaalamu!
Broo umemshauri vizuri Sana huyu jamaa asije pata pressure buree. Niko ktk magari ya mtu tunapanga kuyapiga minada yote, scania mende Bei iko poa kama utaziitaji ukachongee body POA tu Ila Ni risk bussines ever
 
Achana na hiyo biashara!
Kama utaziweza hizi changamoto try!
1-Ale dereva!
2-Ale msaidizi!
3-Ile gari!
4-Ile serekali!
5-Ale dalali!
6-Ale Trafic
Kitakacho fika kwako sound!....

Wekeza kwenye kilimo cha Kitaalamu!
Kila mtu mwenye semi angekuwa na mawazo kama yako hakuna semi ambayo ingekuwa inatembea barabarani ssahivi.

Watu wengi tu wanaanza na semi moja au mbili baada ya miaka kadhaa unakuta kafikisha hadi 7 huko au zaidi. Mtoa mada naomba usikatishwe tamaa na mawazo finyu ya huyu jamaa.
 
Hakuna Biashara isiyo na risk Ndugu yangu, Risk huwa kubwa kutoka na investment yako, Mtu unatoka nyumbani na chapati 100 kwenda kuziuza, Jiulize hao watu mia yeye anao hana, Ni anaimani kwamba atakutana na watu na watanunua na zitaisha hii n risk, Biashara hupungua risk baada ya kuwa na uhakika na wateja wako ambao ni permanent tu bila hivyo Biashara zote unavyooanza ni Gambling 😄 So fanya kama unamini katika hilo. Mwanzo ni mgumu.
 
Back
Top Bottom