Mkuu mimi kama FUNDI FRIJI DAR nikupe mwongozo mfupi wa kiufundi:
1. Top-Mount (Friza Juu, Friji Chini):
• Ufanisi: Ndiyo friji imara zaidi duniani kote, mifumo yake ya compressor hailii mzigo mkubwa na inadumu sana.
• Nafasi: Rafu zake ni pana. Inafaa kama una tabia ya kuingiza sufuria kubwa au sinia la chakula.
• Matengenezo: Ni rahisi sana kupata vipuri (spare parts) na mafundi wengi wanazijua vizuri.
2. Side-by-Side (Milango miwili sambamba):
• Ufanisi: Ina muonekano wa kisasa na wa kifahari, lakini hutumia umeme mwingi zaidi kwa sababu ina mifumo miwili mikubwa ya kupoza upande kwa upande.
• Nafasi: Ni ndefu kwenda juu lakini nyembamba kuelekea pembeni. Sufuria kubwa au sinia halingii hapa.
• Changamoto: Ikishapata hitilafu ya mfumo wa umeme au leakage ya gesi, matengenezo yake ni gharama kubwa sana na vipuri vyake ni adimu hasa vifaa vya umeme.
Ushauri wangu kama Mtaalamu: Kama unaangalia urembo na unahifadhi vitu vidogo vidogo, chukua Side-by-Side. Lakini kama unataka friji ya kazi, ya kudumu, na isiyosumbua kwenye matengenezo, chukua ile ya kawaida ya Friza Juu.