Ushauri wa kifamilia/kijamii

Ushauri wa kifamilia/kijamii

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,490
Reaction score
8,305
Naamini hamjambo.

Naomba tushauriane juu ya hili swala linalohusu familia zetu. Kama tujuavyo katika mahusiano migongano haikosekani. Mingine hata kuitatua Ni vigumu sana, hata hivyo kama muwazazi ni muhimu sana kuwaweka mbali watoto wetu na migongano yetu.

Si unajua tena wakati mwingine ni wivu tu au mmoja wenu kutokuwa na uwezo wa kutimiza wajibu wake. Ni hatari sana unapomzungumzia vibaya mwenzi wako mbele ya watoto wenu, unaumiza hisia zao.

Epuka pia kusengenya mtu mbele ya watoto inakupunguzia heshima na unawafanya kudhani kuwa kusengenya ni Jambo zuri, achilia mbali pale watoto wenyewe wanapokuwa na imani kuwa hata wewe siyo mzuri kihivyo.

Tuwape watoto fursa ya kuchagua yupi mwema na yupi mbaya. Mtoto aliyeshibishwa matukano na masengenyo ya watu wazima anapoteza imani na ujasiri wa kuchanganyika na watu au kuwaamini wengine anapokuwa mkubwa. Pia huamini kuwa hata yeye anasengenywa asipokuwepo.

Ni vigumu pia kuwa na moyo wa upendo kwa watu wanaomzunguka. Tuwaache watoto wawe watoto.

Asante.
 
Back
Top Bottom