Ushauri wa kanuni bora za kilimo cha Migomba na Soko lake


Huna mwenyeji kipande hicho?
 
Mheshimiwa, Red Giant umezungumzia zao muhimu sana na wachangiaji wamemwaga uzoefu wao kiasi cha kutia hamu sana kulitazama zao hili kwa jicho la husuda. Mimi nikiamua kujua kipato cha ndizi huwa ninachukulia kuwa litatunzwa na kuvunwa mwaka mzima. Kwa vile aina tofauti zinapandwa nafasi tofauti, fupi hupandwa karibu karibu mita 3 kwa mita 3 na ndefu hupandwa kwa nafasi pana zaidi, mita 4 na kuendelea. Kwa hiyo ni muhimu ujue idadi ya mashimo (mashina) kwa shamba la ekari moja. Upandaji wa 3m x 3m hutoa mashina 444 na hushauriwa kupishanisha umri wa mashina kwenye kila shimo ili uweze kuvuna kila baada ya miezi 3 au 4 kwa kila shimo kwa hiyo kila shimo shambani unatarajiwa uvune mikungu 3 kwa mwaka! Kwa hiyo kipato kwa mwaka ni mikungu 444 x 3 x bei ya mkungu 12,000/- = Tshs 15,984,000 kwa kwa ekari moja kwa mwaka. Unaweza kupunguza kipato hiki kwa asilimia 10 kufidia mashina yenye matatizo na yaliyokufa. Zidisha kipato hiki kwa eneo lako uliwezalo kulimudu!

Ni vizuri pia kulima eneo kubwa ambalo linaweza kumlipa Mlinzi na ukabaki na faida maana ni rahisi sana kuibiwa ndizi ukilinganisha na mazao mengine! Maeneo mengi hasa karibu na makazi wizi wa ndizi ni kikwazo kikubwa.

Kuhusu aina gani ya ndizi inafaa kupanda angalia soko linataka aina gani! Nenda sokoni tambua aina zinazolipa sana na ambazo ukifika nazo hapo wafanyabiashara wanazikimbilia, kisha angalia katika aina hizo ulizoona zinakubalika ni ipi inakubaliana na mazingira utakayolimia, ikibidi mwanzoni usilime aina moja tu, panda aina hata tatu maarufu kisha baadae utaendelea na itakayoonekana kukulipa zaidi! Kuna aina za ndizi zinabei kubwa lakini zinachakaa haraka sana shambani na hazina uzao mkubwa, zingine zina bei wastani lakini zinazaa sana na kudumu shambani muda mrefu.

Kuhusu udongo ikitokea udongo ulionao ni kichanga na huna jinsi cha muhimu ni kuurutubisha kwa samadi! Ndizi zinahitaji urutubishaji mkubwa hasa kwenye udongo usiona rutuba ya kutosha!

Aina
ya mbegu bora utolewa kwenye vituo vya utafiti wa Migomba kama Maruku Kagera, mashamba ya Magereza na JKT, SUA na Vyuo vya kilimo. Popote utakapopata mbegu uipendayo hunabudi kuzalisha hiyo mbegu, si rahisi kupata mbegu kwa eneo kubwa pia gharama za usafirishaji mbegu zinaweza kuwa kubwa sana.
 
hapo kwenye nyekundu si kweli maana China kilimo cha mpunga kipo juu sana sema tu analima kwa biashara ya hapa kwetu maana ni dili zaidi ya kusafirisha

Ndugu...Tembelea ukaone..wamepewa eneo na RUBADA na mara ya mwisho nilipopita walishaweka kambi na vifaa... labda kama wamesitisha mradi...
 
Iko sehemu moja inaitwa Mbingu, ni kama kilomita 60 ukitokea Ifakara mjini kwenda Milmba/ Mngeta. sehemu hii hujulikana kama Tandale, kutokana na umaarufu wa ndizi zake kujaza soko la tandale Dar-es salaam. Hii ni sehemu ambayo ina maji mengi sana kutokana na mito midogo midogo inayotririka kutokea kwenye hifadhi ya Milima ya Udzungwa yaani Udzungwa National Parks escarpments.
Wakazi wa eneo hili hujaza malori na malori ya ndizi na kupeleka Dar kwaajili ya kuuza, ama huwauzia watu wenye malori wanaokuja kulangua ndizi toka Dar.
Ikiwa Mdau kama Bwana Mallila umetoa utaalamu kama huo, hii ni sehemu nzuri sana kwa wadau wanataka kuanzisha kilimo hicho kuwekeza mahali pale. Na kama uko dar unatumia usafiri wa Tazara train ambayo hupita pale walau kwa wiki mara mbili.
Kama wenyeji hupata mazao mengi kiasi kile bila kutumia utaalamu alioutoa mdau haop juu, je ikiwa mtu akijitosa na kutumia utaalamu kama huo si ataona positive results kwa muda mfupi?
Sehemu hii ni kubwa na wala haina uhaba wa ardhi, nilipita pale juzi, nikaona tangazo kuwa kama kuna mtu anahitaji shamba basi akamwone mwenyekiti wa kijiji na atapewa bure na kama ni ekari nyingi atalipia kila ekari sh 5000/ !!!.
Wadau, fursa za namna hii ni chache sana katika nchi zingine, ila nchini mwetu zimejaa mbona hatuzitumii??
 
Kwa uzoefu wangu mdogo juu ya zao hili ni kuwa pamoja na maji mengi, linahitaji mbolea nyingi ya samadi au mboji.
Unaweza kupata mboji nzuri kama utajenga mtambo (compost pit / biogas plant)-Anayehitaji ninaweza kumsaidia hii kwakuwa ni kazi yangu. Angalia mfano wa mgomba wangu ulioko kwenye sandy soil na una miezi minne tangu upandwe na unatumia mbolea inayoyoka kwenye mtambo wa biogas.


Pia kwa habari ya mbegu za kuanzia ni kweli vituo vya utafiti wanazo, kama kile cha Minazi DSM ninakumbuka miaka kama 12 iliyopita walionyesha teknolojia ya kubeba mashina/ mbegu za migomba kwa mamia nani ya kichupa kidogo. Hivyo kwa wanaoenda kulima mbali wanaweza kupata mbegu na teknolojia hiyo ya kusafirisha mbegu toka kwao.
 
Safi sana japo mimi sijaanza na ndizi nimeegemea sana kwenye mananasi na mahindi mda ukifika nitabadirisha adia
 
heka moja inaweza ikapandwa mashina mangapi na kipindi cha mavuno kikifika kwa mwezi mmoja unaweza ukapata mikungu mingapi
 
umenisisimua sana na habari yako nilifika ifakara sema nilikuwa kwenye utalii wa ndani nikaishia kwenda kuona mto kilombero ntajitahidi nifika hadi huko mbingu one day. thanks sana kwa taarifa.
 

Mkuu, nilifika Tandale kisa hakikuwa ndizi, kisa kilikuwa cocoa. Kuna NGO moja iko pale RC mbingu inajiita MOCOA ndio niliwafuata. Hili tangazo la ardhi liko kijiji gani pale watu tudamkie huko asubuhi? Maana hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Mkuu, nilifika Tandale kisa hakikuwa ndizi, kisa kilikuwa cocoa. Kuna NGO moja iko pale RC mbingu inajiita MOCOA ndio niliwafuata. Hili tangazo la ardhi liko kijiji gani pale watu tudamkie huko asubuhi? Maana hakuna kulala mpaka kieleweke.

Kuna jamaa yangu wa Ifakara aliniambia Mbingu kupata ardhi ni issue cause ile ardhi ni nzuri sana na Wamarekani wamepewa sehemu kubwa sana hapo
 
Kuna jamaa yangu wa Ifakara aliniambia Mbingu kupata ardhi ni issue cause ile ardhi ni nzuri sana na Wamarekani wamepewa sehemu kubwa sana hapo

Ni kweli, ni gharama sana pale Mbingu, hata juzi nimeongea na bosi wa MOCOA kasema, kipande hapa Mbingu ni balaa. Hii vita simalizii jf hapa, naenda huko huko hata kama ni Chita.
 
Ni kweli, ni gharama sana pale Mbingu, hata juzi nimeongea na bosi wa MOCOA kasema, kipande hapa Mbingu ni balaa. Hii vita simalizii jf hapa, naenda huko huko hata kama ni Chita.

Chita Kuna unafuu kaka nilikuwa na namba ya mwenyeji wa huko niliipoteza ngoja niulizie kama kuna mtu anayo alikuwa jirani yetu kwao kulikuwa ni Chita anaweza kukusaidia kukupa mwongozo
 
Chita Kuna unafuu kaka nilikuwa na namba ya mwenyeji wa huko niliipoteza ngoja niulizie kama kuna mtu anayo alikuwa jirani yetu kwao kulikuwa ni Chita anaweza kukusaidia kukupa mwongozo

Chita nakwenda mwenyewe,nikifika nitajua namna ya kuingia kwa wenyewe. Ubaya wa kupelekwa, ni huu, mwenyeji wako anaweza kukupa sifa ambazo zitakuumiza.
 
Chita nakwenda mwenyewe,nikifika nitajua namna ya kuingia kwa wenyewe. Ubaya wa kupelekwa, ni huu, mwenyeji wako anaweza kukupa sifa ambazo zitakuumiza.

Ni kweli wakafikiri Pedeshee anakuja ukaishia kuumia
 
Sabayi na Malila msipuuze post ya Alex Mponela, unaweza kuta mkapata ardhi nzuri na ya bwelele huko. mkuu Malila ni vyema kwenda kujionea mwenyewe kama ulivyosema utaenda chita.kuna jamaa yangu aliwahi niambia eti huko malinyi ardhi ni 5,000 kwa ekari!!. watu wengi wakikwambia eti ardhi ni ghali sana mara nyingi huangalia ile ya ''mjini'' au karibu na barabara, lakini ukiingia hata km 5 au 10 ndani utakuta bei cheap ajabu.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu binafsi sijapuuza ni kweli kuna sehemu Malinyi ardhi ni 5000 Kwa ekari ila nilisikia ya hapo Mbingu ni ghari kidogo na kupata ni issue ila sehemu kubwa ya Malinyi ardhi bado ipo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…