Ushauri wa kanuni bora za kilimo cha Migomba na Soko lake

HHabari,Mimi nahitaji watu wa kuwauzia ndizi na viazi mikoa ifuatayo,morogoro, dares salaam na singida...nipo mbeya hivyo nahitaji agents/wanunuaji kwa mikoa hiyo...no 0743185408
 
Mimi napenda kuangalia ukulima wa mazao mbalimbali. Kuhusu ndizi nikapata habari zilizonipendeza nikasema nishirikiane nanyi.

Ukipanda ndizi leo itachukua kati ya miezi kumi hadi kumi na mbili kuzaa mkungu. Pia itategemea hali ya maji maana ndizi zinahitaji maji mengi sana. Ukishuvuna mkungu huo mmea unaukata na itachukua miezi mingine kama hiyo kwa machipukizi ya ndizi kuvunwa.Kuvuna huku kunaweza endelea kwa miaka 25 hapo ndio mtu unaweza kutoa mimea yote na kuanza upya.Twende kwenye uzaaji.

Kwa wakulima wa kawaida ekari ya ndizi huzaa tani 7 za ndizi ambazo ni sawa na kg 7000.

Kwenye vituo vya utafiti ilionekana ekari moja inaweza kuzalisha mpaka tani 24 yaani kg 24000.

Mkungu mmoja wa ndizi kwa wastani una uzito wa kg 12. kwa hiyo ukipata kilo 7000 utakuwa umepata mikungu 583 ya ndizi.

Kwa Dar es salaam mkungu mmoja wa ndizi ni kati ya tsh 12000-18000 ikitegemea na kipindi.Basi kwa mikungu 583 utapata tsh millioni 7 hadi milllioni 10!!.

Je, ukiwa na ekari 10, 20 au 30 utakuwa wapi?.

Mambo ya kuzingatia ni kuhakikisha migomba yako inapata maji ya kutosha na unaikinga na magonjwa na panya wala mizizi.

Pia ni vizuri ukalima eneo kubwa kidogo au mkakubaliana na majirani ili kuepuka kusafirisha mzigo kidogokidogo kitu kinachoweza kukupa hasara.

Wenye experiance na nyongeza naombeni muongezee. Malila, Chasha, Sabayi, Kubota etc

update 26/3/2015

Wakuu nimepata ekari tatu nimeanza kuzipanda kidogokidogo.Mpaka sasa nimepanda miche 200 niliyopanda mwezi wa February. Ila napanga mpaka mwezi wa saba niwe nimemaliza. Nimefanya utafiti na kwa kauzoefu nilikopata nimejifunza yafuatayo.

- Watafiti wa Uganda walifanya utafiti kuhusu spacing ya migomba. Kuna waliyoweka 3mx3m na kupanda migomba 400 kwa ekari. Mikungu iliyozaliwa ilikuwa na kilo 14. 2.5x2.5 walipanda migomba 640 kwa ekari na ilikuwa na mikungu ya kilo 12.5 hadi 13. Kuna mingine ilikuwa 2x2 na walipanda migomba 1000 kwa ekari na mikungu yake ilikuwa kilo 11.

Kutokana na hivyo mi napanda 2.5x2, ambayo itatoa migomba 800 kwa ekari. Huu ulikuwa utafiti wa ndizi Uganda ila mimi napanda mzuzu.

Shimo linakuwa kipenyo cha 60cm na urefu wa 60cm. au urefu wa hadi gotini kwa mtu mzima. Kila shimo wanachimbia sh 300 hadi 500 kulingana na ugumu. Maximum 400,000 kwa ekari.

Kila mche nanunua tsh 300 na kubeba hadi shambani ni tsh 200. Jumla itakuwa 400,000 kwa ekari.

Napandia debe moja la samadikila shimo. Nimeinunua 20,000 na kila debe wanabebea tsh 400. Jumla ni 340,000 kwa ekari. Kupanda ni 100 sawa na 80,000 kwa ekari.

Jumla ya kukamilisha eka itakuwa 1, 220,000. Gharama za palizi na zingine ntakuwa nawaupdate.

Mkuu uko sahihi kabisa,

Ktk kilimo napenda migomba ( kwa sasa natafuta shamba),nyuki,cocoa ( wizi wa matunda),miti ya mbao,samaki na ufugaji( kwa sasa swine bado). Hivi vitu unaweza kuvifanya bila shinikizo la damu kukupanda na mavuno yake yako bayana kwa maana ya soko.

Mkuu nilikwenda sokoni Tandale pale Mbingu Ifakara 2011 kutafuta shamba, mashamba yako juu sana.Kule Mby mashamba ni ghari sana, sijakata tamaa. Kuna mdizi mmoja niliuona mahali fulani kule Mwalusembe, ni balaa. Maeneo yale mzuzu unazaa vizuri sana. Mzuzu na mshale unaweza kukaa muda mrefu sana bila kuharibika. Mazao ya ndizi kutoka ktk eka kumi yanaweza kuendesha miradi mingine. Kuna bonde fulani nalifanyia upekuzi, nikiona liko vizuri basi nitarudi jamvini ili wanaotaka kulima pamoja na mimi tujitose.

Asante kwa kurusha hii kitu jukwaani.

Mkuu Saluti nyingi sana kwa huu uzi
Unachoongea ni kweli kabisa Ndizi zinalipa sana ila tusiangalie soko la Tandale tu ukiweza kufanya in large scale kuna soko kubwa sana Botswana na Pia ulaya ambapo waganda huwa wanacross boarder kuja kuzinunua Bukoba na kuzipeleka Ulaya unaweza fanya hii kitu mwenyewe.

Sabayi kwa vile hili ni zao la kitropiki nafikiri halihitaji baridi maana kama wiki mbili zilizopita nilikuwa ifakara kuna joto na zimestawi sana, nahisi zinataka maji kwa wingi tu. labda na udongo wa pwani wa kichanga unaweza kuwa tatizo. pia kama ukitoka rungwe ukifika milima ya uporoto hili zao halistawi na niliambiwa ni sababu ya baridi kuwa kali sana.

Mkuu Sabayi na wadau wengine wote,
Nimeona article hii hapa kwenye internet kuhusu zao la ndizi.
Inaweza kuwa ni mwomngozo mzuri kwetu, na kwa wengineo pia.
Asanteni.

Mkuu nakumbuka miaka ya Tisini mwanzoni tulikuwa na migomba nyumbani kwetu Dar na ilikuwa inakubali vizuri tu nahisi labda inahitaji sana Maji na ndo maana Tukuyu ambako mvua inanyesha sana hii migomba inakubali sana

Mu-Israeli nimeipenda article yako, ntaisoma tena na tena. imeeleza kwamba ndizi zinataka joto la kati ya 26-30 [SUP]0[/SUP]C.
 
Mkuu uko sahihi kabisa,

Ktk kilimo napenda migomba ( kwa sasa natafuta shamba),nyuki,cocoa ( wizi wa matunda),miti ya mbao,samaki na ufugaji( kwa sasa swine bado). Hivi vitu unaweza kuvifanya bila shinikizo la damu kukupanda na mavuno yake yako bayana kwa maana ya soko.

Mkuu nilikwenda sokoni Tandale pale Mbingu Ifakara 2011 kutafuta shamba, mashamba yako juu sana.Kule Mby mashamba ni ghari sana, sijakata tamaa. Kuna mdizi mmoja niliuona mahali fulani kule Mwalusembe, ni balaa. Maeneo yale mzuzu unazaa vizuri sana. Mzuzu na mshale unaweza kukaa muda mrefu sana bila kuharibika. Mazao ya ndizi kutoka ktk eka kumi yanaweza kuendesha miradi mingine. Kuna bonde fulani nalifanyia upekuzi, nikiona liko vizuri basi nitarudi jamvini ili wanaotaka kulima pamoja na mimi tujitose.

Asante kwa kurusha hii kitu jukwaani.

Safi sana Mkuu. Mimi na wenzangu tumeanza mikakati ya kulima ndizi kule Kisarawe kwa kushirikiana na wadau wengine. Lengo letu ni kulibadilisha lile eneo, kwa uwezo wa Allah, liwe ni ukanda wa ndizi. Kwa kushirikiana na wadau tunataka mpaka miaka ijayo tuwe na ekari kama 300 hivi za migomba. Kwa kuanzia tunaanza na ekari kama kumi hivi.
 
Neo

Safi
 
Naulizia jamani hivi wale wataalamu wa hiki kilimo bado wako humu??
Kama wamo ninaomba waufufue huu uzi ili tuliofata mawazo yao tuwape mlejesho jamani

Kuna pahala tunakwama tungependa mtupe ufafanuzi aseee
 
Kichana eti 500-400-300-200 ukikaa vibaya.
Ndiyo maana tunaambiwa tunatakiwa tufanye utafiti kabla ya kuanza kufanya jambo/kazi fulani na bei/gharama zikiwa ni kitu mojawapo cha kujua mapema kabla hujaanza. Kama wanajamvi walivyosema kwenye comments za mwanzo mwazo wa huu uzi, ni kwamba si kila aina ya ndizi ina bei nzuri. Lakini pia katika biashara yoyote ile huwa kuna msimu ambao bei huwa zinashuka kuliko misimu mingine hiyo ni kawaida katika biashara yoyote ile hapa duniani. Cha msingi ni kuangalia tu kama demand/uhitaji wa hiyo bidhaa bado utaendelea kuwa mkubwa katika kipindi kijacho kirefu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom