Ushauri wa Gerald Hando kuhusu tiktok ni mwiba kwa uhuru

Nyie ambao hampendi uhuru hamieni Korea Kaskazini, Afghanistan, Iran, China na nchi za mfano huo. Msitake kuwaweka watu wote kwenye chungu cha ujima, udikteta na ufashisti.
Kila kitu kina limitation, na kila jamii ina tamaduni zake. Ndio maana hata unaambiwa una uhuru lakini jaribu tembea barabarani ukivuta bangi uone kama unao uhuru wa kiasi hicho. Hatua zisipochukuliwa si kwa serikali tu hata kwa jamii na wazazi wenyewe, tunaenda kutengeneza jamii ya kizazi ambacho ipo siku tutaanza kujiuliza tumefikaje hapa.
 
Si TikTok pekee hata upuuzi uitwao Instagram, Telegram, Facebook ni uozo mtupu.

JF, LinkedIn, Sky sports, Goal.com ndiyo Apps sahihi kidogo na Twitter.
Mitandao hiyohiyo unayosema haifai ndio ina waingizia pesa wamiliki...

Watumiaji ndio wenye shida.

Mitandao haina shida.

Kwanza hata huko instagram, facebook kuna page za kuamua uzi follow ama uache...

Mtu akiamua ku follow udaku halafu aseme mtandao mzima unashida, ni yeye mwenye Shida...

Kuna page nzuri za kufundisha kwenye hiyohiyo mitandao ya facebook na instagram...
 
Telegram ndo kuna biashara za kuuza nyuchi, usichanganye mambo
Hujaelewa, nimesema mabinti siku hizi wamegeuka wadangaji kwa sababu ya yale maisha ya instagram wanayoyaona wenzao wanaishi. Hawajui kutofautisha kipi kweli kipi uongo. Si telegram tu, tinder, escort na kwingineko wanauza na bei wameweka.
Kama jamii inabidi kuwa responsible si kuacha maji yafuate mkondo wake. Hili ni bomu linahesabu muda kulipuka.
 
Kila kitu kina limitation, na kila jamii ina tamaduni zake. Ndio maana hata unaambiwa una uhuru lakini jaribu tembea barabarani ukivuta bangi uone kama unao uhuru wa kiasi hicho. Hatua zisipochukuliwa si kwa serikali tu hata kwa jamii na wazazi wenyewe, tunaenda kutengeneza jamii ya kizazi ambacho ipo siku tutaanza kujiuliza tumefikaje hapa.
Tamaduni gani mpya ambazo hazikufai au hazifai kwa jamii yako unaona zimeletwa na mitandai ya kijamii hadi utake mitandao ifungiwe??
 
Hata bunduki haina shida wenye shida ni watumiaji ! Kwanini imetungiwa sheria ya matumizi na sio haki ya kila mtu kuwa nayo?
Tayari kuna sheria nyingi za kudhibiti vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, wakati wengine wanaona hizi sheria zimepitiliza nyie wengine mnafikiri hazitoshi mnataka mitandao kufungiwa kabisa!
 
Hata bunduki haina shida wenye shida ni watumiaji ! Kwanini imetungiwa sheria ya matumizi na sio haki ya kila mtu kuwa nayo?
Wakati wanaunda Tik-tok kwani ilikuwa inajulikana kwamba mtandao huo utaleta mmomonyoko wa maadili?

Bunduki ni silaha, Wakati inaundwa ilifahamika wazi inaweza leta maafa na madhara isipo wekewa sheria.

Sasa Tik-tok ni mtandao hauna madhara yeyote ya kibinadamu.

Kila kitu kina madhara, hata hii JF ina kasoro zake na mapungufu yake.

Sasa kwa mfano thread kama kula tunda kimasihara, ipi ni Sexual fantasy yako n.k maudhui yake yana maadili kweli?

Je kupitia nyuzi hizi, Uta conclude kwamba mtandao mzima wa JF una haribu maadili?

Vivyo hivyo kwenye Tik tok, kuna maudhui yafaayo na yasiyo faa.
 
Marekani hawajaribu kuzuia tiktok kwa sababu za maadili, ni uongo mkubwa na upotoshaji unaofanywa na huyo hando.
Tiktok inaandamwa Marekani kwa sababu za kisiasa tu.
Yule akiona kitu kinakuja juu ambacho kinatoka nje lazima atoke na porojo nyingi,watu huamini maneno yao ref:huawei
 
Back
Top Bottom