Ushauri wa Bure: Usinunue gari hizi mkononi

Multi-skilled

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
1,030
Reaction score
3,855
Ewe mtanzania mwenye kuhitaji gari BAJETI NDOGO ya mkononi kwa mtu kwa ushauri usijaribu kununua gari mkononi mwa mtanzania mwenzako isipokuwa kwa gari zifuatazo.

1. Toyota premio, Toyota allion, Toyota corolla x, corona premio, Axio, Toyota carina ( Mafundi tele, spare tele na cheap, zina mifumo rahisi ya gear box na engine)

2. Toyota ist, Toyota Runx, Toyota allex, Toyota spacio, Toyota Rumion, toyota vitz. ( fuel economy, mifumo rahisi, mafundi na spare za kutosha.

Pia neno langu sio SHARIA nimetoa ushauri kulingana na uzoefu wangu especially kwa wale wenye VIPATO vya chini.

KAma unanunua mkononi kwa mtu KAA MBALI NA
Anything BMW, Anything AUDI, SUBARU, Baadhi ya MAZDA, BENZ.

Narudia kusema neno langu sio sharia ni ushauri kutokana na uzoefu kama una kipato cha kawaida na ungependa gari yako iongozane na wewe kila sehemu sio ipaki kama pambo

IMG_6049.jpeg
 
View attachment 3518522
Kwa Manual Car Ni Zipi bora Mkuu
 
Mnaosema tusinunue magari used, wale matajir wanaobadilisha magari Kila baada ya miezi 6 watayapeleka wapi?
Nafikiri magari used usinunue bei sawa na bei ya sokoni. Mfano gari sokon ni 35M, ukiuziwa 10-12M baada ya kuikagua na fundi wa uhakika sio mbaya
 
Nunua tu mkuu Gari used lakini kuwa makini na aina ya gari usijeuza tena kwa bei ya chini zaidi
Mnaosema tusinunue magari used, wale matajir wanaobadilisha magari Kila baada ya miezi 6 watayapeleka wapi?
Nafikiri magari used usinunue bei sawa na bei ya sokoni. Mfano gari sokon ni 35M, ukiuziwa 10-12M baada ya kuikagua na fundi wa uhakika sio mbaya
 
Hujaongea chochotr kuhusu NISSAN mkuu
Point yangu kubwa ilikuwa wenye kipato kidogo Mkuu NISSAN used kwa Tanzania utapata shida hasa XTRAIL, MURANO, FUGA, TEANA, PRIMERA na BLUE BIRD may be kama utaagiza japan lakini mkononi mwa watu ni maumivu Hasa MURANO, JUKE na XTRAIL utakabidhiwa gari yenye marekebisho yatakayo shtua moyo au kukutia umasikini kabisa hii ni kwa sababu magari haya yanahitaji Uangalizi wa mara kwa mara na wabongo wengi hawana habari Na gari zinazoweza kuvumilia wavivu wa service nyingi ni za toyota
 
Back
Top Bottom