Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep Quite!, Don't Ridicule Them!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,583
Reaction score
134,220
Wanabodi,

Kwanza nampongeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe kwa ushindi wa kishindo mahakamani leo kwenye kesi dhidi ya Chadema!.

Tangu day one niliwaeleza humu kuwa maamuzi ya CC ya Chadema, ni maamuzi ya kipuuzi kabisa sijapata kuona!, niliuliza hiyo CC ilipata wapi mandate ya kumvua ZZK madaraka yake wakati haina uwezo huo?!. Kesi ya msingi nayo pia atashinda!, Chadema italazimishwa kumrejeshea vyeo vyake vyote, kisha ufuate utaratibu rasmi kumvua vyeo hivyo na hatimaye kumvua rasmi uanachama wake!.

Ushauri wangu wa bure kwa Zitto, nakuomba sana, be calm, keep quite, don't boast, don't ridicule Chadema!. Pia usiendelee kutoa siri nyingine zozote za viongozi wako zaidi ya zile ulizokwisha toa!.

Sijapenda jinsi ulivyo toa siri za M/Kiti wako alivyopokea mihela ya Rostam na Mkono!. Sijapenda 'ulivyonunua' lile gari la Mkono bila kueleza popote umelinunuaje na kwa nini ulinunue kwake!, na pia sijapenda jinsi 'unavyolikodisha' lile gari jingine, huku ukiendelea 'kulilipia bila matatizo' bla kueleza lolote!.

Nakushauri baada ya kushinda kesi hii ya pingamizi, pia utashinda ile kesi ya msingi, ila Baraza Kuu, litakuvua rasmi vyeo vyako vyote na litakuvua uanachama wako, ambapo nafahamu utarudi tena mahakamani kuweka pingamizi mpaka 2015!.

Kwa vile umeishajua mustakabali wako Chadema na kiukweli hatimaye utaondoka, sisi baadhi ya tunaokukubali, tunakuomba na kukusihi, usiendelee kuibomoa Chadema!. Chadema ina wenyewe ambao udini kwao sio tatizo, ukabila kwao sio tatizo wala ukanda kwao sio tatizo!, pigania haki yako, ili uondoke Chadema kwa heshima bila kunyea kambi!.

Narudia tena, hongera sana Zitto Zuberi Kabwe!.

Congratulations!.

Pasco.

---------------------------

 
Pasco stop noising to the stiff-necked, big headed deaf
 
Last edited by a moderator:
Pasco,

Nia na madhumuni ya huu ushauri unaujua mwenyewe ila ki ukweli sidhani kama unachukia utumwa.Just my perception
 
Mkuu Pasco kesi ya msingi ni ipi?
 
Last edited by a moderator:

Pasco una hekima sana! Pia busara unayo na pia ueledi wa hali ya juu! Pia mtu wa kuona mbali!
 
Huwezi Kumbomoa kwa njia za uonevu kiongozi aliyejitolea kwa moyo wake wote kukijenga chama halafu hicho chama kikabaki salama.

Tokea mwanzo watu tuliona wazi hili ni Jungu tu anapikiwa Zitto ili "Wenye Chama chao" waendelee kukiongoza chama kama kampuni yao ya mfukoni.

Kumfukuza Uanachama wanaweza, Lakini hii itaonyesha kwa Umma kwamba hiki si chama cha watu makini, kimejaa wababaishaji, wenye choyo, chuki na Husda.
 
Tulisema lisu hana anachojua sheria anazichangaya halafu anawachanganya na wenzake ona sasa aiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu kweli.
 

Kuna wimbo mmoja wa wanamapinduzi wa rege zamani unasema "hipokrit i love u" umeusikia? Je una maana yeyote kwako?
 

Kwa uzi wako huu na nyuzi nyingine nyingi nashauri JF liunde jopo lake la ushauri sio kila member akivimbiwa na maharage ya mama ntilie anapost kama anavyojisikia!
 

Mpongeze na David Mataka...
 

mkuu unaonaje huyu kijana zitto aingie ccm na ajiunge ktk orodha ya wasaka uraisi the like of EL?
 
Tusisahau, umeme juu,Gasi juu na subirini impact yake viwandani,Mashambani n.k ili tujifunze kusimama na kushabikia ya msingi.Huyo Zitto anakwenda kunywa mvinyo wake baada ya ushindi na Msando alafu waandamanaji watakutana na giza majumbani mwao baada ya luku kukata ghafla kutokana na kuweka umeme wa kuungaunga!

Watanzania haya yanafaa kuwa madogo na yale yanayogusa maisha yetu yawe makubwa! Gesi 65,000/= , Umeme unit 8 ni 10,000/= , maji hakuna wiki sasa alafu habari kama hizi ndio zinageuka BIG ISSUE!

Acha watukaange hadi tutie akili na ikibidi sembe kilo moja iwe laki na maharage hivyo hivyo!!!!!!!!!!:doh::doh::doh::doh::doh:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…