Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,364
Mh Lissu ni mmoja kati ya wabunge wanaochangia sana bungeni. anajituma sana na hili ni jambo zuri! tatizo alilonalo ni kuwa na papara ya kuchangia. ni vizuri akatulia na kutamka maneno yenye uhakika. jana alipokua anachangia hotuba ya uchukuzi, lissu alimlaumu waziri mwakyembe kwa kutotoa kauli ya pole kutokana na ajali ya meli znz. alimtaka aombe radhi na aeleze kwa nini ktk hotuba yake hakutaja ajali hiyo.
alisimama mbunge wa ccm na kunukuu ukurasa ambao una maneno ya pole kutokana na meli ya znz. lissu alinywea na kuomba radhi. lissu licha ya kuwa mwanasheria ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.
Cheo hicho kinahitaji mtu makini anaetumia ubongo kwa umakini mkubwa. Mifano ya kuteleza kwa Lissu bungeni ni mingi. takriban kila anaposimama lazima ateleze. nawashauri chadema kumteua mnadhimu mwengine la sivyo hadhi ya chadema itazidi kushuka bungeni kila uchao
wakatabahu: wakuziba
mzee wa maneno ya ukweli unao choma nyoyo
Unashangaa hiyo mbona malipo ya NSSF hadi kufikisha umri wa kustaafu (miaka 55) yalipitishwa bila wabunge kujua?