Ushauri wa Bure kwa TRA: Wote Waliolipwa Fedha za Escrow Wanapaswa Kuzilipia Kodi ya Mapato

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,770
2,000
Nashangaa hadi sasa TRA wako kimya juu ya watu waliodhihirika kulipwa mamilioni kwa mabilioni ya fedha za Escrow, kuanzia mawaziri, viongozi wa dini na kadhalika. Ukweli ni kwamba kwa hao watu wote waliolipwa, fedha hizo ni mapatao yanayostahili kulipwa kodi, na hivyo walistahili kuya-declare kwa TRA ili wakatwe kodi (income tax) zinazostahili kulingana na fedha walipolipwa.

Hivyo basi kuna mambo mawili hapa; kwanza ni kuangalia kama fedha hizo ni "proceeds of a crime" ili wazirudishe zote au kutaifishwa mali zao; na pili, kama ni fedha halali wamelipwa basi zinastahili kukatwa kodi ya mapato.

Sie wafanyakazi tunakatwa kodi mishahara tunayovujia jasho wakati watu wanalipwa fedha za wizi kiulaini kabisa na TRA hamuwakati kodi. Hii sio sahihi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom