Ushauri wa Bure kwa TBC1! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa Bure kwa TBC1!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by LordJustice1, Nov 17, 2011.

 1. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi nimeona TBC1 wakiwaalika wabunge wa CCM na CUF katika kipindi cha Jambo Tanzania na mara nyingi Wabunge hao wamekuwa wakijaribu kujibu hoja zilizotolewa na CHADEMA Bungeni na kutoa lawama kwa chama hicho kikuu cha upinzani! Lawama nyingi za CCM na CUF zimekuwa hazijibu hoja za CHADEMA moja kwa moja bali zimekuwa ni 'calculated move' ya kukipaka matope CHADEMA!
  Unless TBC1 nacho ni chombo cha kisiasa, nashauri wawe wanawaalika na Wabunge wa CHADEMA ili kupata upande mwigine wa shilingi!
  Au mnasemaje wakuu?
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uko sawa mkuu,Hata mimi sijui kwa ninin hawa tbc wanafanya kitu namna hii. Watuhumiwa ni CDM, kwenye kutoa maelezo hawaitwi, wanaitwa watu wale wale, sasa sisi wanamchi ambao tbc ni ya kwetu, tutapata wapi maelezo ya upande wa wanaotuhumiwa?? Wabunge wa ccm walobaki bumngeni hawajadili huu muswada, na badala yake kila anayesimama ni kumshabulia MH. Tundu Lissu personally. Wengine wamekwenda mbali hata kuhoji weledi wake kwenye sheria, tena kwa kebehi. Mh Lissu ni msomi aliyebobea kwenye fani yake: WaTanzania wanajua hivyo na dunia nzima inajua hivyo!!Hii siyo haki kabisa,TBc angalieni mnachokifanya hakisaidii katika kumaliza utata huu. Kama alivyosema Machali wa NCCR, wananchi ndo wanaotaka muswada huu ungesomwa mara ya kwanza. Kwanini serikali ina haraka kupitisha?? Hii katiba ni ya wananchi na ndiyo wanaotaka washirikishwe katika hatua hii, kwa nini serikali inyoitwa "sikivu" imeziba masikio katika hili?? Kunakitu hapa. Tunawasubiri hao wabunge wa ccm warudi tuwaulize walikuwa wanawakilisha mawazo ya nani kwenye huu mchakato. Labda wote wabaki huko huko Dodoma au wakimbilie Dar kama walivyozoea.
   
 3. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ni hii hii katiba tunayojaribu kuiepuka ndio inayowafanya TBC wawe vibaraka wa CCM. Katiba hii ya kale inampa mamlaka Rais kuteua watu muhimu na wenye nguvu kabisa ktk MIKOA na WILAYA na kuwafanya wawakilishi wake kwa wananchi badala ya wao kuwawakilisha wananchi kwake. Kwa maneno mengine hawa WAKUU WA MIKOA na WILAYA hawawajibiki kwa wananchi badala yake wanawajibika kwa Rais aliyewazawadia vyeo. Kwa minaajili hii, kujipendekeza kwa serikali ni sera binafsi ya kila mfanyakazi wa idara nyeti ktk habari ili siku moja awe kama Betty Mkwasa, Halima Kihemba na wengineo ambao kwa kuongea kwao vizuri kuhusu serikali wamezawadiwa. Unaweza kuona juzi hapa Betty Mkwasa ambaye kitaaluma ni mwanahabari, alikuwa mstari wa mbele kuwazuia wanahabari wenzake kufanya kazi yao ktk tukio la uvunjaji wa kihuni wa nyumba pale DODOMA. Huu ni ukibaraka ambao Watanzania inabidi tuukemee kwa nguvu zote.
   
 4. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Hili halina shaka. TBC1 wanakasoro kubwa tena kubwa. Nadhani wamekusoma
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hawa watu watakuwa wanaogopa yaliyompata Tirdo Muhando, sio bure!
   
 6. m

  ma2ngwa Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli tbc hata mimi nimenote hii ila wajue kuwa ccm haitakuwapo milele na hawana uhakika kama hata kesho,wiki ijayo,mwezi ujao,mwaka ujao ama miaka ijayo hiyo ccm itakuwepo wanatakiwa watende haki hao wanaowabagua wanaweza kuwa ndo viongozi wao sasa sijui wataacha kazi ama??wajirekebishe wananchi tunawaona!!!!!!!
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mambo yote haya tunaweza kuyaweka katika neno moja KATIBA. Katiba ya sasa inawapatia CCM mamlaka ya ku-hire and fire mtu yeyote wanayeona hafanyi kazi za CCM kwa nafasi waliyompatia. Hawa TBC kama waganga njaa wengine wanatetea unga wao kwa mabwana wao waliowaweka. Usitarajie TBC kuwa huru na haki kwa hali ya sasa.

  Kama TBC ingekuwa na Board yake iliyohuru inayoendeshwa kitaalam ingeajiri wataalam. TV za wenzetu kama BBC et al. Habembelezwa mwanasiasa hata awe ni mtawala.
   
 8. babad

  babad Member

  #8
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata mimi nimeliona hili siku nyingi na linanikera.Angalau ITV,MLIMANI TVna STARTV wanajitahidi kutuelimisha.Kweli TBC ya ukweli ilikuwa ya TIDO na hii ya sasa ni ya CCM kwani hata watangazaji wake wameshakuwa empty kimitazamo
   
Loading...