Ushauri wa bure kwa vijana waliomaliza vyuo

chiyelu

Senior Member
Mar 1, 2023
157
407
Salaaam..wana jukwaa! Niende Moja Kwa Moja kwenye hoja yangu, Kumekua na ongezeko kubwa la vijana wanao maliza VYUO na upatikanaji wa Ajira umekua mdogo sana .

Kama kijana unaweza kufanya haya ya fuatayo yatakusaidia.

1. Jichanganye na watu ambao unawaona hawana Elimu. Hili ni kundi kama Bodaboda, Mama ntilie ,machinga n.k.

Hawa watu inawezekana kweli hawana Elimu ya darasani lakini wanaijua Elimu ya kitaa ..wanajua machimbo na fursa nyingi pia Wana uzoefu mzuri na kitaaa unaweza pata mawazo kwao.

2. Anza na kidogo
Vijana wengi wanao maliza VYUO Wana ndoto za kufanya makubwa sana.mara nyingi hata unapokutana nao na kuwahoji kuhusu ndoto zao ..huishia kusema wamekosa mitaji. Anzeni Kwa mtaji mdgo hata wa laki 2 . vijana wengi hutumia muda mwingi kutafuta mitaji mikubwa kitu ambacho kina wakwamisha wengi.

3. Rudi kijijiji jihusishe na kilimo
Nenda kijijiji kwako kama ni Namtumbo,Parangu kokote... Anza kilimo kidogo kidgo inategemeana na aina ya mazao mfn .Mahindi Lima heka 2 au 3 najua utaweza . Simamia vizur ukivuna mwaka unao fuata utalima 5 kidgo kidogo utatoka.

4. Ishi Maisha ya uhalisia wako
Vijana wengi wa VYUO wanapokua VYUO huchangamana na na watu tofauti tofauti. Wanapo maliza VYUO huendelea na maisha Yao ya kuingiaza ya chuo.kitaa kinahitaji uhalisia sio maigizo.

5. Kubali kua plan A imefeli
Ieleze nafsi yako huku ukiwa unasikitika kua Ajira selikalini nimekosa.hivyo huna budi kutumia plan B au C Ili maisha yaende. Kumbuka umri unasonga haungoji mipango yako.

6. Punguza kujilaumu na kulalamika

Vijana wengi ukikutna nao kusota Kwa maisha lawama zote ni Kwa selikali. Punguza lawama Anza kuchukua hatua.

NB: Hakuna chama wa selikali itakuja kubadili maisha yako ...mabadiliko yanaanza na wewe!
 
Jmaa anadanganya vijana wetu.
Waambie vijana kupambana kunaanza sasa,
Tembeza bahasha, jihusishe kila kona, hakuna kujishusha, Ishi na watu wa kada uliyosoma. Nenda hata intern. Mwanzo ni sasa, uza simu, uza nguo hizo ndio plan B.
A endeleza ulichograduatia
Vijana wenu tunao mwaka wa 5 huu huku mitaani Elimu za kwnye makaratasi haziwasaidii maisha n magumu Sana kwao
 
Back
Top Bottom