ngongoti2000
JF-Expert Member
- Nov 20, 2017
- 2,235
- 2,124
Nilimsikia kwa kumuona kwenye TV Mh Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejeiment ya Utumishi wa Umma, Mary Mwanjelwa akizungumzia kwamba sasa watumishi watapimwa kikamilifu utendaji wao kwa kupitia mfumo wa Open Performance Review And Appraissal System (OPRAS) .Napenda kutoa angalizo kwamba kwa sasa kuna baadhi ya taasisi yanautumia mfumo huu lakini una mapungufu makubwa sana. Nimeshuhudia baadhi ya watu wanasubiri wakati wa OPRAS ili kukomoana, hivyo huwa hakuna uhalisia kabisa. Na wengi wa watumishi hawajapata mafunzo au walipata mafunzo haya muda mrefu nyuma hivyo hata utekelezaji wake unakuwa hauna tija wala uhusiano wa moja kwa moja na uhalisia wa utendaji wake.Kwa hiyo kama mnataka mfumo huu uwe na tija na ufanisi wa ukweli kwanza kabisa kunahitajika mafunzo kamilifu na pia ufuatiliaji wenye vigezo vyenye haki na usawa.
Nawasilisha.
Nawasilisha.