Ushauri wa bure kwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuhusu OPRAS

ngongoti2000

JF-Expert Member
Nov 20, 2017
2,235
2,123
Nilimsikia kwa kumuona kwenye TV Mh Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejeiment ya Utumishi wa Umma, Mary Mwanjelwa akizungumzia kwamba sasa watumishi watapimwa kikamilifu utendaji wao kwa kupitia mfumo wa Open Performance Review And Appraissal System (OPRAS) .Napenda kutoa angalizo kwamba kwa sasa kuna baadhi ya taasisi yanautumia mfumo huu lakini una mapungufu makubwa sana. Nimeshuhudia baadhi ya watu wanasubiri wakati wa OPRAS ili kukomoana, hivyo huwa hakuna uhalisia kabisa. Na wengi wa watumishi hawajapata mafunzo au walipata mafunzo haya muda mrefu nyuma hivyo hata utekelezaji wake unakuwa hauna tija wala uhusiano wa moja kwa moja na uhalisia wa utendaji wake.Kwa hiyo kama mnataka mfumo huu uwe na tija na ufanisi wa ukweli kwanza kabisa kunahitajika mafunzo kamilifu na pia ufuatiliaji wenye vigezo vyenye haki na usawa.
Nawasilisha.
 
Mwaka wa 15 najaza hayo makitu, kibaya zaidi huwa nakopi na kupaste ya mwaka uliopita, sijawahi kuona athali yake au hasi wala chanya! Wewe jaza wape, nenda zako kutafuta kibarua cha kujazia kwenye mshahara! Wabunge na wanasiasa ndio wanakula keki ya Taifa, huku kwingine tunakamuliwa tu kupitia income tax!
 
Mleta mada umesema kweli bila chenga opras ni shida sana ,alafu ata upatikanaji wakuu wa idara uko kwenye mahalmashauri kuna tuhuma utumishi +tamisemi kuweka watu wao Kwa vifigisu......
 
Kwani upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma kwa OPRAS si umekuwepo muda mrefu? Kwanza kwenye taasisi nyingi za serikali wengi wa wasimamizi wa idara, vitengo au walio chini yao hawajui kabisa kujaza hizo form za OPRAS. Sina hakika tangu zimeanza kutumika kama zimekuwa na impact yoyote chanya kwenye ufanisi wa kazi hususani kwenye hizi halmashauri zaidi ya kuendekeza rushwa, wizi wa fedha za miradi, uvivu, upendeleo, ufuska miongoni mwao, majungu n.k.
 
Nilimsikia kwa kumuona kwenye TV Mh Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejeiment ya Utumishi wa Umma, Mary Mwanjelwa akizungumzia kwamba sasa watumishi watapimwa kikamilifu utendaji wao kwa kupitia mfumo wa Open Performance Review And Appraissal System (OPRAS) .Napenda kutoa angalizo kwamba kwa sasa kuna baadhi ya taasisi yanautumia mfumo huu lakini una mapungufu makubwa sana. Nimeshuhudia baadhi ya watu wanasubiri wakati wa OPRAS ili kukomoana, hivyo huwa hakuna uhalisia kabisa. Na wengi wa watumishi hawajapata mafunzo au walipata mafunzo haya muda mrefu nyuma hivyo hata utekelezaji wake unakuwa hauna tija wala uhusiano wa moja kwa moja na uhalisia wa utendaji wake.Kwa hiyo kama mnataka mfumo huu uwe na tija na ufanisi wa ukweli kwanza kabisa kunahitajika mafunzo kamilifu na pia ufuatiliaji wenye vigezo vyenye haki na usawa.
Nawasilisha.
wewe unafanya kazi serikalini au?
 
Mwaka wa 15 najaza hayo makitu, kibaya zaidi huwa nakopi na kupaste ya mwaka uliopita, sijawahi kuona athali yake au hasi wala chanya! Wewe jaza wape, nenda zako kutafuta kibarua cha kujazia kwenye mshahara! Wabunge na wanasiasa ndio wanakula keki ya Taifa, huku kwingine tunakamuliwa tu kupitia income tax!

Nakuelewa...tatizo kuna uonevu unafanyika baadhi ya sehemu za kazi kwa kisingizio cha OPRAS....lakini OPRAS ina vipengele vingine mfano uhitaji wa mafunzo nk ambavyo huwa havileti impact yeyote
 
OPRAS haina umuhimu wowote katika utendaji wa mtumishi wa umma ingekua vema endapo mamlaka husika ikatoa reward kwa better performance na penart kwa upande wa underperformance baada a kujazana hakuna kinachoendelea ipa iyo OPRAS inatumika baadhi ya taasisi za umma pekee
 
OPRAS haina maana kabisa.. I believe, serikali hii itafutilia mbali kabisaaa
 
Kwani upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma kwa OPRAS si umekuwepo muda mrefu? Kwanza kwenye taasisi nyingi za serikali wengi wa wasimamizi wa idara, vitengo au walio chini yao hawajui kabisa kujaza hizo form za OPRAS. Sina hakika tangu zimeanza kutumika kama zimekuwa na impact yoyote chanya kwenye ufanisi wa kazi hususani kwenye hizi halmashauri zaidi ya kuendekeza rushwa, wizi wa fedha za miradi, uvivu, upendeleo, ufuska miongoni mwao, majungu n.k.
duh!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom