Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la Richmond!, Bora Ujikalie Kimya!

Status
Not open for further replies.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Nimeusoma waraka wa
Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb) Waziri wa jumuiya ya ushirikiano wa Afrika Mashariki.
WARAKA WA DK. HARRISON MWAKYEMBE( MB), WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI...

POLE SANA MNAOPOTEZA MUDA KUWASHABIKIA MAFISADI KAMA LOWASA KWA NGUVU YA FEDHA.
Nalisema hili bila kukemea jicho wala kuwa na wasiwasi wowote na maisha yangu kwani najiamini na mwenyezi mungu ananilinda na watanzania wananiombea daima na najisikia furaha kuwa miongoni mwa wabunge wa CCM ambao hatukuufumbia macho ufisadi wa kampuni feki la kuzalisha umeme iliyomuhusisha waziri mkuu ambaye mimi namuita aliyejiuzulu na sio kustaafu.
Namuona Lowasa kama mtu ambaye anatapatapa huku akiujua ukweli kwamba hana nafasi hata kiduchu ndani ya CCM.
Nakushauri ujitafakari vizuri kwani CCM haitoweza kumkabidhi nduli nchi hii.
Unahaha kutumia mabilioni kuhonga na kusafirisha watu kwenye tendo la kutangaza nia tu, hivi unafijiri kamati zote za CCM zina njaa ya pesa zako za kifisadi? Hivi hujui watanzania wakushangaa unasema safari ya matumaini wakati safari hiyo ni ndani ya bahari iliyojaa majoka na mizimu ambayo imejivika ngozi ya kondoo ili iwameze katikati ya bahari?
Nitakuwa wa kwanza kujitafakari na kuitafakari CCM na kuchukua hatua ambayo najua watanzania wasiouza utu wao kwa dhamana ya fedha.
Ninakusubiri kwa hamu ili nikusikie utakavyokuwa unabadili jihanam kuwa peponi, Kwa manufaa ya watanzania nitaanika hadharani uozo wako wote kwa ujasiri na bila hata chembe ya woga ili watanzania wasipotoshwe tena kwa njia ya nbwembwe za fedha. Eh mwenyezi mungu nipe uthabiti kwa hilo.
Rai yangu kwa wana CCM na watanzania tuchague viongozi bora na sio kwa nguvu ya fedha, wapambe na kutembelea nyota ya mtu.
Utauficha wapi uso wako wakati ambapo CCM itakapokuangusha kwa kishindo na kuchagua wawakilishi walio safi? Utapata kiharusi na shock bure kwa kupoteza fedha za madili uliyopiga RICHMOND na ufisadi mwingine.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb) Waziri wa jumuiya ya ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Japo bado sijapata authentication ya waraka huu, hili limesemwa hivyo tayari lipo, hivyo mimi ningekuwa ni mshauri wa Dr. Mwakyembe, katika hii safari ya matumaini, ningemshauri kujinyamazia tuu, kusubiria maamuzi ya vikao vya chama bila yeye kusema chochote kwa sababu ndiye aliyekuwa mwanzo, sitaki aje tena awe mwisho!.

  1. Ni Mwakyembe huyu huyu!.. ambaye ni mwana sheria nguli anayejua kanuni ya kwanza kabisa ya haki ni "no body is condemned unheard", katika ile tume yake ya bwembwe, alim condemn Lowassa bila kumsikiliza!.
  2. Ni Mwakyembe huyu huyu!..Katika uchunguzi wake aligundua wazi kabisa dili la Richmond ni dili la nani, lakini ili kuokoa jahazi mwenye dili lake asijulikane maana ingekuwa ni aibu, ndipo akatafuta mbebaji wa kumtwika zigo la Richmond, kama alivyotikwa YULE aliyebaba dhambi za dunia bila kosa na kuishia kuteshwa hadi kifo msalabani, lakini ni kwa kupigwa kwake sisi tunaponywa, ni vivyo hivyo kwa kuteswa kwa Lowassa CCM imeponywa!.
  3. Ni Mwakyembe huyu huyu!..aliyeishauri serikali kuuvunja mkataba wa Richmond kwa sababu ni kampuni feki, na Tanzania ikashitakiwa wakashinda na Tanzania ikatozwa faini ya mabilioni!.
  4. Ni Mwakyembe huyu huyu!..aliyejiapiza kuwa Tanzania isilipe tozo hiyo na kamwe haitalipa!, lakini ukweli Tanzania imeishalipa tozo ile, na Watanzania wote tunafidia kupitia kupandishwa kwa bili ya umeme!, hivyo Mwakyembe huyu huyu ndiye ameisababishia Tanzania hasara ya mabilioni ya tozo!. Tanzania ingekuwa ni Uchina, saa hizi Jina la Mwakyembe lingeisha kuwa ni historia siku nyingi kwa 'alikuwa!'
  5. Ni Mwakyembe huyu huyu!..aliyejiapiza kwa maneno "over my dead body!", kupinga kununuliwa mitambo ya Richmond au kuitaifisha!...baada ya kulithibitishia bunge kuwa Richmond ni kampuni feki, Zitto akashauri serikali inunue mitambo hiyo au iitaifishe kwa manufaa ya umma.
  6. Ni Mwakyembe huyu huyu!..aliyezawadiwa uwaziri kwa kazi nzuri ya kumhifadhi mmiliki halisi wa Richmond, na kiukweli japo ameboronga kule Uchukuzi, lakini ameendelea kubebwa kwa kuwekwa kwenye wiraza ambayo ni insignificant na haina impact!.
  7. Ni Mwakyembe huyu huyu!..ambaye amelithibitishia bunge kuwa Richmond ni kampuni feki, hivyo kisheria kitu kikisha kuwa feki yaani batili, then ni batili tangu mwanzo kumaanisha hakipo na hakijawahi kuwepo, 'void ab initio' kitu ambacho ni uongo wa wazi wa mchana kweupe kwa sababu hata kama Richmond ni kampuni feki, ufeki wa Richmond ni kwenye makaratasi tuu, ile mitambo ya Richmond sio mitambo feki, na ule umeme wa Richmond sio umeme feki, ni mitambo real na inafua umeme real, hivyo Watanzania tulidanywa!.
  8. Ni Mwakyembe huyu huyu!..aliyeilaani Mitambo ya Richmond, lakini ndiye aliyekuwa akicheza ngoma nyuma ya JK siku ile Obama anazindua Simbion, kwa msiojua Kampuni la Richmond ni jina tuu, ilipokuwa ikiitwa Richmond ilikuwa ni shetani, lakini sasa inaitwa Simbioni, imekuwa ni malaika!, mitambo ni ile ile, umeme ni ule ule na capacity charge ya shilingi milioni 152 kwa siku bado ni ile ile!.
  9. Ni Mwakyembe huyu huyu!..litangazia bunge letu jinsi tunavyoibiwa kwa capacity charge ya shilingi milioni 152 kwa siku, hivyo hii capacity charge ikawa ndio mzizi wa fitna yote ya Richmond, lakini, ni Ni Mwakyembe huyu huyu!.. ambaye sasa amejinyamazia kimya wakati Tanzania tukiendelea kulipishwa capacity charge ile ile na kampuni ya Simbion!.
  10. Ni Mwakyembe huyu huyu!..aliyesema Richmond sio halali lakini sasa anashangilia uhalali wa Simbion, mitambo ni ile ile, umeme ni ule ule, mkataba ni ule ule na capacity charge ni ile ile!, na Watanzia tumenyamaza!.
My Take.
Na kwa msio jua kumhusu Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb), hili ni moja tuula sarakasi za Richmond, ukistaajabu haya, uelewa kuwa haya ni ya Musa tuu ya firauni yanakuja, mkiyasikia ya Tazara hamtaamini, mkiyasikia ya ATCL!, hamtaamini!, mkiyasikia ya TRL mtabaki midomo wazi!. Na hayo yote ni mambo ya kiutendaji, achilia sarakasi za kisiasa kama uasisi wa CCJ , na politics of sensetionalisim!.

Kiukweli ningekuwa mimi ndio Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb), kwenye hili la Richmond, bora ningejinyamazia kimya tuu!, ili nisije kukumbushia au kutonyesha makovu ya kadhia ile yasije kufukunyua na mengine yasiyohusika!.

Kwenye Richmond, Watanzania Tuliumizwa, Tukaumia, Watanzania Tuliteswa, Tukateseka, na hadi sasa donda la Richmond bado ni donda bichi hakijakauka na wala kovu bado kwa sababu Watanzania bado tunaendelea kuumizwa na tunaumia, na bado tunaendelea kuteshwa na tunateseka na ....

Naomba nisimalizie kwa uchungu!.

NB. Kuna thread nyingine huwa ni za majadiliano na kuna thread nyingine ni info pack tuu ili wasio jua wajue kama ilivyo unaposoma gazeti, huwezi kumuuliza kitu chochote mwandishi, hivyo naomba kwa uzii huu, tumchukulie Pasco wa jf kama mwandishi tuu wa gazeti letu la jf, hivyo naomba msiniulize kitu chochote kwa sababu sitajibu kitu kufuatia threa hii kuwa ni info pack tuu!.

Jumapili Njema
Pasco
 
CCM hakuna msafi wote wezi, mafisadi na wapenda rushwa, hawana mgombea asiye na kasoro.
Tumaini la watanzania ni Ukawa, tunawatakia kila la heri viongozi wetu wa Ukawa watuchagulie wagombea wazuri kuanzia udiwani, ubunge na urais.
 
Na mpambano uendelee maana najua Mwakyembe na yeye atakuja na nondo zake mpya.

Ila Pasco, una uhakika aliyeandika huo ujumbe unaotamba kwenye makundi ya Whatsapp na Facebook na hata hapa Jamiiforums na kwingine kwingi ni Mwakyembe kweli?

Msijekuwa mnachezeshwa li-Gwaride na yule wa mdimu. Anyway, mnyukano ni mzuri kwa afya ya TAIFA. Bila msuguano, hakuna maendeleo. Mwisho wa kuwa na miungu watu ni sasa.

red-tailed-racer-close-9.jpg
 
CCM hakuna msafi wote wezi, mafisadi na wapenda rushwa, hawana mgombea asiye na kasoro.
Tumaini la watanzania ni Ukawa, tunawatakia kila la heri viongozi wetu wa Ukawa watuchagulie wagombea wazuri kuanzia udiwani, ubunge na urais.
CCM ni wabovu sana lakini ni wazuri ukiwalinganisha na UKAWA.Hao ni wajasiriasiasa "vyama vyao ni vitega uCHUMI"
 
mwakyembe hawezi andika walaka ambao hauna kichwa wala miguu! hakuna kipya nilichokiona zaidi ya kuona namna mpika habari alibyokosa ujuzi katika kupika mambo.
 
Pasco ni WAKUKURUPUKA TU ili kumchafua MWAKYEMBE.

Lowasa ni FISADI-PERIOD.

KAMWE HAWEZI KUWA RAIS WA NCHI HII-PERIOD
Anachofanya Pasco pamoja na wenzake walioshikwa masikio na Lowassa ni kutafuta platform ya kumsafisha Lowassa kwa kuchafua wengine
 
Last edited by a moderator:
mwakyembe ni aina ya wasomi walioiangusha nchi hii,huko TRL na bandari kasababisha hasara ya zaidi ya trilioni moja,bandari kaleta hasara ya bilioni 800,kwenye mabehewa kaleta hasara ya zaidi ya bilioni 300 na ni ndani ya mwaka mmoja,bado shirika la ndege
 
bado sijaamini kuwa waraka huo ni wa mwakyembe, ila pasco tanzania mazingaombwe ni mengi mno ndio maana kila mtu nchi hii analia ufisadi unaliangamiza taifa miaka lundo lakini jela wanaweza wasizidi wafungwa watano wa ufisadi na kifungo chao hakizidi miaka miwili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom