Ushauri wa Bure kwa Director Modestus Francis Kipilimba

Ushauri wa Bure kwa Director Modestus Francis Kipilimba

Ujumbe wake ni mrefu sana lakini tunamshauri mkuu wa Usalama aimarishe taarifa toka kwa wasaidizi wake huko mikoani wilayani ambapo wengi sasa wanawalinda ma RC na DC na viongozi wengine huko, wamekuwa watetezi wa Maovu mfano huko Tarime mara siku Rais magufuli alipohutubia DC na OCD waliwapora Mabango wananchi kimya kimya hivyo kukosa fursa ya kuanika kero zao mbele ya Rais magufuli, pia OCD amenunuliwa na matajiri wa madini ambapo huenda kwenye migodi yao kuwapiga kuwapora madini na mali zao kisha kuwabambikia kesi ili waogope na pindi wakiwa jela matajiri wa madini hutumia mda huo kupora madini yao na mali zao, hapo ndipo wananchi wanaona idara ya usalama inawalea viongozi wanaowatesa wananchi na kuwabambikia kesi.
Policies and procedure are man made to ensure desired goals are realized. Decisions made on bad policies and standard operating procedures can delay on hinder true patriots who can make a remarkable economic change in motherland Tanzania
 
Taasisi hii kazi yake unajulikana malengo na kazi zake toka kuanzishwa kwake. Ni ngumu kubadilika.

Hii hapo ndio kazi yake kuilinda CCM na mabwana wake mambo ya maendeleo ni ya kwao binafsi. Ni taasisi ya wachumia tumbo tu.
 
Kwanza kabisa nakupongeza kwa majukumu mazito ya kuwa sehemu ya Uongozi wa taasisi ambayo kwa sasa wewe ndiyo mtendaji mkuu.

Nataka kuamini unashaurika kupitia wanaokufahamu, pia hata na watu usiowafahamu maadamu msingi wa ushauri wao umelenga kwenye uzalendo na ujenzi wa taifa letu Tanzania.

Bila shaka kunaweza kuwa na namna nyingi za kukufkishia ujumbe, na bila shaka kuna nyakati ujumbe unaweza usikufikie. Na kuna uwezekano ujumbe ukikufikia, huenda ukawa umechujwa na “context” ya mtuma ujumbe isifikishwe sawia ili kutimiza malengo ya mtuma ujumbe.

Msingi wa kuandika hapa kwako na wasaidizi wako, ni kwa lengo la kuwafanya mtambue na kuwa kila Mtanzania ana uwezo wa kuwa sehemu ya mafanikio ya kuifikia nchi ya “maziwa na asali”. Bill Hybels mmoja wa walimu nguli wa Uongozi anasema, “Everyone has influence. You have influence” Pia Dr. Myles Monroe mara kadhaa amewahi kusema, makaburini ndiko kuna utajiri ambao haukuwahi kutumika. Mimi nataka kuamini, wewe kwa nafasi yako unaweza ku-harness utajiri katika akili za Watanzania ambao bila shaka haujatumika au uko-underutilized.

Nimesikia kutoka vyanzo vinavyoaminika ya kuwa wewe pia ni Mchungaji, na bila shaka biblia ni moja ya kitabu ambayo unakisoma. Kwa muktadha huo, naomba kukufikirisha hadithi kadhaa kutoka katika biblia.

Naomba nikukumbushe hadithi tatu kutoka katika biblia na baada ya hapo ntakurejesha kwenye hoja.

Yusufu mwana wa Yakobo alikuwa mfungwa gerezani. Japo alifungwa kwa kusingiziwa, tunakumbuka, ni “mfungwa huyu” alikuja na suluhisho la kiuchumi kwa Misri ambalo lilikuwa Taifa kubwa kiuchumi na kijeshi nyakati hizo.

Njaa ilikuwa ni kitu halisi kule Misri, na tafsiri ya ndoto hali kadhalika ilikuwa tafsiri halisi. Kuwa kufanya detailed analysis; miaka 7 ilikuwa muhimu kweli kukusanya chakula cha ziada, kujenga maghala ya kuhifadhi chakula, kuweka mifumo ya kudhibiti wadudu wasiharibu chakula. Kuwa na magari yak u-support logistics, kuweka ulinzi ili chakula kisiibwe. Kuwa na mifumo ya kudhibiti moto usitokee ili hifadhi ya chakula isipotee. Bila shaka kukusanya zaida kwa ajili ya ongezeko la watoto Misri na mataifa jirani na Misri ambayo kama yakipata njaa yanaweza kwenda kununua chakula.

Hadithi ya pili ni ya Daudi mwana wa Yese ambae alikuwa mchunga mifugo. Wakati nabii Samuel anafanya mchakato wa kutafuta kiongozi kuchukua nafasi ya Mfalme Sauli, baba yake mzazi hakuona “potential” kama mwanae Daud kama anafaa kuwa kiongozi. Baba alidhania kaka zake ndiyo kumbe hawakuwa watu sahihi kwa kazi ya kuongoza taifa.

Miaka kadhaa baada ya kupakwa mafuta, Daudi amekwenda kwenye “battle ground” kupeleka chakula kwa maelekezo ya baba yake. Alipofika bonde la Soko, kaka yake na Daudi aitwae Eliab alimwona Daudi kwa jicho la mtu mvivu alietoroka mifugo ya mzee Yese kwa lengo la kujionea/kushuhudia “sinema ya bure” ya mpambano kati ya Israeli na Wafilisti.

Wengi tunakumbuka Daudi alimuua Goliath kwa kombeo baada ya watu wengine kupeleka ujumbe kwa Mfalme Sauli kuwa kuna kijana mwenye ujasiri na ari ya kumpiga na kumuua Goliath kama atapata ridhaa ya Amri Jeshi Mkuu. Inafahamika Daudi hakuwa military trained na hakuwa enlisted jeshini kama Eliab (kaka wa Daudi)

Hao waliokuwa na uzoefu wa kijeshi na vita kwa muda mrefu ikiwemo Sauli ambae alikuwa Amri jeshi mkuu, wote walikuwa waoga maana hawakuwa na option (weather ni strategy, methodology au tactic) yoyote ya kumkabili Goliath ambae alikuwa tishio la Usalama wa Taifa la Israel, tishio kwa Ufalme wote na bila shaka tishio kwa kizazi cha Israel baada ya vita. Tishio kubwa halikuwa uwezekano wa kuuwawa kwa atakaejitokeza kumkabili Goliath, bila shaka tishio lilikuwa utumwa ambao Taifa la Israel lingeupata baada ya yeyote ambae angemkabili Goliath kuuwawa na Jenerali huyu nguli na mzoefu wa vita.

Hadithi ya mwisho inamuhusu Jenerali wa Jeshi la Syria kwa jina la Naaman. Naaman alipata habari (taarifa) kutoka kwa mkewe kuwa katika nchi ya Israel, kuna nabii yuko Samaria anaweza kumponya ukoma. Actually, aliemjuza mke wa Naaman, ni “house girl” aliekuwa katika nyumba ya Naaman.

Jenerali Naaman, aliamini na kuchukua hatua ya kwenda kwa nabii Elisha. Alipopata taarifa kupitia msaidizi wa Elisha ya kuwa anatakiwa kujichovya/kujitumbukiza mara saba katika mto Jordan, Naaman alivunjika moyo na hakutaka kufanya hivyo. Ndipo wasaidizi wake wakamsihi kwa nia njema bosi wao, kuwa, what’s a big deal. Kama angeambiwa jambo kubwa si angefanya. Jenerali Naaman baada ya kukubaliana na ushauri wa “aides” wake, alijichovya mara saba na ukoma ukatakasika.

Ushawishi wa kwanza ulitoka kwa “house girl” kwenda kwa mke wa Jenerali Naaman. Ushawishi wa pili ulitoka kwa “Mrs Naaman” kwenda kwa Jenerali Naaman. Hata Jenerali Naaman alipopata maelekezo ambayo hakuyapenda; aides wake waliokoa jahazi kwa kumshawishi bosi wao. Jenerali Naaman, alipo-buy in, alitakasika.

Naomba kumshauri Director Kipilimba kama layman katika mambo machache ya kukuza uchumi wa Tanzania kimkakati, hususan katika miaka hii ya Mhe. JPM ambae amejipambaua kuwafanya Watanzania kuwa “middle class” wa kati kwa kutumia viwanda kama nguzo ya kusisimua/kukuza uchumi.

Ikumbukwe, Daudi wala hakuwa enlisted jeshini, yet mkakati wake wa kumuua Goliath alileta matokeo.

Yusuf pamoja na kukaa kwa Captain Potifa kama mkuu wa wafanyakazi, hakuwahi kushika wadhifa na majukumu ya uongozi mkubwa katika Taifa la Misri. Yusuf alitoa tafsiri ya ndoto, ila mkakati wa hifadhi ya chakula kwa miaka 7 ulikuwa ni matokeao ya creativity, strategic planning na juhudi za Farao aliekuwa mtawala wa Misri kuona umuhumu wa kumjumuisha “mtu wa kuja” kwa kuwa alikuwa na akili ya kutatua matatizo ambayo insiders katika serikali ya Farao walishindwa kuja na majibu ya tafsiri ya ndoto na mkakati wa muda mrefu ya Taifa la Misr kuhifadhi chakula wakati wa neema ya chakula cha ziaada.

Hata yule house girl wa kwa Jenerali Naaman, japo alikuwa utumwani, yet alikuwa na ushawishi wa nia njema kwa bosi wake aweze kupona. Nami niko hapa kama mzalendo kwa nia njema kushauri.

Nadhani sote tutakubaliana pia, ajali ya MV. Nyerere, kisiwani Ukara majuma machache yaliyopita, wavuvi wa ukara (laymen), waliweza kuchukua jukumu la kwanza kuokoa waliokuwa hai na kuwaokoa miili ya watu waliopoteza maisha kabla ya vikosi ya uokoaji kutoka majeshi yetu havijafika visiwani Ukara. Hivyo, kwa lugha yangu ya “U-layman”, bila shaka kuna jambo Director Kipilimba na wasaidizi wako mtaokota.

Toka 1997 wakati dira ya Taifa inazinduliwa na toka JPM atangaze namna ya kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda, sisi kama Taifa je kuna mkakati wa pamoja wa kiuchumi (strategic economic inclusion)?

Je tuna model ya kiuchumi/model za kiuchumi ili kutimiza malengo ya kupata output kubwa katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda?

Moja ya chanzo nilichosoma kutoka maandiko mbalimbali ya model ya kiintelijensia ya kukuza uchumi inasema… If intelligence is the capability of understanding and interacting with the environment in order to act to obtain competitive advantages.

Kuna maeneo kadhaa sisi Tanania tuna “competitive advantage”. Competitive advantage inaweza kuwa realized kwa haraka kama yafuatayo yatafanyiwa kazi

  • To define the strategy, including approach and the task of each countrymen through diverse organizations they are in;
  • To have the capability for abstract reasoning and understanding of the multiple interactions existing in complex environments, including a capability of judgment and knowledge development.
  • To have the capability to detect substitute products or disruptive technology and to understand cultural or demographic changes.
  • To develop the capability to be ahead of changes in regulatory or economic conditions of market dealers in order to launch offensive or defensive actions.
Intelligence must be firstly strategic and then economic. Then, it will be competitive or solely reduced to the analysis previous to knowledge acquisition through the appropriate techniques and technologies.

Ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa pamoja ambao nataka kuamini kuna outsiders ambao wanaweza kuwasaidia akina Dr. Mpango (Waziri wa Fedha) Waziri VIwanda Mwijage na Waziri wa Kilimo Tizeba, Waziri wa Mifugo Mpina na Waziri wa Ajira Mhagama na Director wa TIC Godfrey Mwambe.

Akina Mark Zuckeberg wa Facebook, Jeff Bezos wa Amazon, Jack Ma wa Alibaba ni “outsiders” katika elimu ya biashara na uchumi. Ila uwezo wa kuwa “creative and Innovative” walianza mdogo mdogo, eventually leo hii wamekuwa sehemu ya kukuza uchumi wa nchi zao.

Director Kipilimba, you can adopt a system of human intelligence that obtains information through persons through economic intelligence, business intelligence and competitive intelligence to ensure Tanzania is thriving economically by use of technology and know-how. Part can be locally harnessed and part can be outsourced.

In your course of governing the entity of which you’re entrusted with God and second, you’re entrusted with the President, you can quickly get results by accepting counsels and adopting the economic models to eliminate poverty and unemployment in this country.

If it happened the outsiders like David, Joseph, the house-girl the list goes on made a difference, you can experience the same by opening-avenue for such people. Some are not far away from the battle ground, you just need to head-pick them; some are “imprisoned through false accusation”

Policies and procedure are man made to ensure desired goals are realized. Decisions made on bad policies and standard operating procedures can delay on hinder true patriots who can make a remarkable economic change in motherland Tanzania.

As you stand in position to analyze a lot of human intel from various sectors/dept. under you. There is a potential of relying to a challenge which face Moses which he was receiving a feedback report from spies who visited the “Promise land”. Up-to this moment some people in junior, middle or senior positions who are serving the current regime are coward like the 10 spies. Either they have bad perception or non believers on how we can arrive into middle income earning country.

Sir, you have a real challenge to listen to a few who are bold like Joshua and Caleb. Very fortunate the boss you serve who is Commander in Chief is a true visionary, very bold, courageous leader who is decisive with audacity to see we Tanzania are navigating towards the promise land.

Mungu Ibariki Tanzania.
Mwezi wa October naona nondo nyingi sana, baada ya Nondo za Tundu Lissu, Barafu sasa hii ni nyuzi bora tena kutoka kwa Freddie Matuja.

Bongo lala hapa hawataelewa.
 
Director Kipilimba, you can adopt a system of human intelligence that obtains information through persons through economic intelligence, business intelligence and competitive intelligence to ensure Tanzania is thriving economically by use of technology and know-how. Part can be locally harnessed and part can be outsourced.
Yaani wewe unajifanya mshauri elekezi?
Utamshauri ni wewe Dk Kipilimba na vineno vyako vya kuokoteza mitandaoni?
Ina maana wewe unajua sana au ni bobezi kuliko kipilimba?
Acheni kudharau fani za watu jamani
 
Freddie Matuja hiki ulichokiandika hapa unataka kifanyike hapa Tanzania au labda umewataarifu ' Kijanja ' Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi Nyeti za United States, United Kingdom, Israel, France, Germany, Russia, China, India, Japan na Korea ya Kaskazini? Ngoja Kwanza niangalie ni Majimbo mangapi kutakuwa na marudio ya Uchaguzi kwa siku za karibuni nchini Tanzania.
 
Taasisi hii kazi yake unajulikana malengo na kazi zake toka kuanzishwa kwake. Ni ngumu kubadilika.
Ni lazima ibadilike kulingana na nyakati sasa ni 21st huwezi kuwa na ile system ya zamani ya enzi ya ujamaa wakati sasa tuko kwenye upebari, Nyingi tu zimebadilika, hii kubaki stagnant na kutokubadilika ni shida ingine
 
Yaani wewe unajifanya mshauri elekezi?
Utamshauri ni wewe Dk Kipilimba na vineno vyako vya kuokoteza mitandaoni?
Ina maana wewe unajua sana au ni bobezi kuliko kipilimba?
Acheni kudharau fani za watu jamani

Kwahiyo Mtu akimshauri jambo / kitu Rais Dr. Magufuli ina maana amemdharau au ni ' Mbobezi ' kuliko Yeye au labda anautaka huo Urais? Ningekuwa Mimi ndiyo Wewe haraka haraka ningefuta hiki ulichokiandika kwani ' Kimekudhalilisha ' mno mbele ya Watu wanaojua ' Kufikiri ' hapa Jamvini. Wewe umesema kuwa Jamaa ana ' dharau ' mbona hata Wewe pia kuna mahala hapo umeonyesha ' dharau ' kubwa Kwake kwa kusema kuwa ameokoteza okoteza maneno mitandaoni? Hivi ' Intellectually ' ni dhambi kuyachukua mawazo ya mwingine ukayajengea hoja zaidi yenye mantiki na ukaiwasilisha kwa mtazamo wako? Kuna Watu akili zenu huwa mnaziacha Uchi / Utupu kabisa hapa Jamvini. Siku zingine jitahidi sana katika Kujifunza Kujenga hoja ili uende sawa na Great Thinkers wenzako humu. Na naamini hata TISS DG mwenyewe kwa Upupu / Upuuzi wako huu ' uliotukuka ' amekudharau mno!
 
Tofautisha kumshauri Magufuli na Kumshauri DG wa TISS
Ni sawa na kumshauri papa jinsi ya kusoma biblia
 
Tofautisha kumshauri Magufuli na Kumshauri DG wa TISS
Ni sawa na kumshauri papa jinsi ya kusoma biblia
Usimdharau ushauri wa mtu yoyote dunia chukua kinachofaa kisichofaa acha. Dunia sikuhizi inaendeshwa kwa ubunifu wa watu na vtu unique hata asiye na shule anaweza kutoa mawazo mazuri ya manufaa.
 
Ushauri mzuri sana kaka,point zako tutazifanyia kazi labda mwakani...sasa tupo busy kuama imebaki miezi miwili tu dirisha kufungwa
 
Tofautisha kumshauri Magufuli na Kumshauri DG wa TISS
Ni sawa na kumshauri papa jinsi ya kusoma biblia

Kwani DG wa TISS na Rais Dr. Magufuli nani kamteua mwenzake? Hivi Mkuu hujishtukii tu kwamba Kichwani mwako ' zimepungua ' kidogo? Halafu bado unataka Ubishi / Ligi / Bundesliga. Hebu tulia Kwanza chini kisha taratibu kabisa pitia ile ' post ' yako halafu jiulize je ulitakiwa uiweke hapa Nyumbani kwa ' Great Thinkers ' waliotukuka? Bado hujakomaa katika kufanya ' Logical Arguments ' na ' Critical Thinking ' hivyo si vbaya ukianza Kujifunza taratibu au utuombe tukufundishe hata bila malipo ili siku zingine ukiwa hapa tuwe tunaenda sawa.
 
Usimdharau ushauri wa mtu yoyote dunia chukua kinachofaa kisichofaa acha. Dunia sikuhizi inaendeshwa kwa ubunifu wa watu na vtu unique hata asiye na shule anaweza kutoa mawazo mazuri ya manufaa.
kama huna Taaluma husika ni vigumu sana kutoa ushauri wa maana
Intelijensia si sawa na kuongoza chama au kampuni
 
Mkuu ungeazima materials pia toka kwa yeriko nyerere;

Keshaandika kuhusiana na intelijensia ya Uchumi.
 
Kwani DG wa TISS na Rais Dr. Magufuli nani kamteua mwenzake? Hivi Mkuu hujishtukii tu kwamba Kichwani mwako ' zimepungua ' kidogo? Halafu bado unataka Ubishi / Ligi / Bundesliga. Hebu tulia Kwanza chini kisha taratibu kabisa pitia ile ' post ' yako halafu jiulize je ulitakiwa uiweke hapa Nyumbani kwa ' Great Thinkers ' waliotukuka? Bado hujakomaa katika kufanya ' Logical Arguments ' na ' Critical Thinking ' hivyo si vbaya ukianza Kujifunza taratibu au utuombe tukufundishe hata bila malipo ili siku zingine ukiwa hapa tuwe tunaenda sawa.
Ongea yote,lakini huyo jamaa yako hana uwezo wa kumpa ushauri DG wa Tiss.TISS sio sawa na chama au kampuni,mnakwenda kukariri mitandaoni halafu mnajifanya kushauri wakati hamjui chochote kuhusu hiyo idara, 2015 mlijaribu sana kuielekeza na kuifundisha kazi idara hii,mpaka kamanda Jack Zoka akatoka pangoni.Nendeni mkawashauri polisi jinsi ya kutoa dhamana huko vituoni
 
kama huna Taaluma husika ni vigumu sana kutoa ushauri wa maana
Intelijensia si sawa na kuongoza chama au kampuni
Kabombe umecremisha hujui tu dunia vtu vingi vinafanyaje kazi ungeelewa hivo ungetoka kwenye hayo mawazo. Hafu ujue kuna vichwa sana sema havijapata nafasi kulingana na mifumo yetu hii ya kubebana, hasa inaposhindikana Ku recruit best candidate. So ukisema huyu hafai kutoa ushauri ur very wrong.
 
Kwenye ku recruit wapo makini sana na mtu akikiuka anaondolewa
Huyo jamaa amekiri kabisa kuwa yeye ni layman,masuala mengine si ya kuleta utani
Nijuavyo mimi layman anaweza kutoa ushauri wa nguvu kwenye kikao cha mazishi au harusi sio kumpa ushauri DG wa TISS
 
Ongea yote,lakini huyo jamaa yako hana uwezo wa kumpa ushauri DG wa Tiss.TISS sio sawa na chama au kampuni,mnakwenda kukariri mitandaoni halafu mnajifanya kushauri wakati hamjui chochote kuhusu hiyo idara, 2015 mlijaribu sana kuielekeza na kuifundisha kazi idara hii,mpaka kamanda Jack Zoka akatoka pangoni.Nendeni mkawashauri polisi jinsi ya kutoa dhamana huko vituoni

Your STUPIDITY has just been CERTIFIED internationally.
 
Your STUPIDITY has just been CERTIFIED internationally.
Punguza povu sio lazima anachoongea mwenzio ukubali unaweza pia kupita kimya
Naona una hasira sana nchi yako pendwa ya Rwanda siku hizi toka Kipilimba ameingia mmeshindwa kabisa kunusa unapikwa mchuzi wa mboga gani
Rwanda ilifikia inaua watu south Africa,kwa kiburi kabisa inasema ni maofisa wa Tanzania ndio wameua.
Rwanda waliandika barua ICAO kuomba kulitawala anga la Tanzania
Ni kipilimba aliekataa na kushauri tununue radar nne za kijeshi ,zifungwe Dar,Songwe,Kia na Mwanza kwa dola milioni 60,Mkandarasi wa kifaransa yupo site,Rada ya mwanza tu ina uwezo wa kuona anga lote la Rwanda,ndio mana mapovu na matusi tu yanakutoka
 
Back
Top Bottom