Ushauri wa Bure kwa Director Modestus Francis Kipilimba

Ushauri wa Bure kwa Director Modestus Francis Kipilimba

Assumption ipi hiyo??
Kwamba hawa watu viongozi serikalini wana nia nzuri, lakini hawajui hili nalile tu, wakijua, watabadilisha mambo wafanye vizuri.

Serikali ina watu wanajua mambo kuliko watu wengi wanavyoelewa, ina mahabari kibao ambayo watu hawana.

Watu wanaposhindwa kufanya vitu, mara nyingi ni uchaguzi wao tu, si kwamba hawana habari.

Kuna rafiki yangu mmoja, jamaa yuko nzuri, familia bora, kasoma mpaka Harvard, halafu kabalance maisha yake vizuri sana, usomi anao, utoto wa mjini anao, halafu mtu mmoja down to earth sana mtu wa kujichanganya mtaani, alikuwa anafanya kazi mpaka na watoto wa mitaani.

Akawa bonge la advocate mambo ya elimu, kafanya ma research kibao, akawa bonge la activist.

Akawa anaona serikali haijui mambo, akipata nafasi ya kukaa na wakubwa tu, atawashauri vizuri, watabadili mambo.

Basi, alivyokuwa well connected, Kikwete akamuona, akampa appointment, akawa mshauri wa rais mambo ya elimu au something like that. Ile ana direct access na mkulu mwenyewe JK.

Ndipo hapo alipogundua, kila anachosema, anaambiwa hicho tunakijua, tushafanya research mwaka fulani, kama unataka data zaidi nenda kwa mtu fulani atakupa.

Akisema hiki, anaambiwa hilo tunalijua, tunalifanyia kazi kwenye mradi fulani tangu mwaka gani.

Akaja kugundua kwamba, tatizo la serikali si kwamba haina habari, si kwamba haina watu wenye weledi, serikali ina bluebooks zote, ina watu wana weledi sana.

Tatizo ni politics, political will, watu hawataki change, watu wana maslahi yao ya kibinafsi, kisiasa etc.

Kwa hiyo unaweza kushauri mambo mazuri kibao, watu wana makabrasha yote.

WaNigeria walikuja hapa kujifunza jinsi ya kuhamisha mji mkuu, kutoka Lagos kwenda Abuja.

Wakijua kwamba tulifanya kazi hiyo kutoa mji Dar kwenda Dodoma.

Wakachukua makabrasha waende kusomea.

Wenzetu wanafunzi wetu wamemaliza zoezi miaka kibao, watoto wanazaliwa hata hawajui Lagos ulikuwa mji mkuu.

Sisi walimu tumebaki namakabrasha yetu.

Sasa unapoona mtu anaandika mengi sana kwa assumption kwamba "wakijua haya tu, watabadilika", unaona anafikiri hawajui, tatizo ni kujua tu.

Kumbe tatizo kuna wheels huko za siasa na ukiritimba kibao.
 
Kwamba hawa watu viongozi serikalini wana nia nzuri, lakini hawajui hili nalile tu, wakijua, watabadilisha mambo wafanye vizuri.

Serikali ina watu wanajua mambo kuliko watu wengi wanavyoelewa, ina mahabari kibao ambayo watu hawana.

Watu wanaposhindwa kufanya vitu, mara nyingi ni uchaguzi wao tu, si kwamba hawana habari.

Kuna rafiki yangu mmoja,jamaa yuko nzuri, familia bora, kasoma mpaka Harvard, halafu kabalance maisha yake vizuri sana, usomi anao, utotowa mjini anao, halafu mtu mmoja down toearth sana mtu wa kujichanganya mtaani, alikuwa anafanya kazi mpaka na watoto wa mitaani.

Akawa bonge la advocate mambo ya elimu, kafanya ma research kibao,akawa bonge la activist.

Akawa anaona serikali haijui mambo, akipata nafasi ya kukaa na wakubwa tu, atawashauri vizuri, watabadili mambo.

Basi, alivyowell connected, Kikwete akamuona, akampaappointment, akawa mshauri wa rasi mabo ya elimu au something like that. ile ana direct access na mkulu mwenyewe JK.

Ndipo hapo alipogundua, kila anachosema,anaambiw ahicho tunakijua, tushafanya research mwaka fulani, kamaunataka data zaidi nenda kwa mtu fulani atakupa.

Akisema hiki, anaambiwa hilo tunalijua, tunalifanyia kazi kwenye mradi fulani tangu mwaka gani.

Akaja kugundua kwamba, tatizo la serikali si kwamba haina habari, sikwamba haina watu wenye weledi, serikali ina bluebooks zote, ina watu wana weledi sana.

Tatizo nipolitics, political will,watu hawataki change, watu wana maslahi yao ya kibinafsi, kisiasa etc.

Hapa inaonesha siasa ndiyo inaharibu mambo. Ndiyo maana mwalimu alisema siasa safi inanafasi ktk kuendeleza nchi.
 
Kwanza kabisa nakupongeza kwa majukumu mazito ya kuwa sehemu ya Uongozi wa taasisi ambayo kwa sasa wewe ndiyo mtendaji mkuu.

Nataka kuamini unashaurika kupitia wanaokufahamu, pia hata na watu usiowafahamu maadamu msingi wa ushauri wao umelenga kwenye uzalendo na ujenzi wa taifa letu Tanzania.

Bila shaka kunaweza kuwa na namna nyingi za kukufkishia ujumbe, na bila shaka kuna nyakati ujumbe unaweza usikufikie. Na kuna uwezekano ujumbe ukikufikia, huenda ukawa umechujwa na “context” ya mtuma ujumbe isifikishwe sawia ili kutimiza malengo ya mtuma ujumbe.

Msingi wa kuandika hapa kwako na wasaidizi wako, ni kwa lengo la kuwafanya mtambue na kuwa kila Mtanzania ana uwezo wa kuwa sehemu ya mafanikio ya kuifikia nchi ya “maziwa na asali”. Bill Hybels mmoja wa walimu nguli wa Uongozi anasema, “Everyone has influence. You have influence” Pia Dr. Myles Monroe mara kadhaa amewahi kusema, makaburini ndiko kuna utajiri ambao haukuwahi kutumika. Mimi nataka kuamini, wewe kwa nafasi yako unaweza ku-harness utajiri katika akili za Watanzania ambao bila shaka haujatumika au uko-underutilized.

Nimesikia kutoka vyanzo vinavyoaminika ya kuwa wewe pia ni Mchungaji, na bila shaka biblia ni moja ya kitabu ambayo unakisoma. Kwa muktadha huo, naomba kukufikirisha hadithi kadhaa kutoka katika biblia.

Naomba nikukumbushe hadithi tatu kutoka katika biblia na baada ya hapo ntakurejesha kwenye hoja.

Yusufu mwana wa Yakobo alikuwa mfungwa gerezani. Japo alifungwa kwa kusingiziwa, tunakumbuka, ni “mfungwa huyu” alikuja na suluhisho la kiuchumi kwa Misri ambalo lilikuwa Taifa kubwa kiuchumi na kijeshi nyakati hizo.

Njaa ilikuwa ni kitu halisi kule Misri, na tafsiri ya ndoto hali kadhalika ilikuwa tafsiri halisi. Kuwa kufanya detailed analysis; miaka 7 ilikuwa muhimu kweli kukusanya chakula cha ziada, kujenga maghala ya kuhifadhi chakula, kuweka mifumo ya kudhibiti wadudu wasiharibu chakula. Kuwa na magari yak u-support logistics, kuweka ulinzi ili chakula kisiibwe. Kuwa na mifumo ya kudhibiti moto usitokee ili hifadhi ya chakula isipotee. Bila shaka kukusanya zaida kwa ajili ya ongezeko la watoto Misri na mataifa jirani na Misri ambayo kama yakipata njaa yanaweza kwenda kununua chakula.

Hadithi ya pili ni ya Daudi mwana wa Yese ambae alikuwa mchunga mifugo. Wakati nabii Samuel anafanya mchakato wa kutafuta kiongozi kuchukua nafasi ya Mfalme Sauli, baba yake mzazi hakuona “potential” kama mwanae Daud kama anafaa kuwa kiongozi. Baba alidhania kaka zake ndiyo kumbe hawakuwa watu sahihi kwa kazi ya kuongoza taifa.

Miaka kadhaa baada ya kupakwa mafuta, Daudi amekwenda kwenye “battle ground” kupeleka chakula kwa maelekezo ya baba yake. Alipofika bonde la Soko, kaka yake na Daudi aitwae Eliab alimwona Daudi kwa jicho la mtu mvivu alietoroka mifugo ya mzee Yese kwa lengo la kujionea/kushuhudia “sinema ya bure” ya mpambano kati ya Israeli na Wafilisti.

Wengi tunakumbuka Daudi alimuua Goliath kwa kombeo baada ya watu wengine kupeleka ujumbe kwa Mfalme Sauli kuwa kuna kijana mwenye ujasiri na ari ya kumpiga na kumuua Goliath kama atapata ridhaa ya Amri Jeshi Mkuu. Inafahamika Daudi hakuwa military trained na hakuwa enlisted jeshini kama Eliab (kaka wa Daudi)

Hao waliokuwa na uzoefu wa kijeshi na vita kwa muda mrefu ikiwemo Sauli ambae alikuwa Amri jeshi mkuu, wote walikuwa waoga maana hawakuwa na option (weather ni strategy, methodology au tactic) yoyote ya kumkabili Goliath ambae alikuwa tishio la Usalama wa Taifa la Israel, tishio kwa Ufalme wote na bila shaka tishio kwa kizazi cha Israel baada ya vita. Tishio kubwa halikuwa uwezekano wa kuuwawa kwa atakaejitokeza kumkabili Goliath, bila shaka tishio lilikuwa utumwa ambao Taifa la Israel lingeupata baada ya yeyote ambae angemkabili Goliath kuuwawa na Jenerali huyu nguli na mzoefu wa vita.

Hadithi ya mwisho inamuhusu Jenerali wa Jeshi la Syria kwa jina la Naaman. Naaman alipata habari (taarifa) kutoka kwa mkewe kuwa katika nchi ya Israel, kuna nabii yuko Samaria anaweza kumponya ukoma. Actually, aliemjuza mke wa Naaman, ni “house girl” aliekuwa katika nyumba ya Naaman.

Jenerali Naaman, aliamini na kuchukua hatua ya kwenda kwa nabii Elisha. Alipopata taarifa kupitia msaidizi wa Elisha ya kuwa anatakiwa kujichovya/kujitumbukiza mara saba katika mto Jordan, Naaman alivunjika moyo na hakutaka kufanya hivyo. Ndipo wasaidizi wake wakamsihi kwa nia njema bosi wao, kuwa, what’s a big deal. Kama angeambiwa jambo kubwa si angefanya. Jenerali Naaman baada ya kukubaliana na ushauri wa “aides” wake, alijichovya mara saba na ukoma ukatakasika.

Ushawishi wa kwanza ulitoka kwa “house girl” kwenda kwa mke wa Jenerali Naaman. Ushawishi wa pili ulitoka kwa “Mrs Naaman” kwenda kwa Jenerali Naaman. Hata Jenerali Naaman alipopata maelekezo ambayo hakuyapenda; aides wake waliokoa jahazi kwa kumshawishi bosi wao. Jenerali Naaman, alipo-buy in, alitakasika.

Naomba kumshauri Director Kipilimba kama layman katika mambo machache ya kukuza uchumi wa Tanzania kimkakati, hususan katika miaka hii ya Mhe. JPM ambae amejipambaua kuwafanya Watanzania kuwa “middle class” wa kati kwa kutumia viwanda kama nguzo ya kusisimua/kukuza uchumi.

Ikumbukwe, Daudi wala hakuwa enlisted jeshini, yet mkakati wake wa kumuua Goliath alileta matokeo.

Yusuf pamoja na kukaa kwa Captain Potifa kama mkuu wa wafanyakazi, hakuwahi kushika wadhifa na majukumu ya uongozi mkubwa katika Taifa la Misri. Yusuf alitoa tafsiri ya ndoto, ila mkakati wa hifadhi ya chakula kwa miaka 7 ulikuwa ni matokeao ya creativity, strategic planning na juhudi za Farao aliekuwa mtawala wa Misri kuona umuhumu wa kumjumuisha “mtu wa kuja” kwa kuwa alikuwa na akili ya kutatua matatizo ambayo insiders katika serikali ya Farao walishindwa kuja na majibu ya tafsiri ya ndoto na mkakati wa muda mrefu ya Taifa la Misr kuhifadhi chakula wakati wa neema ya chakula cha ziaada.

Hata yule house girl wa kwa Jenerali Naaman, japo alikuwa utumwani, yet alikuwa na ushawishi wa nia njema kwa bosi wake aweze kupona. Nami niko hapa kama mzalendo kwa nia njema kushauri.

Nadhani sote tutakubaliana pia, ajali ya MV. Nyerere, kisiwani Ukara majuma machache yaliyopita, wavuvi wa ukara (laymen), waliweza kuchukua jukumu la kwanza kuokoa waliokuwa hai na kuwaokoa miili ya watu waliopoteza maisha kabla ya vikosi ya uokoaji kutoka majeshi yetu havijafika visiwani Ukara. Hivyo, kwa lugha yangu ya “U-layman”, bila shaka kuna jambo Director Kipilimba na wasaidizi wako mtaokota.

Toka 1997 wakati dira ya Taifa inazinduliwa na toka JPM atangaze namna ya kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda, sisi kama Taifa je kuna mkakati wa pamoja wa kiuchumi (strategic economic inclusion)?

Je tuna model ya kiuchumi/model za kiuchumi ili kutimiza malengo ya kupata output kubwa katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda?

Moja ya chanzo nilichosoma kutoka maandiko mbalimbali ya model ya kiintelijensia ya kukuza uchumi inasema… If intelligence is the capability of understanding and interacting with the environment in order to act to obtain competitive advantages.

Kuna maeneo kadhaa sisi Tanania tuna “competitive advantage”. Competitive advantage inaweza kuwa realized kwa haraka kama yafuatayo yatafanyiwa kazi

  • To define the strategy, including approach and the task of each countrymen through diverse organizations they are in;
  • To have the capability for abstract reasoning and understanding of the multiple interactions existing in complex environments, including a capability of judgment and knowledge development.
  • To have the capability to detect substitute products or disruptive technology and to understand cultural or demographic changes.
  • To develop the capability to be ahead of changes in regulatory or economic conditions of market dealers in order to launch offensive or defensive actions.
Intelligence must be firstly strategic and then economic. Then, it will be competitive or solely reduced to the analysis previous to knowledge acquisition through the appropriate techniques and technologies.

Ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa pamoja ambao nataka kuamini kuna outsiders ambao wanaweza kuwasaidia akina Dr. Mpango (Waziri wa Fedha) Waziri VIwanda Mwijage na Waziri wa Kilimo Tizeba, Waziri wa Mifugo Mpina na Waziri wa Ajira Mhagama na Director wa TIC Godfrey Mwambe.

Akina Mark Zuckeberg wa Facebook, Jeff Bezos wa Amazon, Jack Ma wa Alibaba ni “outsiders” katika elimu ya biashara na uchumi. Ila uwezo wa kuwa “creative and Innovative” walianza mdogo mdogo, eventually leo hii wamekuwa sehemu ya kukuza uchumi wa nchi zao.

Director Kipilimba, you can adopt a system of human intelligence that obtains information through persons through economic intelligence, business intelligence and competitive intelligence to ensure Tanzania is thriving economically by use of technology and know-how. Part can be locally harnessed and part can be outsourced.

In your course of governing the entity of which you’re entrusted with God and second, you’re entrusted with the President, you can quickly get results by accepting counsels and adopting the economic models to eliminate poverty and unemployment in this country.

If it happened the outsiders like David, Joseph, the house-girl the list goes on made a difference, you can experience the same by opening-avenue for such people. Some are not far away from the battle ground, you just need to head-pick them; some are “imprisoned through false accusation”

Policies and procedure are man made to ensure desired goals are realized. Decisions made on bad policies and standard operating procedures can delay on hinder true patriots who can make a remarkable economic change in motherland Tanzania.

As you stand in position to analyze a lot of human intel from various sectors/dept. under you. There is a potential of relying to a challenge which face Moses which he was receiving a feedback report from spies who visited the “Promise land”. Up-to this moment some people in junior, middle or senior positions who are serving the current regime are coward like the 10 spies. Either they have bad perception or non believers on how we can arrive into middle income earning country.

Sir, you have a real challenge to listen to a few who are bold like Joshua and Caleb. Very fortunate the boss you serve who is Commander in Chief is a true visionary, very bold, courageous leader who is decisive with audacity to see we Tanzania are navigating towards the promise land.

Mungu Ibariki Tanzania.
Una maono lakini ukweli in kuwa watawala wako bize kulinda madaraka yasiwaponyoke. Sidhani kama house ushauri ni wa watawala wa kizazi hiki!
 
Hapa inaonesha siasa ndiyo inaharibu mambo. Ndiyo maana mwalimu alisema siasa safi inanafasi ktk kuendeleza nchi.

Lo, hapa nadhani pana kitu kipya cha kujifunza.

"----------siasa ndio inaharibu mambo."
Ninaukumbuka sana msemo huo wa Mwalimu , wa "Ili tuendelee tunahitaji--------", ikiwemo siasa bora.

Lakini sikuwahi kudhani kwamba kushindwa kutimiza wajibu kwa mtu yeyote, iwe ofisini, shambani, n.k., vyote vitahusishwa na kukosa siasa bora. Ninaelewa vizuri jinsi mtu anavyoweza kuitanua dhana hiyo ya siasa bora kuwa ndani ya kila jambo zuri au baya. Kinachonishinda kujua ni huo uhusika wa moja kwa moja kwa siasa.

Usafiri wa mabasi yaendayo mbio ukizorota, ni sababu ya Siasa? Boti likimwaga watu majini, siasa itahusishwa?

Nikifikia hapo, uelewa wangu wa mahitaji ya siasa bora katika maendeleo unagota.

Kwa hiyo basi, ngoja nisubiri kisomo hapa ninufaike.
 
Mwl. Nyerere alisema, ili tuendelee twahitaji
1) watu 2) Siasa safi na 3) Uongozi bora
Kuwa na watu wa hovyo au wabovu bila kujali wana uzoefu wa kiasi gani au wasomi kiasi gani... tuna potential kubwa kuingizwa chaka.

Siasa safi yenye nia ya kuwatumikia watu wengi kwa kuwajengea uwezo wawe sehemu ya ujenzi wa Taifa ni muhimu sana. Nchi nyingi za Africa it take no time watu wanaingia katika nafasi za siasa hawana "kitu", over a sudden they become extremely wealth. Je, utajiri wao unatokana na fedha ya halali kwa mapato ya mishahara na posho?

Kuwa na right leaders in place, Siasa ikiwa safi ikifuatia, uwezekano wa kutekeleza dhana ya Uongozi bora huja bila viongozi katika senior post, middle management post au junior post kusukumwa kutekeleza majukumu yao au kuogopa wa kutumbuliwa.
 
Ipitie comment #101 ndugu
 
Kwamba hawa watu viongozi serikalini wana nia nzuri, lakini hawajui hili nalile tu, wakijua, watabadilisha mambo wafanye vizuri.

Serikali ina watu wanajua mambo kuliko watu wengi wanavyoelewa, ina mahabari kibao ambayo watu hawana.

Watu wanaposhindwa kufanya vitu, mara nyingi ni uchaguzi wao tu, si kwamba hawana habari.

Kuna rafiki yangu mmoja,jamaa yuko nzuri, familia bora, kasoma mpaka Harvard, halafu kabalance maisha yake vizuri sana, usomi anao, utotowa mjini anao, halafu mtu mmoja down toearth sana mtu wa kujichanganya mtaani, alikuwa anafanya kazi mpaka na watoto wa mitaani.

Akawa bonge la advocate mambo ya elimu, kafanya ma research kibao,akawa bonge la activist.

Akawa anaona serikali haijui mambo, akipata nafasi ya kukaa na wakubwa tu, atawashauri vizuri, watabadili mambo.

Basi, alivyowell connected, Kikwete akamuona, akampaappointment, akawa mshauri wa rasi mabo ya elimu au something like that. ile ana direct access na mkulu mwenyewe JK.

Ndipo hapo alipogundua, kila anachosema,anaambiw ahicho tunakijua, tushafanya research mwaka fulani, kamaunataka data zaidi nenda kwa mtu fulani atakupa.

Akisema hiki, anaambiwa hilo tunalijua, tunalifanyia kazi kwenye mradi fulani tangu mwaka gani.

Akaja kugundua kwamba, tatizo la serikali si kwamba haina habari, sikwamba haina watu wenye weledi, serikali ina bluebooks zote, ina watu wana weledi sana.

Tatizo nipolitics, political will,watu hawataki change, watu wana maslahi yao ya kibinafsi, kisiasa etc.

Kwa hiyo unaweza kushauri mambo mazuri kibao, watu wana makabrasha yote.

WaNigeria walikuja hapa kujifunza jinsi ya kuhamisha mji mkuu, kutoka Lagos kwenda Abuja.

Wakijua kwamba tulifanya kazi hiyo kutoa mji Dar kwenda Dodoma.

Wakachukua makabrasha waende kusomea.

Wenzetu wanafunzi wetu wamemaliza zoezi miaka kibao, watoto wanazaliwa hata hawajui Lagos ulikuwa mji mkuu.

Sisi walimu tumebaki namakabrasha yetu.

Sasa unapoona mtu anaandika mengi sana kwa assumption kwamba "wakijua haya tu, watabadilika", unaona anafikiri hawajui, tatizo ni kujua tu.

Kumbe tatizo kuna wheels huko za siasa na ukiritimba kibao.
Boss...
Myahudi anaitwa Mooly Eden anasema from the age of
zero we are educated to challenge the obvious, ask questions, debate everything, innovate,”

Utamaduni huo umewafanya kwa pamoja kukua kama nchi na kuyabadili mambo kwa haraka ili kupata matokeo yanaowafaidisha wengi.
Kuyaacha mambo yawe kama yalivyo (business as usual) hatutapiga hatua jamani.

It is high time to take initiative and challenge one another with a positive spirit of pushing the bound for a true transformation.
 
Kuwa na watu wa hovyo au wabovu bila kujali wana uzoefu wa kiasi gani au wasomi kiasi gani... tuna potential kubwa kuingizwa chaka.
Bandiko nililo-'quote' halikuyataja hayo unayoyazungumzia hapa, ambayo sote tunayaelewa. Nililenga nipate elimu pana kutokana na aliyeweka bandiko hilo na mwenzie waliyekuwa wnajibishana na kukubaliana kuhusu uhusika wa 'Siasa safi.'
Hata hivyo nashukuru kwa majibu yako ingawaje hayakukidhi kiu yangu ya kupata elimu.
 
Bandiko zuri saana, economic intelligence miaka ya leo ndio hufanya taifa lipige hatua kiuchumi , bila uchumi ulio bora hakuna maisha yenye tija kwetu, kama nchi tunapaswa kuwa na model za kiuchumi zitakazo tufikisha eneo fulani katika hivi vizazi vyetu
 
Boss...
Myahudi anaitwa Mooly Eden anasema from the age of
zero we are educated to challenge the obvious, ask questions, debate everything, innovate,”

Utamaduni huo umewafanya kwa pamoja kukua kama nchi na kuyabadili mambo kwa haraka ili kupata matokeo yanaowafaidisha wengi.
Kuyaacha mambo yawe kama yalivyo (business as usual) hatutapiga hatua jamani.

It is high time to take initiative and challenge one another with a positive spirit of pushing the bound for a true transformation.
Ningeelewa kama ana challenge angekuja hapa kuanika mapungufu ya idara.

Sasa barua ya wazi ya idara akiomba kwa utiifu kifanyike hiki na kile, wakati tunaoijua idara tunajua watu wanajua yote hayo anayoomba,tena kwa kupitia JF si kwa kupitia idara, hapo sijaona challenge.

Hapo nimeona complacency.

Nimesema tatizo si kwamba hawa viongozi hawajui hizi habari, wanajua hizi na nyingine zaidi za muelekeo huu, kushinda hizi.

Tatizo hawana political will.Kuna politics zinaendesha mambo. Kuna ukiritimba.

Sasa sehemu yenye matatizo hayo, unai challenge vipi kw akuandika barua ya wazi JF?

Hiyo ndiyo challenge kweli?

Juzi nimeona barua ya Malisa, one of our whipersnapper Young Turk lawyers.

Analaumu sana ma DC na ma RC wanavyotumia madaraka kinyume cha spirit na letter of the law kufunga funga watu ovyo.

Malisa ni lawyer, hata mimi nisiye lawyer ila nina interest tu ya kusoma najua kwamba kwenye sheria inayompa nguvu DC kufunga watu, kuna very specific justification inatakiwa zifikiwe.

Halafu mara baada ya hiyo sheria tu, kuna sheria nyingine ya adhabu kwa DC atakayetumia mamalaka vibaya.

Malisa analalama tu, hajafungua kesi hata moja dhidi ya DC kuweka record clear watu tupate kuona sheria inavyochukua mkonodo wake na ma DC wapate kujua hawana Draconian hand with impunity.

Tumekuwa watu wa utamaduni wa kulalamika sana, ukiuliza kipi kinafanyika kubadili mamabo, hakuna kitu.

Ndiyo maana Kikwete aikuwa akiona maneno yanavuma sana, alikuwa anasema "ni upepo tu, utapita".

Anajua wabongo wanachonga sana, lakini vitendo hakuna.

Nimeuliza kama hii barua Kipilimba kapelekewa, mpaka sasa sijaona jibu.
 
Bandiko zuri saana, economic intelligence miaka ya leo ndio hufanya taifa lipige hatua kiuchumi , bila uchumi ulio bora hakuna maisha yenye tija kwetu, kama nchi tunapaswa kuwa na model za kiuchumi zitakazo tufikisha eneo fulani katika hivi vizazi vyetu
Unafikiri hao watu wa Usalama wa level ya Kipilimba hawajui hayo mambo basic hivyo?
 
Unafikiri hao watu wa Usalama wa level ya Kipilimba hawajui hayo mambo basic hivyo?
Mkuu natambua ni basic ndiyo, swali linakuja kama wanatambua hivi vitu ni basic je wanavifanyia kazi ( sijui kama wanafanyia kazi) , je hata walio pita walifanyia kazi ? Matokeo yapo wapi ? , au wameanza kuyafanyia kazi leo?
 
Nimeandika hapo juu kwamba, wanatambua, tatizo hakuna political commitment, kuna ukiritimba wa kisiasa, uzembe etc, mambo hayafanyiwi kazi.

Ssa mtu anayejua yote anayotakiwa kufanya, tena kukushinda wewe wa nje, halafu hafanyi.

Halafu wewe unamuandikia barua ya wazi, hatujui hata kama imemfikia, unategemea mabadiliko vipi?

Haya, tufanye imemfikia, mtu anajua zaidi ya uliyoandika, kama wewe umeandika 20, yeye anajua 200.

Huyu tatizo lake si kujua, kuna mengine mengi tu.

Ssa asipoyafanyia kazi, kwa sababu aliyajua hata kabla hujaandika, utashangaa nini?

Na asipoyafanyia kazi utafanya kipi zaidi?

Halafu mtu mwenyewe aliyeandika kaandika kwa a very hyperbolic style, anamsifia mpaka Jiwe, wakati Jiwe ndiye tatizo la kwanza kabisa.
 
Wakuu neno "economic. Intelligence " limetajwa sana kwenye huu uzi..lakini kwa Tanzania hii sio issue hawa viongozi wanajua na wasomi wanajua. Tatizo la Tanzania ni siasa zetu. Sio nzuri hasa za chama cha mapinduziiii...

Kinachotakiwa watu ni kujitoa muhanga kwa msalahi ya walio wengi bila ya hivyo mambo yatabaki blablaa sijui uchumi wa kati....inchi ya viwanda nk.

Hiki ni kipindi pekee ambacho kina massive movement ya Dr. And Prof. Kwenye siasa

Mtoa mada nimekusoma lakini pale mwishoni umetumia kingereza kigumu sijakuelewa
 
Tatizo miaka nenda rudi tabaka la wanasiasa lilijijenga sana Tanzania na kuathiri system za nchi kuweza kufanya mambo yake kwa weledi usiochakachuliwa na milengo ya kisiasa. Ndo maana hadi leo utasikia movie za kuhama vyama na kuitisha chaguzi za marudio.
 
Freddie Matuja asante kwa bandiko, ingawa bandiko limekuwa refu unnecessarily, umerudia rudia kiasi ambacho mpaka mtu aifikie point ni issue.

Hata hivyo, kama anavyosema Kiranga, hakuna wasichokijua viongozi wetu, write-ups zimejaa library.

Siku ukibahatika kupata Document ya Mkukuta na Mkurabita unaweza kushangaa, kuna nondo zimeandikwa humo si mchezo, njoo Kilimo Kwanza, Njoo BRN, ni mipango ya kufa mtu, lakini mipango yote inaisha kwenye makaratasi.

Hapo hatujazungumzia Azimio la Arusha, Zanzibar, na mipango mikakati mingine, imejaa madini. Shida ni kwamba hakuna mwenye utayari wa kuamua kufanya actual implementation ya yalioyandikwa, yanaishia kwenye karatasi na akija mtawala mwingine anakuja na sera zake.

Leo hii tunazungumzia Uchumi wa Viwanda:-

- Jiulize mlolongo wa taratibu uliowekwa unapoanzisha biashara, ni kama hawataki watu wafanye biashara

- Kodi zimeongezeka, leo hii wazalishaji wa Cement wako hoi, halafu unazungumzia Uchumi wa Viwanda wakati Viwanda ulivyovikuta unachangia kuviharibia

- Elimu duni, chumba kimoja kinakuwa na watoto 200, hivyo viwanda unavyovizungumzia unataka nani aajiriwe (aviendeshe)?

- Wanasiasa ndo wataalamu wa kila kitu, si ajabu kukuta waziri anamfokea mtu mwenye profession yake kisa tu apate umaarufu, hata kabla ya kuuliza

- Uchumi wa Viwanda, kuna viwanda gani vimefufuliwa na vikawa effective toka hii sera imeanza?
 
Watu wameona umeandika mambo ya msingi sana, ila nimesoma na kuelewa kuwa uliyoyaandika ni ya msingi ila nayaona kama ni sawa na bure tu!!!!

Huwezi kuwa na version ya nchi ya viwanda na maisha ya kipato cha kati kwa mfumo wa elimu tulionao hivi sasa, hata hao majasusi wangefanya nini, elimu iliyopo kwa sasa haina cha ziada cha kuichangamsha jamii kifikira, maaana ina tengeneza taifa la wapiga kura na sio kuchochea wabunifu na wagunduzi ndani yataifa letu!!

Bado tuna watanzania asilimia zaid ya 90 kwa nionavyo mimi ambao uelewa wao wa mambo mbali mbali ya kiuchumi ni mdogo sana sana, watu wetu hata uwezo wa kubuni na kigundua mambo mbalimbali yenye tija kwa uchumi wetu ni zero!!! tuna watu wataaalamu waliosoma notisi za madarasani wakapata kufuaulu mitihani yao kwa kupata division na kuja kuajiliwa!! hawana msaada wowote na taifa hili. yote nikutokana na kusomea jambo fulani ili apate ajira na sio kuendeleza kipaji chake kitu ambacho kingemfanya kuwa mbunifu na mgunduzi wa kitu au jambo ambalo lingeiletea faida nchi!!

Mimi nadhani DIRECTOR angeutendea haki ushauri wako vizuri sana kama angekuwa na taifa la watu wenye elimu sahihi inayoakisi maisha yao na mahitaji halisi ya maisha yao ili uwepo wa viwanda na teknolojia uwepo! na hapo ndio ujasusi wa kiuchumi utafanya kazi kwa asilimia 100. Ila Directa huyu mnampa kazi asiyoiweza kutokana na nature ya sasa ya watanzania wapenda udaku na upuuziii wa maisha ya watu na sio maswala ya msingi ya nchi, yote sababu ya elimu mbovu, Hivyo tutatue kiini cha tatizo letu kwanza!!!! fumueni hii elimu kwanza, hayo mengine baadaye!!!
 
Yani mi Raisi namkubali ila hii idea ya watu kujiuzulu na hakemei inamshushia credibility kabisa na itamfanya record yake huko mbeleni ije kuwa fedheha aisee, sioni huo umuhimu sijui rudia uchaguzi niunge mkono washauri hawampi ukweli hyo kitu imempunguzia heshima yake.
Hafu maendeleo mazuri ni ya watu pia maendeleo ya miundo mbinu. Faida ya miundo mbinu itaonekana like 10 years to come, pia asisahau uchumi sasa sio mzuri walah.

Hao wa marufuku kuvaa suti wamekosa kazi muhimu ya kufanya nchi inachagamoto nyingi kuliko wavaa suti. Huyo RC amejizalilisha au ndo alikua anatafta kiki.
Sasa hivi kuna kikao cha World Bank kinaendelea Bali Indonesia. Wadau wakubwa wanachosisitiza ni ku invest kwenye watu na hasa early education. Wameona jinsi nchi nyingi za Africa zinakazania kujenga viwanda, infrastructure but they do not invest in Education. Ina maana tungewekeza kwenye elimu kama Mw. alivyofanya kwenye late 60s and seventies tungekuwa mbali.
Sasa hivi unajenga reli za kisasa lakini watu wako hawajui kusoma na kuandika hata wale walio madarasani wanasoma hewa. Kweli hapo? Huo uchumi utafikiwaje? Kwa kualika wachina kuja kuujenga? First Education the rest will solve themselves.
 
Back
Top Bottom