Ushauri wa Bure kwa Director Modestus Francis Kipilimba

Ushauri wa Bure kwa Director Modestus Francis Kipilimba

Punguza povu sio lazima anachoongea mwenzio ukubali unaweza pia kupita kimya
Naona una hasira sana nchi yako pendwa ya Rwanda siku hizi toka Kipilimba ameingia mmeshindwa kabisa kunusa unapikwa mchuzi wa mboga gani
Rwanda ilifikia inaua watu south Africa,kwa kiburi kabisa inasema ni maofisa wa Tanzania ndio wameua.
Rwanda waliandika barua ICAO kuomba kulitawala anga la Tanzania
Ni kipilimba aliekataa na kushauri tununue radar nne za kijeshi ,zifungwe Dar,Songwe,Kia na Mwanza kwa dola milioni 60,Mkandarasi wa kifaransa yupo site,Rada ya mwanza tu ina uwezo wa kuona anga lote la Rwanda,ndio mana mapovu na matusi tu yanakutoka

Ulichokiandika hapa na Mada ya Uzi husika vina ' Logical Connection ' gani? Halafu nikikuambia kuwa Wewe ni really ' CERTIFIED IDIOT ' unabisha. Na najua unajifanya umeiva Kijasusi / Kinjagu hivyo umeongelea na kuiweka hapa Rwanda na ' Ututsi ' wangu kama ' mtego ' wako Kwangu usikie nitasemaje na uweze Kuokotozea mawili matatu ili Uandike ripoti vizuri upeleke. Cheza na Watu wote siyo GENTAMYCINE. Halafu kuwa makini sana unapoiongelea Rwanda, Watutsi na Rais Paul Kagame sawa? Familia yako bado inakuhitaji hasa Wanao na ' Mbunye ' ya Mkeo.
 
Nimekuvutia mtaroni umejaa,huu ni uthibitisho tosha kabisa kwa nini unapenda sana kujua jua mambo yasiokuhusu
Sijawahi kumuogopa binadamu mwenzangu,hiyo mikwara yako mbuzi katishaneni huko huko kwenu
 
Tusipojifunza kuwa na uchungu na nchi yetu nakuwekeza kwenye ya msingi step zetu za kimaendeleo zitakuwa very slow. Tusione China anamkaribia USA tukafikiri ni kazi rahisi intelligence yao imewekeza kila corner.

Ukitazama takwimu za vyuo vikuu muhimu vilivyopo State zote za Marekani, na vile vya Uingereza, Ujerumani katika miaka kuanzia mapema 1980 hadi 2000 utagundua ni kiasi gani China walivyojizatiti kutafuta uwezo wa watu wao. Vyuo hivyo vilikuwa na waChina wengi sana utadhani wamevikodisha vyuo hivyo. Waarabu, Irani, Turkey na hata Egypt nao walianza hivyo hivyo. Sadam alikuwa amepania kweli kuibadilisha Iraq, lakini wakamuwahi.

Hapa kwetu Afrika, kama Ethiopia hawatavurugwa na matatizo yao ya kikabila, nchi hiyo ina kila dalili za kutoka vizuri, tena haraka sana. Lakini walikuwa wanafuata mkakati ulioeleweka vizuri. Ni miaka ya hivi karibuni tu GDP ya Ethiopia ilikuwa chini ya ile ya Kenya, na hata sisi tulikuwa juu yao, leo hii wamekwishapaa na kuongeza GDP yao maradufu. Sisi bado tunapapasa tu hata hatujui mlango uko wapi!

Hofu yangu kubwa ni huu utumiaji wa mabavu zaidi katika kufanya mambo badala ya kutumia akili. Hili litaturudisha nyuma sana.

Kikwete alikuwa na mambo ya hovyo sana katika kuachia mali zetu kuchezewa hovyo na kuruhusu rushwa itawale. Lakini uchumi ulianza kukua kwa kasi na kusema kweli kasi ile iliweka matumaini ya GDP yetu kuipiku Kenya katika miaka michache ijayo.
Kilichotakiwa kufanywa na ngwe hii ilikuwa ni kutumia akili (sio mabavu) kurekebisha madudu ya Kikwete na kuuacha uchumi uendelee kuua kwa kasi zaidi.

Sasa tunazima mwanga kila mahali, tunafanya yetu gizani tukidhani kwamba kuteteleka kwa uchumi kunaweza kufichwa kabatini kusionekane!
 
Tanzania ni nchi yetu. Tukisimama kwa pamoja kwa nia njema na kuwa na lengo la kukuza uchumi wetu based on our competive advantage tutafika.

Ila tukiendelea kuzodoana itathibitisha kilichosemwa "And if a kingdom be divided against itself, that kingdom cannot stand "
It is high time to join forces and wage war against our common enemies

Of course unaelewa jukumu la uongozi katika haya uliyoyasema hapa. Haya hayawezi kuwepo kimiujiza tu bila kuwekewa mazingira yanayoruhusu hali hiyo kustawi.

This is the big problem, and you know it, but you chose to nimble around it.
Hili nalo ni tatizo kubwa kwetu waTanzania. Unaona kabisa tatizo liko wapi, halafu unajifanya kufumba macho kana kwamba huoni kitu!
 
Punguza povu sio lazima anachoongea mwenzio ukubali unaweza pia kupita kimya
Naona una hasira sana nchi yako pendwa ya Rwanda siku hizi toka Kipilimba ameingia mmeshindwa kabisa kunusa unapikwa mchuzi wa mboga gani
Rwanda ilifikia inaua watu south Africa,kwa kiburi kabisa inasema ni maofisa wa Tanzania ndio wameua.
Rwanda waliandika barua ICAO kuomba kulitawala anga la Tanzania
Ni kipilimba aliekataa na kushauri tununue radar nne za kijeshi ,zifungwe Dar,Songwe,Kia na Mwanza kwa dola milioni 60,Mkandarasi wa kifaransa yupo site,Rada ya mwanza tu ina uwezo wa kuona anga lote la Rwanda,ndio mana mapovu na matusi tu yanakutoka

Wanangu msigombane huku nje, ingieni mkagombane kule ndani
 
Umenikumbusha Secondary kwenye kuandika Ese unapamba zile point na maelezo mengi ya kujaza hata karatasi 8 halafu mwisho wa siku unapata 6 ya 20.

Sijaelewa ulichoandika.
hiyo 6 ya 20 mwalimu anakuwa bado kampendelea kama huyu mleta mada anakiwa ampe 1 ya 20 ya walau ku attempt swali hilo kumpa 6 ya 20 ni nyingi mno
 
I like ur topic ume elaborate vzuri nchi yetu inahtaji economic intelligence, business intelligence ili tupige hatua .
Bussiness and Economic intelligence ipo na inafanya kazi ndio iliyoondoa uchumi na biashara za kupiga dili zilizokuwepo.Nchi haiwezi kuendelea kwa kuendekeza wapiga deal kwenye bussiness na economy.Tanzania ilishaingia kwenye MAFIA STATE ambako wapiga dili ndio walikuwa wameshika uchumi wa nchi ,biashara,siasa na mashirika ya umma,taasisi za serikali nk.Wengi mnapiga yowe humu sababu mlikuwa sehemu ya PIGA DILI ECONOMY.Kazi ya business and Economic intelligence ni pamoja na kushughulika na magenge ya PIGA DILI economy yaliyoko kwenye Siasa,biashara,taasisisi,vyama vya siasa,serikalini nk ili kuuweka uchumi ukae mahali sawia na sio mikononi mwa makundi ya KIMAFIA ya kupiga dili
 
Uko vizuri sana lakini ungechaguwa lugha ya kuwasilisha hoja zako labda kwa kingereza tupu su kwa kiswahili tupu, hii changanyachanya lugha inaondowa umakini wa bandiko lako.
wana-Lumumba mmeanza ule ujinga wenu wa woga wa kusoma! pambaf!
 
Ila mie sijui huyu kipilimba kwa sasa ni nani na yuko wapi! Si mnajua tena siku hizi 'teuzi na tenguzi' ni kila uchwao.
 
Mleta mada hongera kwa uzalendo wako hongera sana kwa kuleta uzi bila mhemuko wa kisiasa.
Ila natamani ungefunguka zaidi ili ueleweke pengine kwa uliyemuandikia au kwa sisi wanajamvi ambao tunaweza kuongezea ushauri pindi tukielewa unachotaka kukisisitiza.
Update uzi wako kwa kuelezea specific issues za kufanyiwa kazi.
 
Mleta mada umejaza porojo nyingi hueleweki.

Pili ukimwandikia mtu mkubwa andika kifupi na direct kwenye point.

Hili jarida uliloandika hakuna mtu mkubwa anaweza pata muda wa kusoma jarida refu kama hilo.

Ungeandika point zako walau kwa paragraff mbili tu au tatu. Umeandika kama mtu ambaye alikuwa yuko kwenye kuota anaandika kwa kutiririka anachoota zaidi.

Hebu andika kwa kifupi kwa paragrah tatu ambazo kila paragraph isizidi sentensi saba nini ulichokuwa ukimaanisha au kushauri
Mkuu, upo upo sahihi... tatizo watanzania hatujawahu kuwa na utamaduni wa kusoma kwa umakini. Ukisoma kwa makini sana utagundua kuwa mwandishi katoa mifano mireefu ya biblia wakati main point ni moja tu na angeweza kuiandika kwa sentensi siyo zaidi ya kumi na ujumbe ukafika.
 
Kwanza kabisa nakupongeza kwa majukumu mazito ya kuwa sehemu ya Uongozi wa taasisi ambayo kwa sasa wewe ndiyo mtendaji mkuu.

Nataka kuamini unashaurika kupitia wanaokufahamu, pia hata na watu usiowafahamu maadamu msingi wa ushauri wao umelenga kwenye uzalendo na ujenzi wa taifa letu Tanzania.

Bila shaka kunaweza kuwa na namna nyingi za kukufkishia ujumbe, na bila shaka kuna nyakati ujumbe unaweza usikufikie. Na kuna uwezekano ujumbe ukikufikia, huenda ukawa umechujwa na “context” ya mtuma ujumbe isifikishwe sawia ili kutimiza malengo ya mtuma ujumbe.

Msingi wa kuandika hapa kwako na wasaidizi wako, ni kwa lengo la kuwafanya mtambue na kuwa kila Mtanzania ana uwezo wa kuwa sehemu ya mafanikio ya kuifikia nchi ya “maziwa na asali”. Bill Hybels mmoja wa walimu nguli wa Uongozi anasema, “Everyone has influence. You have influence” Pia Dr. Myles Monroe mara kadhaa amewahi kusema, makaburini ndiko kuna utajiri ambao haukuwahi kutumika. Mimi nataka kuamini, wewe kwa nafasi yako unaweza ku-harness utajiri katika akili za Watanzania ambao bila shaka haujatumika au uko-underutilized.

Nimesikia kutoka vyanzo vinavyoaminika ya kuwa wewe pia ni Mchungaji, na bila shaka biblia ni moja ya kitabu ambayo unakisoma. Kwa muktadha huo, naomba kukufikirisha hadithi kadhaa kutoka katika biblia.

Naomba nikukumbushe hadithi tatu kutoka katika biblia na baada ya hapo ntakurejesha kwenye hoja.

Yusufu mwana wa Yakobo alikuwa mfungwa gerezani. Japo alifungwa kwa kusingiziwa, tunakumbuka, ni “mfungwa huyu” alikuja na suluhisho la kiuchumi kwa Misri ambalo lilikuwa Taifa kubwa kiuchumi na kijeshi nyakati hizo.

Njaa ilikuwa ni kitu halisi kule Misri, na tafsiri ya ndoto hali kadhalika ilikuwa tafsiri halisi. Kuwa kufanya detailed analysis; miaka 7 ilikuwa muhimu kweli kukusanya chakula cha ziada, kujenga maghala ya kuhifadhi chakula, kuweka mifumo ya kudhibiti wadudu wasiharibu chakula. Kuwa na magari yak u-support logistics, kuweka ulinzi ili chakula kisiibwe. Kuwa na mifumo ya kudhibiti moto usitokee ili hifadhi ya chakula isipotee. Bila shaka kukusanya zaida kwa ajili ya ongezeko la watoto Misri na mataifa jirani na Misri ambayo kama yakipata njaa yanaweza kwenda kununua chakula.

Hadithi ya pili ni ya Daudi mwana wa Yese ambae alikuwa mchunga mifugo. Wakati nabii Samuel anafanya mchakato wa kutafuta kiongozi kuchukua nafasi ya Mfalme Sauli, baba yake mzazi hakuona “potential” kama mwanae Daud kama anafaa kuwa kiongozi. Baba alidhania kaka zake ndiyo kumbe hawakuwa watu sahihi kwa kazi ya kuongoza taifa.

Miaka kadhaa baada ya kupakwa mafuta, Daudi amekwenda kwenye “battle ground” kupeleka chakula kwa maelekezo ya baba yake. Alipofika bonde la Soko, kaka yake na Daudi aitwae Eliab alimwona Daudi kwa jicho la mtu mvivu alietoroka mifugo ya mzee Yese kwa lengo la kujionea/kushuhudia “sinema ya bure” ya mpambano kati ya Israeli na Wafilisti.

Wengi tunakumbuka Daudi alimuua Goliath kwa kombeo baada ya watu wengine kupeleka ujumbe kwa Mfalme Sauli kuwa kuna kijana mwenye ujasiri na ari ya kumpiga na kumuua Goliath kama atapata ridhaa ya Amri Jeshi Mkuu. Inafahamika Daudi hakuwa military trained na hakuwa enlisted jeshini kama Eliab (kaka wa Daudi)

Hao waliokuwa na uzoefu wa kijeshi na vita kwa muda mrefu ikiwemo Sauli ambae alikuwa Amri jeshi mkuu, wote walikuwa waoga maana hawakuwa na option (weather ni strategy, methodology au tactic) yoyote ya kumkabili Goliath ambae alikuwa tishio la Usalama wa Taifa la Israel, tishio kwa Ufalme wote na bila shaka tishio kwa kizazi cha Israel baada ya vita. Tishio kubwa halikuwa uwezekano wa kuuwawa kwa atakaejitokeza kumkabili Goliath, bila shaka tishio lilikuwa utumwa ambao Taifa la Israel lingeupata baada ya yeyote ambae angemkabili Goliath kuuwawa na Jenerali huyu nguli na mzoefu wa vita.

Hadithi ya mwisho inamuhusu Jenerali wa Jeshi la Syria kwa jina la Naaman. Naaman alipata habari (taarifa) kutoka kwa mkewe kuwa katika nchi ya Israel, kuna nabii yuko Samaria anaweza kumponya ukoma. Actually, aliemjuza mke wa Naaman, ni “house girl” aliekuwa katika nyumba ya Naaman.

Jenerali Naaman, aliamini na kuchukua hatua ya kwenda kwa nabii Elisha. Alipopata taarifa kupitia msaidizi wa Elisha ya kuwa anatakiwa kujichovya/kujitumbukiza mara saba katika mto Jordan, Naaman alivunjika moyo na hakutaka kufanya hivyo. Ndipo wasaidizi wake wakamsihi kwa nia njema bosi wao, kuwa, what’s a big deal. Kama angeambiwa jambo kubwa si angefanya. Jenerali Naaman baada ya kukubaliana na ushauri wa “aides” wake, alijichovya mara saba na ukoma ukatakasika.

Ushawishi wa kwanza ulitoka kwa “house girl” kwenda kwa mke wa Jenerali Naaman. Ushawishi wa pili ulitoka kwa “Mrs Naaman” kwenda kwa Jenerali Naaman. Hata Jenerali Naaman alipopata maelekezo ambayo hakuyapenda; aides wake waliokoa jahazi kwa kumshawishi bosi wao. Jenerali Naaman, alipo-buy in, alitakasika.

Naomba kumshauri Director Kipilimba kama layman katika mambo machache ya kukuza uchumi wa Tanzania kimkakati, hususan katika miaka hii ya Mhe. JPM ambae amejipambaua kuwafanya Watanzania kuwa “middle class” wa kati kwa kutumia viwanda kama nguzo ya kusisimua/kukuza uchumi.

Ikumbukwe, Daudi wala hakuwa enlisted jeshini, yet mkakati wake wa kumuua Goliath alileta matokeo.

Yusuf pamoja na kukaa kwa Captain Potifa kama mkuu wa wafanyakazi, hakuwahi kushika wadhifa na majukumu ya uongozi mkubwa katika Taifa la Misri. Yusuf alitoa tafsiri ya ndoto, ila mkakati wa hifadhi ya chakula kwa miaka 7 ulikuwa ni matokeao ya creativity, strategic planning na juhudi za Farao aliekuwa mtawala wa Misri kuona umuhumu wa kumjumuisha “mtu wa kuja” kwa kuwa alikuwa na akili ya kutatua matatizo ambayo insiders katika serikali ya Farao walishindwa kuja na majibu ya tafsiri ya ndoto na mkakati wa muda mrefu ya Taifa la Misr kuhifadhi chakula wakati wa neema ya chakula cha ziaada.

Hata yule house girl wa kwa Jenerali Naaman, japo alikuwa utumwani, yet alikuwa na ushawishi wa nia njema kwa bosi wake aweze kupona. Nami niko hapa kama mzalendo kwa nia njema kushauri.

Nadhani sote tutakubaliana pia, ajali ya MV. Nyerere, kisiwani Ukara majuma machache yaliyopita, wavuvi wa ukara (laymen), waliweza kuchukua jukumu la kwanza kuokoa waliokuwa hai na kuwaokoa miili ya watu waliopoteza maisha kabla ya vikosi ya uokoaji kutoka majeshi yetu havijafika visiwani Ukara. Hivyo, kwa lugha yangu ya “U-layman”, bila shaka kuna jambo Director Kipilimba na wasaidizi wako mtaokota.

Toka 1997 wakati dira ya Taifa inazinduliwa na toka JPM atangaze namna ya kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda, sisi kama Taifa je kuna mkakati wa pamoja wa kiuchumi (strategic economic inclusion)?

Je tuna model ya kiuchumi/model za kiuchumi ili kutimiza malengo ya kupata output kubwa katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda?

Moja ya chanzo nilichosoma kutoka maandiko mbalimbali ya model ya kiintelijensia ya kukuza uchumi inasema… If intelligence is the capability of understanding and interacting with the environment in order to act to obtain competitive advantages.

Kuna maeneo kadhaa sisi Tanania tuna “competitive advantage”. Competitive advantage inaweza kuwa realized kwa haraka kama yafuatayo yatafanyiwa kazi

  • To define the strategy, including approach and the task of each countrymen through diverse organizations they are in;
  • To have the capability for abstract reasoning and understanding of the multiple interactions existing in complex environments, including a capability of judgment and knowledge development.
  • To have the capability to detect substitute products or disruptive technology and to understand cultural or demographic changes.
  • To develop the capability to be ahead of changes in regulatory or economic conditions of market dealers in order to launch offensive or defensive actions.
Intelligence must be firstly strategic and then economic. Then, it will be competitive or solely reduced to the analysis previous to knowledge acquisition through the appropriate techniques and technologies.

Ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa pamoja ambao nataka kuamini kuna outsiders ambao wanaweza kuwasaidia akina Dr. Mpango (Waziri wa Fedha) Waziri VIwanda Mwijage na Waziri wa Kilimo Tizeba, Waziri wa Mifugo Mpina na Waziri wa Ajira Mhagama na Director wa TIC Godfrey Mwambe.

Akina Mark Zuckeberg wa Facebook, Jeff Bezos wa Amazon, Jack Ma wa Alibaba ni “outsiders” katika elimu ya biashara na uchumi. Ila uwezo wa kuwa “creative and Innovative” walianza mdogo mdogo, eventually leo hii wamekuwa sehemu ya kukuza uchumi wa nchi zao.

Director Kipilimba, you can adopt a system of human intelligence that obtains information through persons through economic intelligence, business intelligence and competitive intelligence to ensure Tanzania is thriving economically by use of technology and know-how. Part can be locally harnessed and part can be outsourced.

In your course of governing the entity of which you’re entrusted with God and second, you’re entrusted with the President, you can quickly get results by accepting counsels and adopting the economic models to eliminate poverty and unemployment in this country.

If it happened the outsiders like David, Joseph, the house-girl the list goes on made a difference, you can experience the same by opening-avenue for such people. Some are not far away from the battle ground, you just need to head-pick them; some are “imprisoned through false accusation”

Policies and procedure are man made to ensure desired goals are realized. Decisions made on bad policies and standard operating procedures can delay on hinder true patriots who can make a remarkable economic change in motherland Tanzania.

As you stand in position to analyze a lot of human intel from various sectors/dept. under you. There is a potential of relying to a challenge which face Moses which he was receiving a feedback report from spies who visited the “Promise land”. Up-to this moment some people in junior, middle or senior positions who are serving the current regime are coward like the 10 spies. Either they have bad perception or non believers on how we can arrive into middle income earning country.

Sir, you have a real challenge to listen to a few who are bold like Joshua and Caleb. Very fortunate the boss you serve who is Commander in Chief is a true visionary, very bold, courageous leader who is decisive with audacity to see we Tanzania are navigating towards the promise land.

Mungu Ibariki Tanzania.[/QUOTEmi nahisi ushauri wako ni mzuri ila una maneno mengi ungeenda straight kwenye ushauri ili kumpa uraisi wa kufanyia kazi maana naamini anamajukumu mengi ya kutufanyia.
 
Ukitazama takwimu za vyuo vikuu muhimu vilivyopo State zote za Marekani, na vile vya Uingereza, Ujerumani katika miaka kuanzia mapema 1980 hadi 2000 utagundua ni kiasi gani China walivyojizatiti kutafuta uwezo wa watu wao. Vyuo hivyo vilikuwa na waChina wengi sana utadhani wamevikodisha vyuo hivyo. Waarabu, Irani, Turkey na hata Egypt nao walianza hivyo hivyo. Sadam alikuwa amepania kweli kuibadilisha Iraq, lakini wakamuwahi.

Hapa kwetu Afrika, kama Ethiopia hawatavurugwa na matatizo yao ya kikabila, nchi hiyo ina kila dalili za kutoka vizuri, tena haraka sana. Lakini walikuwa wanafuata mkakati ulioeleweka vizuri. Ni miaka ya hivi karibuni tu GDP ya Ethiopia ilikuwa chini ya ile ya Kenya, na hata sisi tulikuwa juu yao, leo hii wamekwishapaa na kuongeza GDP yao maradufu. Sisi bado tunapapasa tu hata hatujui mlango uko wapi!

Hofu yangu kubwa ni huu utumiaji wa mabavu zaidi katika kufanya mambo badala ya kutumia akili. Hili litaturudisha nyuma sana.

Kikwete alikuwa na mambo ya hovyo sana katika kuachia mali zetu kuchezewa hovyo na kuruhusu rushwa itawale. Lakini uchumi ulianza kukua kwa kasi na kusema kweli kasi ile iliweka matumaini ya GDP yetu kuipiku Kenya katika miaka michache ijayo.
Kilichotakiwa kufanywa na ngwe hii ilikuwa ni kutumia akili (sio mabavu) kurekebisha madudu ya Kikwete na kuuacha uchumi uendelee kuua kwa kasi zaidi.

Sasa tunazima mwanga kila mahali, tunafanya yetu gizani tukidhani kwamba kuteteleka kwa uchumi kunaweza kufichwa kabatini kusionekane!
Kuliko kupoteza muda tukimlaumu Kimwete hapa, tungejikita kwenye real solutions zitakazomwinua mtanzania awe katika uchumi wa kati.

Mfano niliouona kwa haraka. Tunaweza kuwa na matatizo mengi sana ambayo viongozi wetu inabidi wayafanyie kazi. Natoa mmoja wengine muendelee.

Problem: SGR, ndege, hata Stiglers Gorge tuna-import mpaka vitu vya aibu. (slab za kulaza reli - ina maana hata zege ya hicho kiwango kwetu ni kizungumkuti kuaminika tutengeneza. Ni aibu sana).

Mapendekezo: Projects zetu angalau 75% ya materials zizalishwe hapa nchini na zitoke kwa suppliers (kampuni) za watanzania. Mfano kwenye reli unamwambia mturuki ajenge lakini 75% ya materials zitengenezewe huku huku na aziagize kutoka kampuni za watanzania. Hata chuma kipo hapahapa. Watanzania wafungue hicho kiwanda hata kwa mkopo wa serikali kisha waturuki waingie mkataba na mwenye kiwanda au mwekezaji anayeweza kufanya manufacturing hapa hapa.
 
Ulichokiandika hapa na Mada ya Uzi husika vina ' Logical Connection ' gani? Halafu nikikuambia kuwa Wewe ni really ' CERTIFIED IDIOT ' unabisha. Na najua unajifanya umeiva Kijasusi / Kinjagu hivyo umeongelea na kuiweka hapa Rwanda na ' Ututsi ' wangu kama ' mtego ' wako Kwangu usikie nitasemaje na uweze Kuokotozea mawili matatu ili Uandike ripoti vizuri upeleke. Cheza na Watu wote siyo GENTAMYCINE. Halafu kuwa makini sana unapoiongelea Rwanda, Watutsi na Rais Paul Kagame sawa? Familia yako bado inakuhitaji hasa Wanao na ' Mbunye ' ya Mkeo.
Rubbish
 
Ukitazama takwimu za vyuo vikuu muhimu vilivyopo State zote za Marekani, na vile vya Uingereza, Ujerumani katika miaka kuanzia mapema 1980 hadi 2000 utagundua ni kiasi gani China walivyojizatiti kutafuta uwezo wa watu wao. Vyuo hivyo vilikuwa na waChina wengi sana utadhani wamevikodisha vyuo hivyo. Waarabu, Irani, Turkey na hata Egypt nao walianza hivyo hivyo. Sadam alikuwa amepania kweli kuibadilisha Iraq, lakini wakamuwahi.

Hapa kwetu Afrika, kama Ethiopia hawatavurugwa na matatizo yao ya kikabila, nchi hiyo ina kila dalili za kutoka vizuri, tena haraka sana. Lakini walikuwa wanafuata mkakati ulioeleweka vizuri. Ni miaka ya hivi karibuni tu GDP ya Ethiopia ilikuwa chini ya ile ya Kenya, na hata sisi tulikuwa juu yao, leo hii wamekwishapaa na kuongeza GDP yao maradufu. Sisi bado tunapapasa tu hata hatujui mlango uko wapi!

Hofu yangu kubwa ni huu utumiaji wa mabavu zaidi katika kufanya mambo badala ya kutumia akili. Hili litaturudisha nyuma sana.

Kikwete alikuwa na mambo ya hovyo sana katika kuachia mali zetu kuchezewa hovyo na kuruhusu rushwa itawale. Lakini uchumi ulianza kukua kwa kasi na kusema kweli kasi ile iliweka matumaini ya GDP yetu kuipiku Kenya katika miaka michache ijayo.
Kilichotakiwa kufanywa na ngwe hii ilikuwa ni kutumia akili (sio mabavu) kurekebisha madudu ya Kikwete na kuuacha uchumi uendelee kuua kwa kasi zaidi.

Sasa tunazima mwanga kila mahali, tunafanya yetu gizani tukidhani kwamba kuteteleka kwa uchumi kunaweza kufichwa kabatini kusionekane!
China walipeleka watu wao vyuo vya nje hasa USA kwenda kujifunza hata kuiba technology ya Marekani na njia walizotumia kuwa superpower then wakaenda na kuzitumia hzo njia kulingana na nchi yao ndo mana China aka acha ule ujamaa na kuingia ubepari, ndo maana China sasa anawekeza Africa kupitia intelligence yake kwenye uchumi, maana. Maana dunia ya sasa inategemea umaskini wetu wa Africa kutunyonya.

Na sisi wa Africa tunafikiri China anatupenda na mikopo sijui misaada huko ni kutunyonya milele. Tatizo la nchi yetu siasa inafanya watu hawatuamii akili pia wataalamu kwetu hawaheshimiwi, China, Malaysia Singapore viongozi wao walijenga misingi na sasa wako vzuri sisi umaskini ukiongezeka kwa kutokuwekeza kwa elimu.

Kwa Africa Ethiopia wanakuja vzuri kuanzia miundo mbinu ya kisasa, umeme hata shirika lao la ndege si mchezo ndege zao zinasafiri dunia nzima wakitulia vzuri Ethiopia ni watakuwa wa kuigwa Africa hasa wakiweza kuondoa ukabila na kuanza Ku invest in human development.

Awamu hii tatizo imejikita kwenye siasa za kufatilia Mara upinzani sijui ukosoaji na kubaki kutumia mda kutofikiria njia za uchumi, maana some reactions za utawala zimeleta athari kwa uwekezaji na biashara, though kuna baadhi ya mambo yanaenda vzuri, ila kwa vtu wakifanya kutoa mabavu nakutumia wataalamu tutapiga hatua, Magufuli anapenda nchi ipige hatua hasa ndo kawekeza kwa miundo mbinu faida yake itaonekana even after five years.

Enzi za jakaya uchumi even democracy vilikuwa pamoja pia wawekezaji walikuwa wanakuja wengi, sema tatizo lake alishindwa kudhibiti mianya ya rushwa, rushwa ilikuwa everywhere. Magufuli kabana mianya ya rushwa na upigaji vimepungua sasa aangalie swala la uchumi ndo kilio cha wana nchi wengi.
 
Bussiness and Economic intelligence ipo na inafanya kazi ndio iliyoondoa uchumi na biashara za kupiga dili zilizokuwepo.Nchi haiwezi kuendelea kwa kuendekeza wapiga deal kwenye bussiness na economy.Tanzania ilishaingia kwenye MAFIA STATE ambako wapiga dili ndio walikuwa wameshika uchumi wa nchi ,biashara,siasa na mashirika ya umma,taasisi za serikali nk.Wengi mnapiga yowe humu sababu mlikuwa sehemu ya PIGA DILI ECONOMY.Kazi ya business and Economic intelligence ni pamoja na kushughulika na magenge ya PIGA DILI economy yaliyoko kwenye Siasa,biashara,taasisisi,vyama vya siasa,serikalini nk ili kuuweka uchumi ukae mahali sawia na sio mikononi mwa makundi ya KIMAFIA ya kupiga dili
Hapo business na economic intelligence mbona umechaganya mambo ni kweli uchumi hauwezi endeshwi kwa kupiga deal hyo ni impossible na hatua zinazochukuliwa nzuri. Shida ni kutokutafiti vzuri mianya tunayopigwa kwenye mikataba mfano mambo ya Acacia walisoma weakness zetu wakaja na mkataba matokeo yake madini yetu hatupati faida. Intelligence nzuri ni ile inayoanza kuangalia masilahi ya taifa kuanzia kiuchumi kijamii hata miswada na mikataba ya nchi ili tusipate hasara
 
Kwenye gesi tuu mkuu mwenyewe kashasema hadharani gesi ni ya wazungu.

Ila viongozi wetu hawana akili ya kuitoa kwenye mikono ya wazungu
 
Back
Top Bottom