Ushauri wa biashara ya kava za simu

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
687
1,360
Habari za muda huu wanajamii.....

Kwanza niseme tu kuwa mimi ni mjasiliamali mdogo nafanya kazi ya kuuza kava na vitu vidogo vidogo vya simu.

Kinachonipa tabu ni hii biashara ya makava ya simu yaani unakuta nikinunua mzigo labda wa laki moja( kulingana na mtaji wangu) mengi yanakaa na kupitwa na wakati yanakuwa hayauziki tena na hii ni kwakuwa wateja wanakuwa selective sana.

Unaweza kuta mtu kaja na simu tofauti na mzigo uliochukua au tena kava la simu yake unalo ila anahitaji la langi ingine au aina nyingine matokeo yake kava zinakaa tu na ukisema uongeze mwingine utafidia ndio kabisaa yanazidi kujazana.

Najua kuna ma hustlers kama mm either wanafanya kazi hii au washawai fanya naomba tupeane uzoefu namna nzuri ya kuifanya hii biashara na kupata chochote kitu.

Ahsanteni
 
Mkuu inabidi ujiongeze kidogo mtindo wa biashara yako tafuta simu nzuri ya camera fungua social medias kama insta,fb ,jiji na whatsapp ..ingia kariakoo piga picha kava kali za kila aina especially za iphones post ukipata hela sponsor ads insta…wateja wengi ni wa delivery so hawatosumbua kuja ofisini kwako ila hiyo njia ya kununua ukayaeka itakua ngumu yapo fasta sana kupitwa fashion
 
Ahsante kwa ushauri

Na je nikifungua izo social network inawezekana kupata wateja wa karibu yangu maana sina usafiri kumfikia mteja inaweza kuwa shida kidogo kwa mteja wa mbali
 
Miaka ya nyuma kidogo kuna jamaa yangu alifungua duka akaweka vitu mix yakiwemo macover enzi hizo Samsung ndio imeshika kasi..alinunua mzigo kama wa 3 mill..kilichomtokea hakuamini maana kwa macover aliuza si zaidi ya 10 na mengi yakawa yamepitwa na wakati after 1 year ..so ilikuwa hasara..biashara ya cover it's better ukaangalia simu hot cover zake zinatembea sana na nunua MACHACHE SANA.
 
Biashara ya cover weka mbali na watoto,hiyo ni biashara kichaa cha mbwa nipo kwenye biashara ya vifaa vya simu 7 years now ila kuhusu cover ziliwahi kunikata 10milioni nashuudia mwenyewe kila ukifukuzana na model za simu ndio unazidi kuzika pesa yako cha msingi uza vitu vinavyoweza kuuzika vyote mfano Usb cable,Flash,memory card,charger,Bluetooth speaker,Earphones,iPod,ringlight,modern,powerbank etc kama nguvu inaruhusu unaweza kumix pia accessories za computer kwahiyo inakuwa unafanya phone &computer accessories kwa wakati mmoja na nguvu ikiruhusu unaweza ukaweka na visimu vya batani ku push mzunguko bila kusahau pia saa za bei ya kati,smart watch,coin battery etc
 
Mimi mzigo nimeweka kwenye shelf mpaka nikaona kero nikatoa nikaweka kwenye mabox
 
Miaka ya nyuma kidogo kuna jamaa yangu alifungua duka akaweka vitu mix yakiwemo macover enzi hizo Samsung ndio imeshika kasi..alinunua mzigo kama wa 3 mill..kilichomtokea hakuamini maana kwa macover aliuza si zaidi ya 10 na mengi yakawa yamepitwa na wakati after 1 year ..so ilikuwa hasara..biashara ya cover it's better ukaangalia simu hot cover zake zinatembea sana na nunua MACHACHE SANA.
Ni changamoto sana mkuu hii biashara ni pasua kichwa unakuta mteja anataka kava ya simu flan ninalo ila inakuja tena either rangi au modal iyo hataki anataka la mdori au la yanga na simba
 
Biashara ya cover weka mbali na watoto,hiyo ni biashara kichaa cha mbwa nipo kwenye biashara ya vifaa vya simu 7 years now ila kuhusu cover ziliwahi kunikata 10milioni nashuudia mwenyewe kila ukifukuzana na model za simu ndio unazidi kuzika pesa yako cha msingi uza vitu vinavyoweza kuuzika vyote mfano Usb cable,Flash,memory card,charger,Bluetooth speaker,Earphones,iPod,ringlight,modern,powerbank etc kama nguvu inaruhusu unaweza kumix pia accessories za computer kwahiyo inakuwa unafanya phone &computer accessories kwa wakati mmoja na nguvu ikiruhusu unaweza ukaweka na visimu vya batani ku push mzunguko bila kusahau pia saa za bei ya kati,smart watch,coin battery etc
Ahsante kwa ushauri mkuu
 
Panua soko makava ambayo yanapitwa kimuonekano huwa yanasambazwa sehem za mbali asikudanganye mtu kava iliyo pitwa fashion Dar kule Maswa bado ni sukari
Swala ni kuwa na mtandao tu una mpushia mtu kwa jumla
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom