Ushauri wa biashara ya daladala (Mwanza, Mbeya, Dodoma, Arusha, Tanga, Dar)

Ok mtaji ni 30million
Mkuu Nenda Tata Tanzania wanakupa basi la siti 40, bei cash ni Tsh 105M unalipia 30% ambayo ndo hyo 30M kwa mwezi unapeleka Mrejesho wa 3.8M, Hakikisha unapata route inayokupa sio chini ya laki mbili per day. uzuri hii inaenda hata rough roads tafuta njia ambayo haina magari mengi utapiga hela.
 
Mkuu Nenda Tata Tz wanakupa basi la siti 40, bei cash ni Tsh 105M unalipia 30% ambayo ndo hyo 30M kwa mwezi unapeleka Mrejesho wa 3.8M, Hakikisha unapata route inayokupa sio chini ya laki mbili per day. uzuri hii inaenda hata rough roads tafuta njia ambayo haina magari mengi utapiga hela
Rejesho ni kwa muda gani tupige hesabu...!?

Isijekuwa mwisho wa siku umeuziwa kwa TSh. Mil 200.
 
Salaam wana Jf,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.

Pamekuwa na nyuzi kadhaa na maswali kadha wa kadha kutoka kwa watu ambao wanatamani kuifanya hii biashara, ila hawana uelewa wa kutosha.

Hivyo, ninaomba
Kwa wenye uzoefu wa biashara hii ya daladala
Ningeomba watupe ushauri kwa wanaohitaji kuanza .. na suala zima la changamoto kiujunla.

Bila kusahau, aina/model nzuri za magari ambayo yanafaa zaidi kwenye biashara hii.

Natanguliza shukran kwa mtakao tumia muda wenu kusaidia kutoa ushauri.


Ahsante.
 
Ninahitaji ushauri juu ya biashara ya daladala. Kununua gari mpaka litoke bandarini cost yake na dereva na konda mkataba wao shingapi na kuingiza kwa siku ni shingapi. In short nahitaji kuelewa hii biashara ya daladala
 
Wauzaji magari wataja saidia jibu gharama za uletaji na kila kitu mpaka kutoka bandarini?

Mkuu gari unayotaka kuagiza ni ni aina ipi hiace, coaster, Tata, Hitcher etc na ulikuwa unataka uindeshee biashara yako mkoa upi?

Usije ukalogwa mpa dreva mkataba mpaka uwe umejiridhisha na utendaji wake wa kazi na uwe umemuamini haswa kwamba hutakuja kukubabaisha mbeleni. Kuhusu hesabu ya siku inategemeana na aina ya gari na route pia inayofanya.
 
Wauzaji magari wataja saidia jibu gharama za uletaji na kila kitu mpaka kutoka bandarini?

Mkuu gari unayotaka kuagiza ni ni aina ipi hiace, coaster,Tata,Hitcher etc na ulikuwa unataka uindeshee biashara yako mkoa upi?

Usije ukalogwa mpa dreva mkataba mpaka uwe umejiridhisha na utendaji wake wa kazi na uwe umemuamini haswa kwamba hutakuja kukubabaisha mbeleni. Kuhusu hesabu ya siku inategemeana na aina ya gari na route pia inayofanya.
Mkoa Dar es Salaam na gari ni coaster
 
Mkoa Dar es salaam, na gari ni coaster

Sijui vitu vingi ila naweza kusaidia kwa uchache maana jamaa yangu yuko anafanya vitu hivi.. daladala inayoonekana kudumu ni hizi Nissan civilian kwa Dar es Salaam naona matajiri wengi wanazikimbilia (unaweza agiza au ukanunua kwa mtu )

Unapokuwa na daladala, mambo muhimu hakikisha una sehemu ya uhakika ya kulaza gari yako, kwa nini nasema hivi “hii itakusaidia pale utakapokuwa na daladala then unaweka limitation ya kupark gari kama ni saa au saa 3 gari iwe parking, itasaidia kuitunza gari maana deiwaka zipo sana”

Hakikisha una fundi wako wa daladala unayemuamini au gereji in case ya tatizo la daladala fundi ndio ana verify tatizo then spear inatafutwa... Kwa nini nasema hivi “unaweza pigiwa simu ukaambiwa tumenunua kifaa fulani tukafunga kumbe uongo”

Jitahidi ujue sehemu utakapopata vifaa kwa bei rahisi hii itapunguza cost kwako maana sometimes fundi naye anaweza weka cha juu.

Ni mengi ila hayo kwa uchache.. hesabu ya siku inategemeana na route kuna hesabu 90,000, laki kwa hizi daladala za kawaida.. tena gari ikiwa mpya kazia hesabu

Mpe dereva uhuru wa kufanya kazi.. sikiliza pale kunapotokea matatizo ya kihesabu.. sometimes kuwa mkali usiwe normal yaani

Usitegemee sana daladala kama sehemu ya kipato cha kuendeshea maisha iwe ni ziada katika uwekezaji wako

..zaidi utauliza na wadau watachangia #asante
 
Back
Top Bottom