kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu siasa za Tanzania tangu miaka ya tisini. Baada ya uchaguzi wa mwaka huu,nimeamua kukubali kuwa CCM hakitakaa kiondoke madarakani kwa njia yoyote ile unayoijua wewe duniani kwa sasa, hata kama itafanya vibaya namna gani!
Mipango yote, mikakati yote ya kukiondoa chama hiki haiwezi kufanikiwa kwa kuwa ukweli unaonekana dhahiri kuwa kimewekeza sana katika kuhakikisha kinakuwa salama baada ya uchaguzi hata kama ni kwa gharama ya maisha ya watu wake.
Mikakati wanayoifanya CCM ni pamoja na kuhakikisha wanatumia inteligensia ya taifa,kuhakikisha kuwa hakuna chama kinachoweza kukua na kuwa tishio kwa ccm halafu kikabaki salama. Kwa watu wengine tulijua mapema jinsi cdm ilivyouwawa hata kabla ya kuingia katika uchaguzi huu. Naweza kusema hivi chadema ilivyo ni kwa sababu ya ubishi na uhodari wa Mbowe. Naamini wasingefika hata hapo walipo bila uthabiti wa viongozi wa juu akiwemo pia dr Slaa.
Kwa hali ilivyo, ninajaribu kuviona vyama vya upinzani kama vile vinatumika kuweka uhalali wa kuendelea kutawala kwa ccm mbele ya jamii ya kimataifa. Baadhi ya vyama vinavyoonekana kuanza kuwa tishio hukabiliana na misuko suko mikubwa na hata kwa baadhi ya wanachama wake kupoteza maisha kwa vile tu wao ni wapinzani.
Sasa nadhani umefika wakati ili kuepusha watu wasio na hatia kuumia kwa vile tu ni wapinzani,vyama hivi vifutwe na kibaki chama kimoja kama zamani. Hakuna sababu ya ccm kutumia nguvu kubwa na rasilimali za taifa kwa kuandaa uchaguzi ambao wao wanajua wanataka kushinda kwa namna yoyote ile.
Nawaomba watanzania waniunge mkono katika hili, wale wabunge waliochaguliwa kupitia upinzani, mniunge mkono kwani mnaweza kugombea tena kupitia CCM pia. Sioni tumaini tena katika mfumo huu wa vyama vingi. Ni bora kuwe na mfumo wa mgombea binafsi au hata CCM wachaguane wenyewe kama wanavyopenda ili mradi watu wasiumie kwa sababu ya uadui wa kisiasa.