Kaka msingi wa CCM ulisimikwa na mfumo wa katiba iliyopo. ni ngumu sana kuitoa CCM madarakani kwa mfumo wa katiba iliyopo. Ndiyo maana mfumo wa rasimu ya pili ya Warioba ulikuwa ni hatari sana kwa CCM kuendelea kubaki madarakani, ndiyo maana waliikataa.
Mimi nakuunga mkono kabisa, haina maana vyama vya upinzani kupoteza rasilimali zao wakati Rais ameshawekwa kabla hata ya uchaguzi.
upinzani wetu hauna watu makini unaongozwa na wasela,upinzani umericruit vijana wahuni ambao wanaondoa mvuto wa chama.tumeona wakati wa kampeni mambo ya kihuni.tazama vijana na washabiki waccm unajua wazi ni watu wa mikakati.vilevile kudandia watu waliotupwa na vyama vyao na kuwawafanya lulu.viongozi huandaliwa sio kuokotaokota.
Watanzania wanaakili sana tizama kuna sehemu wamechagua diwani mpinzani lakini urais wamepigia ccm.
Ccm inachaguliwa kwa kuwa hadi sasa ndio chama bora kuliko vingine.mtu na akili zako huwezi sema hata likiweka jiwe utalichagua kuliko ccm.huko ni kuvia ubongo na matokeo yake tunayaona.
Kinachotakiwa ni kujenga vyama bora kuliko ccm.na kuachana na viongozi ndumila kuwili.