Ushauri unaponunua vitu kutoka China ( Alibaba)

Nov 26, 2018
14
38
Habari Watanzania, Heri ya miaka 58 ya uhuru!
Bila kupoteza muda ngoja tuongee namna ya kununua vitu kutoka nchini China hasa kupitia platform ya Alibaba ( Made in China)
Kwanza Kabisa Alibaba sio platform peke yake ya kuweza kununua vitu nchini China kuna platforms kama Global sources, Made-in-China, Banggood na kadhalika,

Najaribu kufikiria unafahamu kuingia kwenye mtandao wa alibaba na unaweza kutafuta bidhaa. Sasa nataka kukuonesha namna ya kuwa mbele ya wauzaji wa kichina kwenye platform ya alibaba na vitu vya kufanya kuepuka kupoteza muda na kuumia kichwa mbeleni.

1. Bidhaa ( Product)

Hakikisha muuzaji wa kichina ( supplier ) anafahamu nini kabisa unataka kununua hapa inamaanisha ( products specifications). Hakikisha unaeleza vizuri kwa ufanisi na kiundani unataka nini hasa kwenye bidhaa yako. Ushauri Chukua dakika 10-15 kuandaa maelezo ya bidhaa, vitu kama
-Size ( Ukubwa)
-Material ( Materio)
- Grade ( kiwango cha ubora)
- Application ( In use)
- Packaging (uhifadhi wake)
- Quantity ( Uwingi)
- Shipping Terms ( namna ya usafiri)
- Target Price ( Bei uliyopanga) HII NI MUHIMU SANA


2. Fanya Kuhakiki ( Evaluation )

Mara zote unapoongea na muuzaji wa kichina ( supplier ) jaribu kuhakikisha vitu vingi tu nje na mbali ya bei ambayo watu wengi wao wanaangalia sana hii na kukosea kuto kuangalia vitu vingine. Jaribu kufirikia kwa namna hii
- Je wanajibu message zako kiusahihi na kwa wakati ) Are they responsive?
- Je wanauliza maswali yanayoendana na nini unataka katika bidhaa yako au wanakupa tu maelezo ya bidhaa zao?
- Je wanapicha za bidhaa unazozitaka wewe?
- Je mnaweza fanya mawasiliano kwa kuwapigia calls, whatsapp call au skype?
- Je wao ni watengenezaji au wao ni kampuni ya kuuza na kununu ( Manufactures Vs Trading company) Hii tutaiongelea siku zijazo
-Je wanatoa maelezo kiuwazi au kuna vitu wanaficha kuuliza?
-Nchi zipi sana wanauza hiyo products zao? Hii ni kubwa sana kwasababu hii inaweza kuonesha ni UBORA gani ambao hawa wanatengeneza.


3. Mazungumzo zaidi ya Biashara ( Negotiations)
Wachina wanamsemo unasema “一分钱一分货” “Yi fen qian Yi fen huo” maana yake "unapata unacholipia"
Hii inamaanisha sio kila wakati ufanye manunuzi ya bei ya chini chini sana, mara nyingi bei za chini na ubora wa bidhaa huendana sana. Wakati unapokua unaongea na wauzaji wengi kwa wakati mmoja unapotaka biadhaa jaribu kuweka mahusiano ya muda murefu unapoengea nao na useme " unataka biashara ya muda mrefu sio biashara ya siku moja tu" kwahiyo ni vizuri kutengeneza urafiki nao ( Hii ni mtazamo wa biashara wa kichina)
Pointi ya kubeba, hata kama una haraka vipi at least ongea na wauzaji zaidi ya 3 kujua vizuri bei ya bidhaa unayoitaka.

Pia Jaribu kuulizia Bei za bidhaa zako zikiwa na uwingi tofauti, kwasababu katika ulimwengu wa wachina uwingi ndiyo kila kitu . Unaweza uliza bei ya piece 5,000 na Bei 50,000 ukakuta gap lililopo ni kubwa sana. Katika mazunguzo zaidi, usisahau kuongelea bidhaa kuwa nyingi.



4. Hakikisha Kimtandao ( Online Research & Due Diligence)
Sio kila king'aacho ni almasi, Yes ni kweli sio kila muuzaji wa kichina ni wa kweli, hakikisha unapitia maelezo yake vizuri kuogopa kuibiwa na kudanganywa mtandaoni. Yes watu wanaibiwa kila siku na kila saa kwa wauzaji wapo kwenye mitandao ya kina alibaba. Kwa teknolojia ya photoshop na kuedit vitu, hata vijana wa chuo wanaweza weka profile zao kwenye alibaba na kuuza.


5. Uliza Sample ( Sample)
Baada ya kuona huyu supplier ni mzuri na unaweza kumuamini kwa kiwango kikubwa, na bei nakila kitu kimekamilika, wakati mzuri wa kuomba Sample. Hapa hatuongelei imani tu kwa kuamini kwa macho, omba SAMPLE utumiwe uone. Sample inaweza tumia siku 5-12 kufika kwa DHL, Fedex na wengine lakini ni vyema zaidi ya kuanza kutengeneza vitu vyenye uwingi mkubwa na vikawa tofauti na unachokihitaji.


6. Pokea Sample ( Evaluate Sample)


Ihakikishe sample yako kama ipo sawa na kile unachokihitaji, kama unataka kubadirisha na kufanya design yako pia ni muda sahihi wa kufanya hivyo.


7. Purchase Order ( P.O)
Unaponunu kitu chochote kwenye mtandao wa alibaba au platform ya China au hata kwa mikataba ya uso wa uso hakikisha unakua na Purchase order ambayo itakulinda kwa siku za usoni. HAKIKISHA Purchase order inakua na maelezo yote unayotaka kuanzia


8. Payments
Unapofanya malipo ya aina yoyote kwanza kabisa hakuna 100% inalipwa bila kupata kitu chochote upfront.
Hakuna standard inayosema lazima ulipe 30% advance payment na baadaye ulipe 70% hii ni imekua kama kawaida lakini kuna wauzaji ( supplier) wanataka 50% advance na 50% kabla hawajatuma kwa meli. Unaweza kuongeza zaidi na mnaweza kubadirisha mawazo namna mnavyotaka iwe.

Usikubali kutuma kwa njia ya Western Union, mara nyingi 98% ni utapeli. Kwa order ya aina yoyote hakikisha unafanya Bank Transfer.

DIRTY TRICK: HAKIKISHA MPOKEAJI WA PESA NA JINA LA USAJILI WA KAMPUNI AU KIWANDA VINAFANANA. KAMA HAIFANANI HII NI BENDERA NYEKUNDU KABISA KUNA MCHEZO UNAWEZA FANYIKA WA UTAPELI ( KUA MAKINI)



9. Usafirishaji ( Shipment)

Inashangaza kwamba watu wananuna kontena na kontena, lakini hawakagui mzigo kabla haujasafirishwa kutoka China kuja Tanzania. Nimesikia case sio moja ni zaidi ya tano watu wanaagiza A wanapokea Z ( wanapokea tofauti na wanachoagiza). Hakikisha unafanya ukaguzi kabla mizigo yako haijaondoka kuanza safari kuja Tanzania.

Kuna makampuni ya ukaguzi ambayo yanafanya hii, lakini mengine yanakua na deal na viwanda kuwaandikia report kua mzigo ni sawa japokua ni mzigo mbovu. ( Kuwa makini)

Baada ya kufanya ukaguzi ndiyo unaweza kuruhusu mzigo kuondoka na kuja sehemu husika.


Kiufupi hii ni namna unaweza kufanya unaponunua bidhaa kutoka China.

Kama unataka wasiliana nami unaweza nitafuta kwa number
+255627637767
Karibu Pia ofisini kwangu Mikocheni, Hekima Garden kwa maelezo zaidi.

Asante.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    37.7 KB · Views: 53
SababuYaKununua,
Hapo kwenye sample, it won't work kwenye bidhaa za machinery. Ila la msingi zaidi ni kujenga mahusiano na supplier. Na anaweza akawa anakuadvice hadi muda mwingine kwenye technical details hasa kwa wale wanunuzi wa mashine. Mawasiliano mara nyingi mtafanya sana Whatsapp lakini ukitaka kununua bidhaa ni vizuri ukafanyia transaction kwenye trusted site ili both parties muwe protected. Kwenye usafirishaji, bado kuna changamoto hasa kama mzigo ni mdogo wa kutojaza kontena moja. Kuna jamaa wanajiita consolidator, hawa wanakuwa na kontena wanapakia mizigo tofauti. Ukifika Mzigo Bongo ujiandae kuwalipa hela yao kutokana na CBM. Kuna lingine, kama unaagiza machinery lazima ujue kama hiyo mashine inatakiwa kufanyiwa inspection before kusafirishwa, bila ya hivyo utapambana na TBS.
 
Una safirisha mizigo kutoka China? Gharama zako zikoje kwa aina za bidhaa?? Au uzito?

Mf. Mashine isiyo zidi kg 10 au kg...
 
Kivipi wakati kwenye website yao silent ocean wakasema hiyo kazi hawafanyi?
Silent ocean si kampuni pekeyao wanaofanya mzigo kuja Tanzania, kuna Choice International, na wengine, pia silent ocean wanafanya loose cargo jaribu kuongea wahusika directly. asante
 
kwa vitu vidogo ambavyo chini ya kg 10 tunatumia sana usafiri wa ndege, kidogo ni ghali japo ndani ya siku 7-9 tunakua tumepata mzigo hapa Tanzania, gharama dola 7.8 /kg na ukifika hapa ni dola 3.
Na huo usafiri mwingine ambao sio ndege ni usafiri gani na bei zipoje kiongozi...
 
Back
Top Bottom