Habari zenu ndugu wapendwa wana MMU wote,
Kwa heshima na taadhima naomba kuwashirikisha mambo yangu wawili yanayohusiana na mahusiano kwa ushauri zaidi na majadiliano,
Case no 1..
Kuna kijana anadai ananipenda lakn nimemkatalia kwa sababu haiwezekani kuwa nae (we are not compatible at all at all)..Age much older than him na mambo mengine.Lakini reaction yake ni kuwa yeye kama akifa saa yoyote basi mimi ndio chanzo na kama wakipeleleza watajua mimi ndio chanzo..Nilikuwa nachukulia utani lakn sasa naona huu wimbo wa kufa unazidi..sijaelewa kama anatania tu au yupo serious lakn ninavyomuona akili zake dakika mbili mbele...Asije akafanya kweli afu nikawa sababu... Nishaurini ni handle vipi hii issue.
Case no 2.
Kuna babu mtu mzima above 60 ananing'ang'ania niwe kwenye familia yake kama mke/mkwe.. Ilianza wakati naanza kazi na nikamkuta hapo ofisini.Alikuwa anaonyesha dalili za ku care lakn sikumpa nafasi ya kuropoka... Baadae sijui alikata tamaa au vipi akaoa yani akafunga ndoa na mke aliyekuwa anaishi nae.Baada ya hilo akaja baba mwingine wa hapo ofisini na kunieleza jinsi huyo babu alivyokuwa anajigamba kuwa ni lazima anioe na alinifanyia hata dawa(kwa mganga) iliyoshindikana anyway.Nilimuita na kumuuliza habari hizo mbele ya mleta habari na hakukana/alikubali..Juzi kati kaibuka tena akidai kuwa ni mpango wa Mungu niwe naye...Ndipo nilimuuliza kama ana mpango mke wake afe ndio anioe(ndoa ni mpaka kifo kitenganishe).Alishtuka kwa maneno hayo na akageuza kibao na kusema kuwa kama yeye imeshindikana basi ni LAZIMA mtoto wake anioe.Akaongeza kuwa nitake nisitake lazima niingie kwenye familia yake..Sijamuelewa huyu mzee ana nini na mimi? na anaringia nini.Ninavyomuona ni kama hatanii na anachoongea. Naombeni ushauri na maombi ikiwezekana ili aniwache nipumue...
kasoro wewe mzabzab
Kaunga dear sina hata tone la kupenda hapo...sometimes huwa nakereka sana to be honest na hata huwa nafikia kuona aibu na kujiuliza hivi hawa wameanzaje anzaje??kwani dada r u currently in a committed love relationship, wots ur plan abt this word love na mahusiano au bado upoupo sana
Kuna unaye mpenda kati yao au kwakuwa wameshow interest tu?
With reference from case no 1; Kiukweli msikilize vizuri huyo mtu dada, kama kweli ana nia ya dhati na kama upo single, basi mpe nafasi, kupenda kunauma wazee. Jiulize, kwa nini ang'ang'anie kwakwo tu? Lazima kuna kitu kaona kwako na hajaona kwa wengine. Na bahati mbaya kama hayo aliyokwambia yakimkuta, na hata kama itokee kwa sababu nyengine tofauti, hivi itakuaje......utaishi kwa mawazo wewee.......Yani ungejua maumivu wanaume tunayopata kwa kumpenda msicha kwa thati halafu anazingua.......kwa kuwa nafahamu maumivu ya haya mambo, mimi naomba kumtetea huyu kijana mwenzangu huyu.........please accept his request.....ila msikilize kwanza.
PLEASE THINK AGAIN AND GET LISTENING TO THESE FEW WORDS BY MARK ANTHONY (I Need you, with lyrics)
I need you. (I really need nobody but you)
Father of All SAUDARI Ruttashobolwa Tized chardams Kindimbajuu BADILI TABIA Kongosho Snowwhite Vin Diesel asakute same ubungo Tetra
Asanteni wote kwa ushauri wenu mzuri.. mbarikiwe.
Father of All SAUDARI Ruttashobolwa Tized chardams Kindimbajuu BADILI TABIA Kongosho Snowwhite Vin Diesel asakute same ubungo Tetra
Asanteni wote kwa ushauri wenu mzuri.. mbarikiwe.
kwanza huyu hivi hana case ya kufile kweli?
nahisi kuna grounds za kufungua kesi hapa!YAWE TU KISHERIA IF SO IS THE CASE?au mi na akili zangu za vitenzi ndo zinanielekza hviii?manake mwalimu wako naye amejaa vikumushi vishirikishi tu kichwani mweh!
Father of All SAUDARI Ruttashobolwa Tized chardams Kindimbajuu BADILI TABIA Kongosho Snowwhite Vin Diesel asakute same ubungo Tetra
Asanteni wote kwa ushauri wenu mzuri.. mbarikiwe.