Ushauri unahitajika: NCC Education Programu ya business information technology

Ushauri unahitajika: NCC Education Programu ya business information technology

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
7,602
Reaction score
7,344
Hii program ina dahili vijana waliomaliza form 4. Mwaka wa kwanza unafanya foundation program ya NCC level 3. Ukifaulu unaingia Level 4 (mwaka mmoja) baadae level 5(mwaka mwingine mmoja). Kila level wanakupa Diploma.

Baada ya hapo kama ukitaka kuendelea unaruhusiwa (ukifaulu Level 5) kudahiliwa na University of Central Lancashire UK na kusoma Level 6 kwa mwaka mmoja. Ukifaulu Chuo hicho kinakutunuku.

BSc (Hons) Business Computing and Information Systems(UCLAN University). Kwa Tanzania kuna vyuo viwili vinahusika. Pia baada ya Level 3 kama ukifaulu na una uwezo kuna vyuo visivyopungua 26 vya UK na nchi nyingine unaweza kuomba udahili na kuanza mwaka wa kwanza wa degree tofauti.

Niombe ushauri kwa wenye uzoefu na hii program kama ni njia nzuri ya kumpitisha kijana ambaye ana interest na Business Computing and Information Technology.

(
 
Hii kitu niligonga mwamba. NACTE waliniambia vyuo vinavyotoa hiyo program kwa Tanzania hawajavitambua (kimoja hakija pata level ya registration inayotakiwa na kingine kilipoteza accreditation yake kwa sababu za kiufundi wala sio uwezo wao wa kutoa hizo program) kwa hiyo hiyo program haitambuliki NACTE.

Kusema kweli sikuelewa logic ya NACTE kwani wenye program UK wanavitambua hivyo vyuo na wametoa accreditation. Lakini kwa Tz mambo siyo hivyo sikuendelea na huo mpango lakini course zinaendelea.
 
Masiya,

Na pia naskia ukienda na hiyo level 6 diploma nacte ambayo wao wanaiita degree unapewa Odinary diploma yani Nta level 6
 
Na pia naskia ukienda na hiyo level 6 diploma nacte ambayo wao wanaiita degree unapewa Odinary diploma yani Nta level 6
Mkuu hapa umechanganya madesa. NCC na level zake ni tofauti kabisa na NTA levels. Ukiwa na NTA level 6 Ordinary Diploma unaweza kufikiriwa kuingia NCC Level 4 Diploma (Year 1 UK University). Ukiwa na Level 6 ya NCC unakwenda TCU wanao assess degrees na si NACTE.
 
Hapana kaka me Kuna watu nilisoma nao walikua wanasoma hii Nakuajiriwa serekalini sasa baada ya awamu hii ya uongozi kuingia ikabidi kwenda kuhakiki vyetu vyao TCU lakini cha kushangaza nikua TCU wakawa wamewakadiria kwa kuwapa ngazi ya elimu ya NTA level 6.

Yani ordinary diploma badala ya bachelors degree kaka kwahio wale waliotegemea nyongeza ya mshahara kwa kupanda ngazi kiielimu ikawa imekula kwao mzee.
 
Mkuu hapa umechanganya madesa. NCC na level zake ni tofauti kabisa na NTA levels. Ukiwa na NTA level 6 Ordinary Diploma unaweza kufikiriwa kuingia NCC Level 4 Diploma (Year 1 UK University). Ukiwa na Level 6 ya NCC unakwenda TCU wanao assess degrees na si NACTE.
Samahani kwa ku changanya Nacte na Tcu chief
 
A.Ngindo,
Kama TCU wameamua hivyo basi uko sawa ingawa sidhani kama tcu kwa uamuzi huo walikuwa sawa.
 
Back
Top Bottom