USHAURI TAFADHALI:mke kagoma kubadili dini yake

Muache aendelee na anachokiamini mradi tu smekweleza wazi. Sababu ni kuwa unaweza kuishi ns mke ambaye kwa nje mko dini moja lakini kumbe mwanzo ni mwanachama katika lile kundi linalotembeaga uchi usiku kwenye wakiwanga. Ni heri aishi na dini nanayoiamini na wewe ishi na dini unayoiamini na kila mtu ameonesha wenzake uzuri wa imani yake kwa matendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wandugu...
Kabla sijamwoa alinijua kuwa Mimi ni muislam,aliniahidi kubadili dini ila nimpe mda.maisha yamesonga miaka imepita tumejaaliwa kuwa na familia
Siku za hivi karibun mwenzangu nikaona amenunua kitabu Cha tenzi za rohoni ...baada ya chakula cha jioni anaanza mapambio ndani...anakemea mapepo juzi Kati kaenda kanisani na kujitambulisha ameokoka.namuuliza mbona unavunja makubaliano anadai yeye uislam hauwez...niko njia panda hapa nawaza watoto ...sijui nifanyaje.wazazi wake hawanipi ushirikiano wowote.nisaidien tafadhal
Huyo ndio mtu mwenye misimamo na Mungu wake, kila mtu aamini juu ya hatma yake baada ya haya maisha, usimlazimishe nyie dada zenu wakitaka kuolewa na wakristo mpo tayari hata kuwachinja
 
1. Ulichokipenda kwake kipo ama kimeondoka?

2. Dini ni nini kama mna upendo na mnaelewana tabia?

3. Kama unamlazimisha abadili imani yake aliyokuwa nayo na imekuwa sehemu ya tamaduni zake basi na kabila nalo atabadilisha? na jinsia nayo atabadilisha ili mfanane kwa kila kitu?
 
Hapo kila mtu abaki na dini yake kama ni kufunga Ndoa fungeni Ndoa ya Serikali, Watoto wakikua wakiwa na akili wana uchaguzi wa kuchagua imani yao.
 
Hii inshu inafanana na Yangu ila mimi nilichoamua kila mtu aendelee na dini yake ndoa tutafunga ya serikali na inshu ya watoto nawapa Uhuru wakikua wachague imani wanayoitaka siwezi kuwalazimisha kwa sababu kila nafsi ni huru,mimi naangalia upendo na maelewano mazuri niliyo nayo na mke wangu,masuala ya dini hayawezi niharibia mambo Yangu.
 
linapokuja suala la dini binadam wengi ni wabinafsi sana bt kitu wasichokijua ni kua dini zote ni njia za kumuelekea mungu hivo zungumza nae kistarabu kama kapenda njia hiyo mwache asali hata usipate shida mkuu
Kama hili ni jibu sahihi basi ni vema mwanamume naye akabadili dini kumfuta mkewe.

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Hii inshu inafanana na Yangu ila mimi nilichoamua kila mtu aendelee na dini yake ndoa tutafunga ya serikali na inshu ya watoto nawapa Uhuru wakikua wachague imani wanayoitaka siwezi kuwalazimisha kwa sababu kila nafsi ni huru,mimi naangalia upendo na maelewano mazuri niliyo nayo na mke wangu,masuala ya dini hayawezi niharibia mambo Yangu.

Uliamua uamuzi sahihi mkuu
 
Ushauri wangu unaanzia kwenye uzoefu niliouona kwa jaamaa yangu tuliyekuwa tumepanga nyumba moja,mke wake kwa asili ni mkristo,na jamaa ni mpemba muislamu pure asiye na makuu kuhusu dini za wengine.

Awali mke alikuwa anaenda msikitini lakini baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka mitano mke akabadili dini na kuwa mkristo,kwa mtoto wao aliyekuwa muislamu naye akawa mkristo,kwa vile huyu jamaa yangu hakuwa complicator maisha yalisonga hadi Leo wako pamoja.

Kinachokusumbua mtoa maada ni kuwa unaamini wewe dini yako ndio njia sahihi ya kukufikisha peponi na hivyo kuwaona wakristo kama watu wasio na mwelekeo,usingekuwa na imani hiyo ungemwacha mkeo afanye yake kama jamaa yangu alivyoamua,na kama hukutaka au kutarajia Haya yakukute ni bora ungeoa mtu wa dini yako .

Mwisho dini ni mpango wa mwanadamu katika kumtafuta Mungu ,sasa kwa Mimi siwezi kumhukumu mkristo au muislamu kwamba kakosea njia ,hivyo relax kaa na mama watoto wako mlee watoto siku zisonge ,life is too short usijipe stress mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake wa sasa ni tofauti sana na wa zamani ama mama zetu.....

Hawa wasasa wanaongozwa na viburi, jeuri na ujuaji ile hali vichwani mwao hakuna wanalolijua.

Zamani mwanamke anapoolewa akiondoka kwao kurudi ni msiba au sijui kuwe na dharula gani ila siku hizi mwanamke unaishi nae siku tatu za wiki nne zilizosalia anazitumia kwa wazazi wake akikimbia majukumu ya ndoa.... Na ukikaa vibaya nguo za watoto mabegi utakuta muda wote yapo kwa bibi yao mzaa mama.

Turudi katika kisa chako. Ni wazi kuwa huyo mwanamke wako alokukubalia hivyo si kutoka moyoni, aidha alikuwa anafanya hivyo ili kukufurahisha au kukufanya ujisikie comfortable kuwa nae. Lakini ndani ya nafsi yake alikuwa na yake..... Sasa ameona yale malengo yake hayajafikia tayati ameanza kuamsha bange zake......

Wanawake wa sasa wanapenda jitisha na vitu vya kipuuzi na pengine hata havipo na havitawatokea. Imagine mtu anaanza kuwaza kuwa utakufa na kumuachia watoto, au anawazia kuwa unaweza mtelekeza yeye na watoto.

Ushauri wangu kwako wewe kaa kimya na ufocus na maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom