Wazazi wa binti hawajui kuwa ''kabla hujafa hujaumbika''?
Kama issue ni ulemavu wa kijana hapo wazazi wanakosea, what if kama binti yao angekuwa mlemavu na akakataliwa ukweni, wangejisikiaje?
Binti ni mtu mzima, japo ushauri wa wazazi ni wa muhimu lakini imefika wakati wa yeye kufanya maamuzi yake. hatuwezi kumwambia afanye nini au aamue vipi ila yapo mambo ya kuangalia katika maamuzi
1. Anawaelewa vizuri wazazi wake? je hao wazazi ni watu wa aina gani? Wapo wazazi wengine majanga tu so hata ushauri wao nao pia unautazama mara mbili mbili...
2. Yeye anaonaje, je issue ya mume ni ya kuchaguliwa na mzazi/ au ya kupata approval kutoka kwao?
3. Anampenda kweli huyu kijana mwenye ulemavu au anamuonea huruma tu kwa sababu ya ulemavu na uyatima wake?
4. je kijana mlemavu, anatosha kuwa mume bora kwake?
Ahsante.......