Ushauri tafadhali kwa huyu dada

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Kuna Dada ambaye yupo kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka miwilii sasa, walibahatika na mumewe kupata mtoto wao kwanza kama baada ya mwaka mmoja wa ndoa ingawa huyu Dada alipata complications nyingi kabla na wakati wa kujifungua. Wiki kama 2 zimepita wamegundua mimba nyingine imetinga tayari bila wao kutarajia. Sasa sasahivi imekua shida na ugomvi kwenye hiyo ndoa kwani mume ameng'ang'ania kwamba watoe hiyo mimba kwasababu hatakuwa na uwezo wa kuilea na sababu nyingine mtoto wao wa kwanza bado mdogo ana miezi 8 sasa. Lakini huyu Dada hataki na hapendi kufanya hiyo kitu na hajawahi kufanya kwa maelezo yake na hasa Imani kali ambayo anayo kwenye Dini yake. Lakini sasa anahofia kuharibu ndoa yake, wakati mwingine anafikiria tu kufanya hivyo kumridhisha mumewe, maana sasa hawaelewani ni kununiana tu ndani ya nyumba.

Sasa mbaya zaidi, Juzi wakati mumewe yupo bafuni alichukua simu ya mumewe kutaka kuitumia, akaona msg zote zimefutwa zimebakia za kwake tu, akangundua kuna namba ambayo mumewe huwa anaitumia sana kwa kupiga na kupigiwa, Lakini hiyo namba imeandikwa jina la Kiume ambalo yeye halijui maana marafiki zake na mumewe wengi anawafahamu. Hiyo namba akairekodi pembeni, kesho yake yaani jana mumewe alipoondoka asubuhi aliipiga hiyo namba akapokea mwanamke, hakuongea naye aliishiwa nguvu akaikata.

Sasa huyu Dada amekuwa na mawazo mengi, hajui aanzie wapi na afanye nini kwenye hayo matatizo yote mawili ambayo yamemkuta. Mwenye ushauri na uzoefu wa mambo kama haya hebu nisaidieni nimshauri vipi huyu Dada.
 
kuhusu mimba waende wote hospitali.madaktari ndio watoe ushauri sahihi..

kuhusu simu,asirudie tena kupekua simu ya mwenzie...
 
Ni kweli kuwa mjamzito wakti ana mtoto wa miezi nane si sawa kiafya hasa ya mtoto, itabidi ajipange vilivyo juu ya afya ya mtoto, kwa maana ya lishe. Simshauri atoe mimba, maana anaweza kupata complications kubwa zaidi na ndo ikawa mwisho wa kuzaa. kama mwanaume anaogopa gharama, ajipange kuzikabili, na ni vizuri mkaenda wote kwa gynaecologist kwa ushauri zaidi.
kuhusu mimba waende wote hospitali.madaktari ndio watoe ushauri sahihi..

kuhusu simu,asirudie tena kupekua simu ya mwenzie...
 
kabla sijakushauri naomba kujua huyo dada ana kazi au bihashara kwa ujumla anakitu anafanya kinachomuingizia income then nimshauri nini cha kufanya hapaswi kupelekwa pelekwa
 
kabla sijakushauri naomba kujua huyo dada ana kazi au bihashara kwa ujumla anakitu anafanya kinachomuingizia income then nimshauri nini cha kufanya hapaswi kupelekwa pelekwa

Asante mama kigogo, Huyu Dada alikuwa na kazi lakini aliacha kutokana na sababu za kimaslahi kama miezi 4 hivi iliyopita, hivyo yupo kwenye harakati ya kutafuta kazi nyingine. Ni mhitimu wa chuo, ana degree moja.
 
Waende tuu kwa daktari waangalie suala la hiyo mimba maana atapata ushauri zaidi wa nini cha kufanya
kama mtoto wa kwanza alizaliwa kwa complications kibao utegemee na kutoa mimba kutakuwa na madhara zaidi kwa huyo dada maana inawezekana asipate tena mtoto maishani wakati ndo huyo ametoa mimba
Ni suala la kujipanga tuu kwa huyo jamaa maana mimba ndo hiyo na mtoto bado ni mdogo
Ila aji/pange tuu maana akija kuzaliwa atamkuta wa kwanza tayari ana mwaka na nusu hivi
 
kwanza kabisa naomba kdhana ya mimba ya bahati mbaya ifutike kwani naamini hakuna bahati mbaya kwenye mimba .. maadam mtoto ana miezi minane ni vyema tu akalea mimba amwachishe mtoto ziwa aendelee na maziwa ya kopo aepukane na maziwa ya ng'ombe ..

suala la simu si vyema kupekua simu ya mume au mke kwani kuna pasua kichwa kinaendelea .. tatizo wengi wetu waonapo kuna ugomv hukiimbilia kupekua simu as if ndo imeleta madhara hayo kumbe ndo unakuza tatizo
 
...iwish baada yakusikia sauti ya kike,mimba itoke kwani angekuwa amebakiwa na tatizo moja!!
 
Waende tuu kwa daktari waangalie suala la hiyo mimba maana atapata ushauri zaidi wa nini cha kufanya
kama mtoto wa kwanza alizaliwa kwa complications kibao utegemee na kutoa mimba kutakuwa na madhara zaidi kwa huyo dada maana inawezekana asipate tena mtoto maishani wakati ndo huyo ametoa mimba
Ni suala la kujipanga tuu kwa huyo jamaa maana mimba ndo hiyo na mtoto bado ni mdogo
Ila aji/pange tuu maana akija kuzaliwa atamkuta wa kwanza tayari ana mwaka na nusu hivi

naamini maamuzi ya kulea au kutokulea liko kwa wahusika wenyewe sasa daktari ni kwenda kusikia nyie wahusika mnatakaje lakini si kutegemea dr awaamulie
 
naamini maamuzi ya kulea au kutokulea liko kwa wahusika wenyewe sasa daktari ni kwenda kusikia nyie wahusika mnatakaje lakini si kutegemea dr awaamulie

Yaani mkuu wanavyoenda kwa Dr tayari wana maamuzi yao maana Dr hata siku moja hawezi kuingilia au kuwaamulia wattoe mimba maana in case wakija kukosa mtoto watamlaumu yule Dr maisha yao yote
La muhimu analoenda kuwashauri Dr ni namna ya kuhandle the situation now ya kuwa na mimba na mtoto mdogo na athari zake na je akizaliwa mtoto hatakuwa na madhara kwa hiyo familia
 
mkuu hapo uko sahihi maana kama ujauzito wa kwanza ulikuwa na matatizo japo mleta mada hajasema matatizo ni yapi lakini kama yanahusiana na ujauzito kwa nini wafikirie kutoa badili ya kutafuta jinsi ya kulea???? na hili la simu nadhani ni nyongeza tu ya kukuza tatizo ila naamini kuna tatizo zaidi ya hili lililopo
 
kabisa mkuu na nahisi wanaficha mambo mengine kuliko hili la mimba
Mkuu mambo ya ndani ya ndoa mengine ni pasua kichwa
 
Nimekuelewa mkuu. Tatizo lilikuwa ni la ujauzito, ilipelekea hata mtoto kuzaliwa Njiti wa miezi 8, ila mtoto alitoka salama na mpaka sasa ana afya nzuri kabisa. Huyu dada ni ndugu yangu wa karibu aliniomba tukutane akanieleza hayo ambayo yapo moyoni mwake, Inawezekana kuwepo mengine lakini yeye aliniomba ushauri kwa hayo. kwa wakati ule nilishindwa kumshauri, nilijikuta najikanyaga kanyaga hata mi mwenyewe maana niliogopa nisije nikatoa ushauri ambao ungeweza kuhatarisha ndoa yake, nilimuomba akae chini kwanza atulie amuombe na Mungu amuongoze kwenye hilo, maana hata mi sihafiki kabisa suala la kutoa mimba. nimemuomba anipe muda na mimi niendelee kufikiria.
 
Nimekuelewa mkuu. Tatizo lilikuwa ni la ujauzito, ilipelekea hata mtoto kuzaliwa Njiti wa miezi 8, ila mtoto alitoka salama na mpaka sasa ana afya nzuri kabisa. Huyu dada ni ndugu yangu wa karibu aliniomba tukutane akanieleza hayo ambayo yapo moyoni mwake, Inawezekana kuwepo mengine lakini yeye aliniomba ushauri kwa hayo. kwa wakati ule nilishindwa kumshauri, nilijikuta najikanyaga kanyaga hata mi mwenyewe maana niliogopa nisije nikatoa ushauri ambao ungeweza kuhatarisha ndoa yake, nilimuomba akae chini kwanza atulie amuombe na Mungu amuongoze kwenye hilo, maana hata mi sihafiki kabisa suala la kutoa mimba. nimemuomba anipe muda na mimi niendelee kufikiri

Sasa kama mume anajua yote haya na anajua tatizo la mke wake kwa nini akimbilie kutoa mimba
je utoaji huo wa mimba ukileta complications zaidi hata kufikia kuharibu kizazi cha huyo dada itakuwaje maana muathirika zaidi hapo ni mwanamke maana mwanaume atatafuta tuu watoto wengine nje huko
Yaani sidhani hata kwa Dr wanaenda kufanya nini
Wakae chini wote wawili yeye na mumewe na mumewe aelezwe madhara ya huo utoaji mimba maana kikubwa hapo ni mama kutokuja kupata mtoto tena au kuharibu kizazi au na kufa maana yote yanawezekana
 
kabisa mkuu na nahisi wanaficha mambo mengine kuliko hili la mimba
Mkuu mambo ya ndani ya ndoa mengine ni pasua kichwa

maana litokalo njia na kusikika kwa watu mara nyingi si tatizo ila lipo ambalo linakaa uvunguni wanaona aibu kulisema kwani lazima liwadharirishe wahusika
 
Nimekuelewa mkuu. Tatizo lilikuwa ni la ujauzito, ilipelekea hata mtoto kuzaliwa Njiti wa miezi 8, ila mtoto alitoka salama na mpaka sasa ana afya nzuri kabisa. Huyu dada ni ndugu yangu wa karibu aliniomba tukutane akanieleza hayo ambayo yapo moyoni mwake, Inawezekana kuwepo mengine lakini yeye aliniomba ushauri kwa hayo. kwa wakati ule nilishindwa kumshauri, nilijikuta najikanyaga kanyaga hata mi mwenyewe maana niliogopa nisije nikatoa ushauri ambao ungeweza kuhatarisha ndoa yake, nilimuomba akae chini kwanza atulie amuombe na Mungu amuongoze kwenye hilo, maana hata mi sihafiki kabisa suala la kutoa mimba. nimemuomba anipe muda na mimi niendelee kufikiria.

hilo alilolifikisha kwako ni sehemu ya tatizo kwani naamini halijaanza ghafla lina mwendelezo wa muda mrefu, na wanaume wengine wanafanya kama kukomoa wakiona hakuna maelewano ndani anaweza akapiga hesabu za mimba kumfunga mke , lakini kwa huyu kulia lia kuitoa ina maana kuna tatizo zaidi isije ikawa wanataka kuachana
 
maana litokalo njia na kusikika kwa watu mara nyingi si tatizo ila lipo ambalo linakaa uvunguni wanaona aibu kulisema kwani lazima liwadharirishe wahusika

Usije ukakuta huyo bwana tayari ana hawara yake ana mimba nje huko so anaona ni mzigo kulea mimba ya nyumbani na ya nje
Maana sioni haja ya mtu kusema kuwa hayuko tayari kulea mimba yake na anashauri kabisa wakatoe mimba mke na mume wakatoe mimba ambayo imeinfia kwa uhusiano halali kati yao wawili
Na mtoto ana miezi nane ukijumlisha na umri wa mimba ya pili miezi tisa mtoto wa kwanza atakuwa na mwaka na miezi mitano ambayo hata kama ni kula anaweza kuwa ameshafikia kupewa na uji na vyakula laini
Ahhh hapo bana kuna issue zaidi ya tunayoelezwa hapa
 
hilo alilolifikisha kwako ni sehemu ya tatizo kwani naamini halijaanza ghafla lina mwendelezo wa muda mrefu, na wanaume wengine wanafanya kama kukomoa wakiona hakuna maelewano ndani anaweza akapiga hesabu za mimba kumfunga mke , lakini kwa huyu kulia lia kuitoa ina maana kuna tatizo zaidi isije ikawa wanataka kuachana

Sidhani kama wamefika huko kwa jinsi ninavyowafahamu. labda nitadadisi zaidi.
 
ndio hivyo rocky, na ndio maana nasema kisa cha mke kupekua simu ni katika kuhalalisha mawazo yake kwa mume kwamba ndo tatizo .. mim bado naamini kuna tatizo ambalo ni mme , mke au wote wawili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom