DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 301
Kuna Dada ambaye yupo kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka miwilii sasa, walibahatika na mumewe kupata mtoto wao kwanza kama baada ya mwaka mmoja wa ndoa ingawa huyu Dada alipata complications nyingi kabla na wakati wa kujifungua. Wiki kama 2 zimepita wamegundua mimba nyingine imetinga tayari bila wao kutarajia. Sasa sasahivi imekua shida na ugomvi kwenye hiyo ndoa kwani mume ameng'ang'ania kwamba watoe hiyo mimba kwasababu hatakuwa na uwezo wa kuilea na sababu nyingine mtoto wao wa kwanza bado mdogo ana miezi 8 sasa. Lakini huyu Dada hataki na hapendi kufanya hiyo kitu na hajawahi kufanya kwa maelezo yake na hasa Imani kali ambayo anayo kwenye Dini yake. Lakini sasa anahofia kuharibu ndoa yake, wakati mwingine anafikiria tu kufanya hivyo kumridhisha mumewe, maana sasa hawaelewani ni kununiana tu ndani ya nyumba.
Sasa mbaya zaidi, Juzi wakati mumewe yupo bafuni alichukua simu ya mumewe kutaka kuitumia, akaona msg zote zimefutwa zimebakia za kwake tu, akangundua kuna namba ambayo mumewe huwa anaitumia sana kwa kupiga na kupigiwa, Lakini hiyo namba imeandikwa jina la Kiume ambalo yeye halijui maana marafiki zake na mumewe wengi anawafahamu. Hiyo namba akairekodi pembeni, kesho yake yaani jana mumewe alipoondoka asubuhi aliipiga hiyo namba akapokea mwanamke, hakuongea naye aliishiwa nguvu akaikata.
Sasa huyu Dada amekuwa na mawazo mengi, hajui aanzie wapi na afanye nini kwenye hayo matatizo yote mawili ambayo yamemkuta. Mwenye ushauri na uzoefu wa mambo kama haya hebu nisaidieni nimshauri vipi huyu Dada.