Ushauri: Taasisi ya misaada ya kielimu

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
HABARI WAPENDWA: NAOMBA USHAURI JUU YA SUALA LIFUATALO:

Taaluma yangu imeniwezesha kukutana na wanafunzi wa ngazi mbalimbali wenye ndoto na nafasi za kusoma/kuendelea na elimu ila kutokana na changamoto za kifamilia na kipato cha wazazi wanalazimika kutafuta misaada.

Binafsi nimefanikiwa kumobilize michango kwa miaka miwili mitatu iliyopita na nashukuru kwa mahusiano niliyonayo na watu wanaonizunguka wanatokea kuniamini sana, tatizo linalokuja ni kwamba sina taasisi rasmi inayoshughulikia suala hilo, linabaki kuwasaidia kienyeji, na ikitokea wanafunzi wanufaika wanapokuwa likizo wanarudi tena kuomba misaada kwangu wakati programu yangu mimi ni ya muda tu haswa wakati wanapokwenda kuanza ngazi fulani ya elimu.

OMBI LANGU: NAOMBA USHAURI
Ushauri ninaouomba kwenu ni namna ipi na kupitia mamlaka zipi nitaanzisha taasisi rasmi itakayomobilize fedha kupitia wadau /matukio/ michezo/ tamasha ili kuweza kuweka fedha za misaada midogomidogo kwa wanafunzi hao japo kwa mwaka kuwasaidia kwa ada na vifaa vya kusomea.

Ni muundo upi wa taasisi unaweza kurahisisha kutimiza azma yangu?

Nitashukuru sana! Tusaidiane kuwasaidia hawa watanzania nao wajipate!
 
Back
Top Bottom