Ushauri: Serikali mrejesheni haraka mwalimu aliyesimamishwa kazi

Kwa muda mrefu sijachangia mada humu ukumbini lakini Leo nitachangia kidogo,

Kwanini mwalimu unakubali hasira zikutawale zaidi ya maarifa, ikiwa wewe mwalimu umekwenda mafunzo ya ualimu na umeshindwa kutumia elimu uliyonayo kumsaidia mwanafunzi na badala yake unatumia hasira tayari unajenga nidhamu ya uongo, wanafunzi hawakufika hapo kwa ajili ya adhabu wamefika hapo ili kupata elimu na mwalimu umeonesha upeo wako wa kusomesha ni mdogo, ni wajibu wa mwalimu kujua jinsi gani ya kumsaidia mwanafunzi sio kumuadhibu
Tatizo walimu wengi wanaotumia adhabu kama hizo, uwezo wao wa kusomesha ni mdogo na wanatumia adhabu kama njia ya kujikinga ili asitambulike au ana matatizo ya akili
 
Weekend hii ni imani yangu kuwa bado mshahara haujaisha embu nenda kanywe hata KITOKO itatosha sana kukupa fikira mpya
 
Kwa sasa wagonjwa ni wengi,lishe mbovu mwl asipokuwa makini anaweza kuua.
 
Ifikie wakati watu wakubali tu ukweli; kazi ya ualimu ni ngumu sana. Na kimsingi walimu wanatakiwa waishi kwa tahadhari kubwa.
Nakubaliana na wewe mkuu. Ila watu hawajui kabisa. Kwa sababu walimu kila watakavyofanya wakidhani wanatatua wanaangushiwa lawama.
 
Kuna dawa flan ukiwa unaumwa unashauliwa uiweke kwenye unyayo au upake mafuta kwenye unyayo na unapona.
 
Tunaua kizazi cha sasa na kesho kwa sababu ya kuchekea chekea watoto.

Sisi mbona tulichapwa fimbo mpaka 50? Sisi mbona tuliteswa uko JKT baada ya kumaliza form six? Tulikufa au tulikuwa tunafundishwa Maisha?
...........
Naongea kama mzazi mwalimu mkuu alejeshwe kazini haraka.
Wewe una mamlaka gani hata utoe amri mwalimu mkuu 'alejeshwe' kazini haraka? Mara wazazi wengine fukuza mwalimu na hawa wengine rejesha mwalimu.

Kama wewe ulipigwa fimbo 50 na hukulalamika haina maana kwamba ilikuwa ni sawa. Haikuwa sahihi hata kidogo.
 
Kashasimamishwa na natamani apelekwe mahakamani halafu tuone nayo itaamua vipi.
Kama mzazi ni muwajibikaji na kweli una Nia ya kumfunza mwanao, basi hata Ile adhabu isingetokea. Ila kwa kubweteka na kutegemea kulelewa mtoto wako na mwalimu, ndio hapo zigo linakuwa halimithiliki kwa mwalimu, na mwalimu anafanya unyama.
 
Yaani wewe ni pumba kabisa,hivi umeonana vile viboko vya unyayoni?vipi katka maisha yako ya shule uliwai kuchapwa viboko kwenye unyayo?
 
Zamani kulikuwa na uhaba wa walimu, tulikuwa tukihitimu kidato Cha sita tunaomba kwa muda kufundisha . Ukiwa mwanafunzi huwezi kujua shida ya ualimu, wengi tuliosoma vyoo, na maficho ya kuvutia Bangi kwa wanafunzi ni vitu vya kawaida sana. Kama hujasoma shule za umma au kufundisha shule za umma ambako usafi, ni WA mwanafunzi, maji ya usafi ni juu ya mwanafunzi, kupalilia eneo la shule ni juu ya mwanafunzi. Sasa kwa hizo shughuli zote ni wangapi wanapenda kufanya hizo kazi kiasi kwamba mwalimu aongee nao kama katekista wafanye hizo kazi kwa hiari bila viboko, Kuna wanafunzi wanapenda kufukuzwa shule, na kupewa adhabu ya kurudi kukaa nyumbani.

Ni shule za umma tu ambako mtoto anakuja shule baada ya mzazi kukamatwa. Rai kwa walimu wapunguze sana kufikiria mafanikio ya wanafunzi, kiasi kwamba u wanajitoa roho, mwili, na akili kulazimisha mwanafunzi afikie mafanikio.
 
Sanamu lako liwekwe popote utakapopenda
 
Asantee karibu
Actually, hutakiwi kunishukru, ni pengine tu labda kwa sababu hujanielewa nilichomaanisha.
Nilichomaanisha ni kwamba, ningekuwa na mamlaka na wewe , ningekuchukulia hatua kali sana za kinidhamu; pengine kuzidi hata zile zilizochukuliwa kwa yule chizi mwenzako aliyeonekana akiwachapa watoto huku akiwa amewakanyaga miguu. Kwa hiyo unatakiwa ujihesabu kuwa wewe ni mtu mmoja mwenye bahati sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…