USHAURI: Rais Magufuli vunja ATCL. Anzisha Tanzania Airways ama Kilimanjaro Airways

Kwa mantiki hiyo, nakushauri Rais wangu fanya maamuzi sahihi. Hata kama utatumbua majipu yote yaliyoota hapo ATCL, vijipu uchungu vitaendelea kujitokeza na hivyo utajikuta unafanya kazi ya kukamua majipu tu kwa miaka yako 10 bila ya ufanisi wa shirika hilo.
Umetililika vizuri lakini hapa umeharibu, hiyo miaka 10 amepewa na nani?
 
Nasikia Kitilya kafutiwa mashitaka!!! hakuna atakayefungwa kwa ufisadi nchi hii: Hata Lugumi, IPTL nazo zifutwe kabisa maana na zenyewe zinafilisi nchi. (KA) Kilimanjaro Airways ndo jina zuri.
 
True, ATCL should be declared Bankrupt ili kuinusuru serikali na madeni ya shirika hilo na iundwe company mpya ya umilki wa ndege mpya. Kwenye biashara ya usafiri wa anga inayohusisha makampuni mengine ya kimataifa mazingira yetu ya kitanzania ya wizi ni bad news. Vunja ATCL na kutengeneza kampuni yenye watu wanaojua biashara hiyo.
 
baba paroko kazi ya kuchagua jina umeiweza. Ila nahisi ukikaa muda kidogo utaanza kujilaumu kwa nini "nimetaja Kilimanjaro ya kina mbowe", bora ningesema Tanzania airways peke yake. Maana wewe chochote karibu na mbowe kwako ni sumu.
Nafikiri Tanzanian airline ingefaa kwa sasa kama jina.
 
Lizaboni hongera kwa kuonyesha uelewa wako wenye tija kwenye mambo ya msingi ya kujenga nchi.
Such thinking is what will make our country move forward with positive altitude toward developments achievement. Keep it up pls.
Nadhani waliotufikisha hapo wamejifunza kitu kutoka kwako.
Ahsante sana Mkuu. Huu ni wakati wa kumshauri Rais wetu ili
Kichwa kweli mwana jamii. MAGU soma hii message ya mtanzania uone watu walivyo na vichwa vilivyo tulia.
Naamini kuwa mheshimiwa Magu ataisoma na kuielewa. Naamini kuwa ataifanyia kazi
 
True, ATCL should be declared Bankrupt ili kuinusuru serikali na madeni ya shirika hilo na iundwe company mpya ya umilki wa ndege mpya. Kwenye biashara ya usafiri wa anga inayohusisha makampuni mengine ya kimataifa mazingira yetu ya kitanzania ya wizi ni bad news. Vunja ATCL na kutengeneza kampuni yenye watu wanaojua biashara hiyo.
Safi sana. Naona hoja hii imeungwa mkono
 
nadhani iitwe Tanzania airways, na kila ndege iwe na unique name, kwa chini mfano kilimanjaro, serengeti, ngorongoro n.k
jina la nchi ni muhimu kujulikana likiunganishwa na majina ya mbuga zetu.watu waweze ku link kati ya nchi na majina ya mbuga zake
 
nadhani iitwe Tanzania airways, na kila ndege iwe na unique name, kwa chini mfano kilimanjaro, serengeti, ngorongoro n.k
jina la nchi ni muhimu kujulikana likiunganishwa na majina ya mbuga zetu.watu waweze ku link kati ya nchi na majina ya mbuga zake
Wazo zuri sana hili. Naamini litafanyiwa kazi
 
Haki ya Mungu huu ujinga sijui umeutoa wapi! Unaijua sheria ya mufilisi?? We unadhani tutafuta tu jina na kuanzisha jina lingine!! Emb endelea kulima mahindi huko buana!! Umetoa maoni kama ya Nape Nnauye kwa kweli!! Just like that??
 
Mbona mlituaminisha kuwa Magufuli kwenye chupa hiyo hiyo ya samaki (ccm) atatuletea mabadiriko sasa inashindikanaje kwa ATCL?au mmeshasahau mlivyokuwa mnatudanganya?
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimetafakari sana juu ya hili shirika letu la ndege hasa baada ya madudu kibao yaliyoainishwa na CAG. Hakika nashawishika kusema kuwa Shirika hilo halina sababu ya kuwa hai mpaka sasa kwa sababu zifuatazo;
  1. Linakula fedha za walipakodi ilhali production yake ni ziro.
  2. Imejenga taswira mbaya na hivyo hata kama tutakuwa na ndege 100, halitaaminika tena na wadau wa usafiri wa anga.
  3. Jina la ATCL halitoi utambulisho wa moja kwa moja kwa nchi yetu tofauti na wenzetu wanaotumia Kenya Airways ama Rwandan Air
  4. Siku zote kipya kinyemi. Kama tutakuwa na shirika jipya la ndege litakuwa na ufanisi zaidi tofauti na kuweka mvinyo mpya kwenye glas ya zamani.
  5. Mentality ya wafanyakazi wa shirika hilo imejengeka katika kubebwa na kudekezwa hivyo hata kama tutaongeza ndege mwisho wa siku watahujumu tu
  6. Hawajatueleza kwa nini ndege zimepungua kutoka 9 hadi 2 na hivyo kama tukiendelea kuwanunulia ndege, tutaishia kwenda kwenye negative.
  7. Madudu yaliyobainishwa na CAG haiwezekani kulikarabati shirika hilo badala yake tunapaswa kulisambaratisha na hapo Mheshimiwa Rais utakuwa umejiwekea rekodi ya kuharibu kibaya ili kuwa na kizuri
Kwa mantiki hiyo, nakushauri Rais wangu fanya maamuzi sahihi. Hata kama utatumbua majipu yote yaliyoota hapo ATCL, vijipu uchungu vitaendelea kujitokeza na hivyo utajikuta unafanya kazi ya kukamua majipu tu kwa miaka yako 10 bila ya ufanisi wa shirika hilo. Wastaafishe watumishi wote wa ATCL, Anzisha shirika jipya, Tangaza nafasi za Ajira utaona jinsi watu kutoka Kenya Airways, Ethiopian Airways, FastJet, Precission Air na hata Rwandan Air watakavyomiminika kuomba kazi na hapo ndipo tutakapokuwa na shirika bora kabisa la ndege.

Nimalizie kwa kusema kuwa "KULINUNULIA NDEGE MPYA SHIRIKA LA ATCL NI SAWA NA KUPANDISHA GHOROFA KWENYE MSINGI WA NYUMBA ISIYO YA GHOROFA"
 
Lazima ifike wakati tukubari kuvunja vya zamani na kuanzisha vipya vyenye tija kwa maslahi ya taifa.
nitafurahi siku nikiona ukija na hoja ya kuitupilia mbali ccm, chama cha zamani,chama cha majipu, chama cha majambazi,chama kilichoifanya nchi yetu kuota majipu kila kona
 
Mbona mlituaminisha kuwa Magufuli kwenye chupa hiyo hiyo ya samaki (ccm) atatuletea mabadiriko sasa inashindikanaje kwa ATCL?au mmeshasahau mlivyokuwa mnatudanganya?
Pole sana ndugu. Hoja yako haina maana kwenye mjadala huu
 
Back
Top Bottom