USHAURI: Prof. Mbarawa, chukua marubani watano tu ATCL

USHAURI: Prof. Mbarawa, chukua marubani watano tu ATCL

ha ha hahaaaaaaa Mkuu unatisha i can imagine that your life is/was full of struggle and inspiring in different way!!! Anyway i hope kwenye harakati za kurudisha mali zetu "kwenye mifuko yenu" hukuwahi kutoa uhai wa mtu, ha ha ha ha aaa. link inagoma, nina shauku ya kujua ya enzi hizo.
Tulivyokuwa tukiiba almasi mgodi wa Mwadui na wenzetu kuuawa
Cheki tena hapo mkuu.
Kuhusu swala la kuuwa,sijui kama niliuwa kwa kukusudia,ile ya kutokukusudia hata Lebanoni na juzi kati kuwaweka kando wale vijana wa Paul pale DRC inawezekana.Maana kuna wakati ASkari wa mgodi anakuja we mkononi una kombeo tu,njia pekee na kumvurumishia jiwe moja la kombeo...Unaona mtu analala tu chini na wewe unakimbia,sasa huku nyuma unakuwa haujui kama umeuwa au umejeruhi!!Kulikuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya kuuwa na kuuliwa!Chchote kitakachotangulia ni heri...Sipendi kukumbuka hayo maisha!Mungu ni mwema
 
wacha kuchanganya desa, zipo ndege za kijeshi za kisasa kabisa hadi marekani walilalamika kuwa hatukustahili kuwa nazo.

Nakwambia waswahili wazushi, na ungo mwingii!! Mmmoja anawakandia marubani wa ndege za kijeshi zinazo beba wana jeshi na mizingo - kasahau kabisa au hajui kwamba hakuna tofauti na ndege Dash Bombadier zote zinatumia Turboprop Engines! Hivi alitegemea akute viti vya anasa kwenye ndege za kijeshi za kubebea mizigo na wanajeshi??

Eti ndege za kijeshi zinabamizwa ovyo zibapo tua - uongo mtupu, yeye kapanda ndege hizo mara moja tu kwa hisani ya jeshi na wala akulipa hata senti tano si hilo tu vile vile hajui chochote kuhusu fisikia ya Aerodyanamics/fluid mechanics hana habari kwamba wakati mwingine ndege inapo tua uwanjani inaweza kukutana na upepo (cross current/wind) wa ghafla na kuifanya itue kwa kishindo wakati mwingine kupinduka bila kujali kama ndege ni ya kiraia au kijeshi - msiwe mnatoa lawama zisizo na msingi.

Kuna ndege ya ATCL mpya aina ya Dash Bombadier iloyonunuliwa na Serikali ya Kikwete iliwahi kupata ajali wakati inatua katika uwanja wa Mwanza au Tabora au Kigoma sikumbuki vizuri, unajua tatizo lilitokana na nini?

Mwisho nataka niwashauri kama mna jambo la maana la kuchangia msiwe na tabia ya kulahumu marubani wa kijeshi bila sababu kumbuka wakati fulani ndio walisaidia kuendesha ndege za uraiani, kumbuka tukipata dhalula wao ndiyo watakuwa kimbilio letu, kitu kingine kinacho nishangaza ni hii tabia iliyo jengeka hivi sasa ya kuwabeza beza makapteni wa ATCL wenye umri wa 50+ yaani mnawachukulia kama takataka vile -WHY?? Mnasahau kwamba wao ndiyo walifanikisha kuendesha ndege zetu za Boeing, Fokker Friendship, Twin Otter bila ya kuangusha ndege hata moja au kusababisha ajali ya za kizembe - leo hii ndiyo mnawaona si lolote si chochote, AKILI GANI HIZI?

Linapo kuja suala la nani afanye nini katika shirika la ndege suala hilo tuliachie Uongozi wa ATCL na Wizara mama.
 
Baadhi ya marubani wa ATCL enzi hizo nadhani walitoka jeshini. Mfano ni hayati Capt. Mvungi. Nadhani pia ndege za serikali ambazo kwa sana zinabeba raia wa kawaida (wafanyakazi wa serikali), marubani wake wametoka jeshini. Sioni shida yeyote ya marubani kutoka jeshini kutumika ili mradi wamepata mafunzo husika na wametoka kwenye ajira yao ya mwanzo.
 
chukua popote unapotaka lkn type rating lazima wafanye kwani ndege zinatofautiana
 
Back
Top Bottom