Umewahi kupanda lile dege la jeshi hata kwa kupewa lift?Umewahi ona "nidhamu" ya uendeshaji wa "Military Aircrafts" na "Civil Aircrafts".
Umewahi ona "short take off" ya zile ndege za Jeshi na "Short landing" zake!?Mazoea hujenga Tabia.Ukiwapa hawa Military Pilots hata uwape training ya "Customer care" kwa kiasi gani,lazima abiria wakimbia ndege za hiyo kampuni.
Hawa akili zao sio kupakia abiria,bali "wanajeshi"...ndio maana lile dege lao ndani halina viti ila mabenchi tu,nyanyuka yao hewani ni kama wamebeba nyanya na vitunguu,tuwa yao ni kama ndani ya ndege wana kuku vibudu waliokufa wakati wana abiria.
Customer Care kwenye usafiri wa anga ni pamoja na raha na utamu wakati wa kutuwa na kupaa!wanaita "Smooth Landing" au "Kissing of the fore landing gear",sio unatuwa kwa kubamiza kama umebeba magari ya rais.Unafika chini nusu ya abiria wametapika na robo wana mshituko wa moyo,niliwahi safiri na shirika fulani la ndege hapa bongo,wakati wa kutuwa jinsi ndege ilivyojibamiza Mama mmoja akajuwa tayari kimenuka,kwa mshituko ule pale pale tulimfunika shuka la kwenda mochwari,lkn yote haya ni utuwaji wa rubani.
Hawa Wanajeshi acha wasafirishe tu kile kiti cha Rais kwenye ziara za mikoani na magari yake,huku kwenye Biashara yetu ya ATCL TUWAACHIE MARUBANI RAIA!!Yaani mwanajeshi unafikiri anaweza sema "Dear customer...we are in final Approach"....."Dear" kwa rubani ni neno lililo mbali ktk misamiati yake