Ushauri please: Vidume vyangu vinadundana balaa

Si tulikuwaga tunagombana sana tupo twins mara 2, tulinyweshwa majani ya kunde hali hiyo ikaisha kuna mtu alimwambia mama ni dawa! Chukua majani ya kunde chemsha halafu maji yake wape.
 
Watoto wanaopigana mbele ya baba yao baadae kuna uwezekano mkubwa wakawa na tabia zinazopishana na jamii ya wastaarabu. Mtoto anapigana na mwenzake huku babake akishuhudia na kuwapigia makofi huyo ni sawa na mtoto asiye na baba tu.
Mkuu umenifanya nicheke kwa huzuni, Malezi ya kizazi cha sasa ni tofauti na zamani.

Wazazi wa sasa wanaishi kihunihuni sana kwa kuzani ndiko kuishi kisasa.

Nakumbuka tukiwa wadogo ilikuwa balsa yaani mtu anayeitwa baba daaah kwanza akirudi tu Nyumba yote kimya watu tunakimbizana kwenda kuoga tuwe wasafi maana tutambulia fimbo ile ilitufanya kutambua kwa haraka vitu vipi mzazi havipendi

Siku hizi sio ajabu kuona mzazi na mtoto wanabishana kwa kujibizana.
Maadili mabovu yanachangiwa na wazazi wenyewe.

Ndo mana Walimu wanapewa zigo kubwa sana hawaeshimiwi na wanafunzi wakitaka kuwapiga kwa lengo la kuwaonya wazazi wanakuja juu dah
 
Watoto wanaopigana mbele ya baba yao baadae kuna uwezekano mkubwa wakawa na tabia zinazopishana na jamii ya wastaarabu. Mtoto anapigana na mwenzake huku babake akishuhudia na kuwapigia makofi huyo ni sawa na mtoto asiye na baba tu.
looohhh
 
ESAU NA YAKOBO WALIANZA KUPIGANA TANGU WAKIWA TUMBONI KWA MAMA YAO,HAO NI KINA MATUMLA WAJAO WATENGENEZEE ULINGO
 
Nimejikuta na furahii kwa jinsi unavyosimulia....ila usiwaze mama watoto,watakuja penda kupenda hao wanao
 

Hivyo ndivyo inavyotakiwa. Tatizo watoto wa siku hizi unakuta baba yao yupo kama shoga unadhani baadae mtoto atakuwaje? Huyu mleta mada mme wake ni mpumbavu na hana akili kabisa na ipo siku hao watoto watakuja kumgeuka na kumuabisha. Tatizo la kizazi cha sasa kinafikiri uzungu ndo kumuachia mtoto, filamu za kina wema sepetu zimwaaribu akili. Siku moja nilikuwa maeneo fulani nikaona mtoto wa miaka miwili amenyolewa kiduku na babake naye yupo hivyo, nikajisemea tu kwamba huyu mtoto amekosa baba kabisa.
 
Weeee. Shika adabu yako. Pumbavu ni wewe hapo usiekuwa na hoja.
 
Si tulikuwaga tunagombana sana tupo twins mara 2, tulinyweshwa majani ya kunde hali hiyo ikaisha kuna mtu alimwambia mama ni dawa! Chukua majani ya kunde chemsha halafu maji yake wape.
Lol. Hii kali
 
kawaida na Mara nyingi mdogo ndo anakuwaga mtata
wa kwangu ni wanawake Ila wanapigana balaa
Nilikuwa napata taabu kumuita kaka yangu "kaka" daah, tunadundana ila ni must kumuita kaka na ni lazima kumuamkia "shikamoo kaka" tukiamka asubuhi. Basi anaitikia kwa misifaaa, nachukia hatari.

Tukimaliza kudundana mama anatuita anaanza kutuhoji, enhee mmepata faida gani mlivyodundana? Tunabaki tunaangaliana tu, alafu lazima kuombana msamaha na kushikana mikono. Kipengele kilikuwa kigumu hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…