Nina rafiki yangu walifunga ndoa na mumewe 2002, mumewe hakuwa na kazi na elimu ya mumewe ilikuwa kidato cha nne kwakweli alimpenda mumewe kwa dhati. Mwanamke kipata chake ni kizuri (mwaajiriwa) alimpeleka mumewe shule na mpk akafikia level ya advance diploma bahati mbaya hakupata ajira mpk leo.Kwahiyo mahitaji ya ndani na kila kitu ni mwanamke. Kila akimpatia mtaji afanye biashara hela hajui anapeleka wapi na biashara hazionekani.
Mwaka 2006 mwanamke akanunua gari na kiwanja akajenga nyumba na vyote akaandika kwa jina lake(mwanamke). Maisha yakaendelea kwa amani na wakahamia ktk hiyo nyumba pamoja.
Mwaka 2010 mambo yakaanza kuharibika baada ya mwanaume kuzaa nje ya ndoa na kuanza manyanyaso kwa mkewe sababu hazai, na bahati nzuiri mwaka 2012 mwanaume akawa anasimamia biashara ya kaka yake na anapata vihela lakini mkewe haoni hata shilingi yake.
Mwanamke alipoma manyanyaso yamezidi akamwambia mwanaume tuachane, mwanaume akakubali kwa sharti wagawane mali(nyumba& gari),mwanamke hataki.
Alichofanya mwanamke akategea ameenda kulala kwa mzazi mwenzie akaleta mteja akauza nyumba na ushahidi wa jirani na mjumbe/serekali za mitaa( kwa kweli uamuzi aliufanya wa hasira sababu ameona mwanaume hakuwa na mapenzi ya dhati kwake na kwanini jasho lake akafaidi mwanamke mwingine NO).
Mwanaume kurudi kakuta geti limefungwa na mlinzi kamwambia nyumba imeuzwa. Mwanamke kaenda kupanga na kamwambia mumewe njoo tuishi nilikopanga tuanze maisha, mwanaume kagoma na kaenda kufungua kesi mahakamani?
Je mwanamke huyu atashinda kesi? au afanye jasho lake lisipotee?
Kwa mujibu wa vifungu vya 58,59 na 60 vya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kama ilivyofanyiwa mapitio 2002 vinaelezea namna ya umiliki ambao ni rebuttable presumption. kuna mali ya pamoja (joint property) na mali ya mmoja.
rebuttable presumption ina maana kuwa mali inaweza kuwa ya peke yako lakin umiliki ukawa wa wote yaan mume na mke na mali inaweza kuwa ya wote lkn ukiletwa ushahid fulan inaonekana umilik wake ni wa mmoja.
kinachotakiwa ni ww kuithibitishia mahakama juu ya aina ya umiliki wa hiyo nyumba.
kama unaushahidi wa kutosha kuhusu umilik na hakimu akiwa fair, utashinda.
Vithibitisho ni kama vipi mfano vya kumyesha mali ni ya mmoja? hati ya myumba, na kadi ya gari vipo kwa jina lake mwanamke.je inaweza kumsaidia ashinde?
Hati ya nyumba pamoja na kadi ya gari ni vielelezo utavyowasilisha mahakamani kuthibitisha umiliki wako. zaidi ya hapo ni ushahidi mwingine wa kimazingira utakaoonesha kuwa hiyo nyumba haikuwa ni ya familia bali ulikuwa unaishi naye tu humo lakini haukuitoa kuwa mali ya pamoja.
Ni mazingira gani concept ya rebuttable presumption of ownership ina apply?
mfano; wewe una nyumba ya urithi toka kwa wazazi wako, lakin kwa kumpenda mumewe unaitoa nyumba hiyo na kuwa ya familia na mnabadili hati inaonesha nyinyi wote ni wamiliki, mkiachana hata ulie vipi hiyo nyumba itakuwa yenu wote. au mmejenga nyumba wewe na mumewe, lakini mumewe kwa kuonesha mapenzi kwako anakupa wewe na hati anaandikisha jina lako, ushahidi huo wa kukupa wewe ukiletwa mahakamani baada ya kuachana mumewe hana cha kupata hiyo ndiyo rebuttable presumption of ownership iliyoelezwa ktk kifungu cha 60 cha law of marriage.
Itambulike kuwa mwanamke yupo kwenye ndoa ndio maana ku
Asante sana, ubarikiwe.
Naomba tu ashinde, maana mwanamke ameapa akishinda anarudisha pesa kwa alimuuzia na anaibomoa nyumba yote maana kawa kama kachanganyikiwa.Hii kesi mi naona imekaa vizuri kwa mwanamke...
Kweli equal right inafanya kazi yake...
Kabla Ya Kukushauri..... Ningependa Kujua Wamefunga Ndoa Ya Kikristo, Kimila Au Kiislamu?
Hapa Nitamshauri Cha Kufanya Ili Awe Safe Mbele Ya Sheria.