Ushauri: Nini cha kufanya ndani ya siku 7 zijazo

Ushauri: Nini cha kufanya ndani ya siku 7 zijazo

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,693
Mtanzania mwenzangu, naomba niwape ushauri mapema juu ya hili janga la Corona linaloikumba Dunia nzima.

Kabla ya huu ugonjwa kufika Africa wengi tulitegemea kuwa utakuwa na impact ndogo sana kwa nchi za Africa tukijipa matumaini kuwa Waafrica tupo strong na ugonjwa wa aina hii (Mafua).

Jana nimeona taarifa ya habari Al Jazeera ikisema Africa ijiandaye kwa mripuko mkubwa wa hili gonjwa ndani ya wiki 2 hadi tatu zijazo.

Jana hiyo hiyo nikamsikia Spika wa Bunge la JMT kuwa Tanzania haiwezi kuweka watu wote home lockdown sababu kipato cha asilimia kubwa ya Watanzania ni cha kubangaiza kila siku. Maana yake hata serikali haiwezi wapa chakula kama baadhi ya nchi zilivyofanikiwa kufanya.

Ushauri wangu ni kufanya yafuatayo.

1. Tafuta kiasi cha pesa chochote kinachoendana na matumizi yako unachoweza kutumia hadi miezi mitatu bila kufanya kazi yoyote ya kukuingizia pesa.

Hata kama huna hiki kiasi, nakushauri tumia hata assets zako nenda kakope mapema. Kumbuka uhai ni muhimu kuliko assets. Hizi zitataftwa tu baadaye.

2. Nunua chakula kinachoweza kutunzika ambacho unaweza kutumia kati ya miezi mitatu hadi sita. Hii fanya mapema kabla serikali haijatangaza total home lockdown. Maana ikitokeaa ikatangazwa chakula kitapanda bei kwa kasi ya ajubu.

3. Tafuta mbadala wa kuweza kufanya shughuli zako nyumbani kama itawezekana mapema iwezekanavyo.

4. Usisubiri Serikali ikutangazie home lockdown. Ikiwezekana anza kujifungia mwenyewe mapema iwezekanavyo. Jikinge wewe na familia yako.

5. Hakikisha Afya yako ipo sawa wakati wote. Waafrica tunakatabia kabaya sana kwa kutojali afya zetu. Mara nying tunaishi na magonjwa mbalimbali. Sasa huu sio wakati wa kuishi na mgonjwa haya madogo madogo yanayoweza kutibika. Mfano malaria, Typhoid, UTI, Minyoo Mafua ya kawaida, vikohozi na mengineyo. Ni muhimu sana kuhakikisha umejitibu mapema magonjwa ya namna hii maana inavyoonekana COVID -19 ikikutana na combination ya magonjwa mengine, survival rate ni ndogo sana.

6. Endapo utaamua kujifungia ndani wewe na familia yako, usibweteke tuu muda wote unaangalia TV au upo kwenye simu. Fanya mazoezi mara kwa mara. Au kwa wale wenye mashamba, nenda shambani panda hata mihogo.

Huu sio muda wa kusubiri kila kitu serikali ikuambie. Tumia na wewe akili zako.

Mwaka juzi niliandika post humu nikishauri Wakulima wa korosho kuuza Mazao yao kwa bei wanayoona ingewelipa kuliko kusubiri ile iliyokuwa imependekezwa na serikali. Maana biashara na siasa ni vitu viwili tofauti. Hivyo hivyo wakati huu siasa na Majanga ni vitu viwili tofauti. Jiongeze mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
IMG-20200331-WA0009.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo nani sasa hivi atanunua assets kwani kila mtu anawaza food..
Pia hata ujifungie assume unajifungia na ilikua ushaupata,
.then hesabu majanga katika hiyo familia..
Hapa kuna vitu vya kujifunza
Serikali, "Inatakiwa kujifunza kuboresha mifumo ya Afya,kiasi kwamba hata Mkuu mmoja akiumwa tusikie kapelekwa Bugando,sio hata katezi dume tu nje..", Pia serikali inatakiwa kujifunza kuweka bajeti ya Pesa za dharula hata Tsh.100bn., Na ilekebishe miundombinu kwa kila kata kuww na Kituo cha afya chenye uwezo wa kulaza wagonjwa wasiopungua 70.
Ifumue na kusuka upya mfumo mzima wa Elimu,

Jamii" Inatakiwa ijufunze kuweka akiba,hasa mtu mmoja mmoja,kiasi kwamba awe na akiba yake ya miezi 4 mbele,hata kama si Corona je angeugua na kulazwa mda mrefu je???", pia jamii inatakiwa kubadiri mtindo wa maisha ,desturi na tamaduni za kikale,

Wafanyabiashara,"Wanatakiwa kuwa na uvumilivu na kua jirani na wateja wao kwa kuwafariji hasa katika majanga kama haya,sio leo naona kila mtandao umepandisha gharama za vifurushi vya internet kwa kushusha kiwango cha data ilihali wanafahau now shugjuri nyingi za watanzani zinasita sita...

Mimi au wewe" Tujifunze kutotegemea watu aunkuongea pumba,kukosoa ovyo ovyo, Nijifunze kua MAISHA HAYANA FORMULA..

mwisho kila mtu afanye lile naona lafaa kwa kukabili,kujikinga na corona,na athari zake.

Kumbukeni kabla ya korona kuja,
Njaa ilikua inaua watu haa watoto taklibani 10k kwa siku lakini ilikua si tishio,
Leo hii korona inaua watu(Hasa kwenye mlipuko mikubwa) takribani 3k < imekua tishio..

Pia mjifunze ulaya si kuzuri,
Msingeenda au msingekuja au kuleta hilo gonjwa humu.

Kila bara na taifa lijifunze kujitegemea kwni now wameona hakuna cha urafiki au mahusiano mazuri au mimi mwanaShiasha nitatibiwa india au marekani wote mtatibiwa kwa yule yule doctor wa kifipa,kihaya,kingoni na nk.

🙌🙌🙌🙌
 
*Kwa wale tunaofikiri wagonjwa 19 wa Covid 19 kwa Tanzania bado SIO SERIOUS!![emoji848] Hebu tuangalie wenzengu wa nchi nyingine walikotoka wiki tatu zilizopita*

[emoji634] Italy
February 21 2020 - 21 cases
March 27 2020 - 86,498 cases

[emoji631] United States
February 21 2020 - 16 cases
March 27 2020 - 100,037 cases

[emoji632] France
February 26 2020 - 18 cases
March 27 2020 - 32,964 cases

[emoji629] Germany
February 25 2020 - 18 cases
March 27 2020 - 50,178 cases

[emoji633] Spain
February 27 2020 - 25 cases
March 27, 2020 - 64,059 cases

[emoji1130] Iran
February 19 2020 - 5 cases
March 27 2020 - 32,332 cases

South Africa [emoji1221]
March 1 2020 - 1 case
March 27 2020 - 1,170 cases

*Tupo pale wenzetu walipokuwepo wiki mbili tatu zilizopita.*
*Kama hatutajitahidi kujikinga nasi tutafika huko*.[emoji22]

*Watanzania wenzangu tujitahidi kuzuia muendelezo wa maambukizi ya Covid 19 kwa kuzingatia njia tunazoelekezwa na wizara.* .

*Ni jukumu lako wewe na mimi! Tuzingatie*[emoji1431][QUOTE="heradius12,

Jr[emoji769]
 
Ni ushauri mzuri sn Ila hapo kwenye kukopa pana ukakasi kidogo wakopeshaji hamna
 
Dunia haitakuwa kama zamani tena
Mjiandae na mchukue tahadhari


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom