Beeb
JF-Expert Member
- Aug 18, 2018
- 29,389
- 59,151
Hahaha naona mikoani kutajaa watuWakitangaza lockdown bila shaka tutapewa muda wa kujiandaa, mimi muda huo nafungasha virago nyumbaniii
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa kaelezea vzuri sanaa,,siasa na majanga kama haya ni tofauti jali tu afya yako basi achana na siasa.Mkuu watu imetupasa kuisikiliza serikali, japo kushauri ni jambo jema pia
Sent using Jamii Forums mobile app
Umeandika vizuri lakini umejichanganya hapo uliposema mtu aende shamba wakati tayari yupo kwenye lockdown.Mtanzania mwenzangu, naomba niwape ushauri mapema juu ya hili janga la Corona linaloikumba Dunia nzima.
Kabla ya huu ugonjwa kufika Africa wengi tulitegemea kuwa utakuwa na impact ndogo sana kwa nchi za Africa tukijipa matumaini kuwa Waafrica tupo strong na ugonjwa wa aina hii (Mafua).
Jana nimeona taarifa ya habari Al Jazeera ikisema Africa ijiandaye kwa mripuko mkubwa wa hili gonjwa ndani ya wiki 2 hadi tatu zijazo.
Jana hiyo hiyo nikamsikia Spika wa Bunge la JMT kuwa Tanzania haiwezi kuweka watu wote home lockdown sababu kipato cha asilimia kubwa ya Watanzania ni cha kubangaiza kila siku. Maana yake hata serikali haiwezi wapa chakula kama baadhi ya nchi zilivyofanikiwa kufanya.
Ushauri wangu ni kufanya yafuatayo.
1. Tafuta kiasi cha pesa chochote kinachoendana na matumizi yako unachoweza kutumia hadi miezi mitatu bila kufanya kazi yoyote ya kukuingizia pesa.
Hata kama huna hiki kiasi, nakushauri tumia hata assets zako nenda kakope mapema. Kumbuka uhai ni muhimu kuliko assets. Hizi zitataftwa tu baadaye.
2. Nunua chakula kinachoweza kutunzika ambacho unaweza kutumia kati ya miezi mitatu hadi sita. Hii fanya mapema kabla serikali haijatangaza total home lockdown. Maana ikitokeaa ikatangazwa chakula kitapanda bei kwa kasi ya ajubu.
3. Tafuta mbadala wa kuweza kufanya shughuli zako nyumbani kama itawezekana mapema iwezekanavyo.
4. Usisubiri Serikali ikutangazie home lockdown. Ikiwezekana anza kujifungia mwenyewe mapema iwezekanavyo. Jikinge wewe na familia yako.
5. Hakikisha Afya yako ipo sawa wakati wote. Waafrica tunakatabia kabaya sana kwa kutojali afya zetu. Mara nying tunaishi na magonjwa mbalimbali. Sasa huu sio wakati wa kuishi na mgonjwa haya madogo madogo yanayoweza kutibika. Mfano malaria, Typhoid, UTI, Minyoo Mafua ya kawaida, vikohozi na mengineyo. Ni muhimu sana kuhakikisha umejitibu mapema magonjwa ya namna hii maana inavyoonekana COVID -19 ikikutana na combination ya magonjwa mengine, survival rate ni ndogo sana.
6. Endapo utaamua kujifungia ndani wewe na familia yako, usibweteke tuu muda wote unaangalia TV au upo kwenye simu. Fanya mazoezi mara kwa mara. Au kwa wale wenye mashamba, nenda shambani panda hata mihogo.
Huu sio muda wa kusubiri kila kitu serikali ikuambie. Tumia na wewe akili zako.
Mwaka juzi niliandika post humu nikishauri Wakulima wa korosho kuuza Mazao yao kwa bei wanayoona ingewelipa kuliko kusubiri ile iliyokuwa imependekezwa na serikali. Maana biashara na siasa ni vitu viwili tofauti. Hivyo hivyo wakati huu siasa na Majanga ni vitu viwili tofauti. Jiongeze mwenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wanatutisha tu
Kwa kweli....me mwenyewe nitarudisha mpira kwa kipaWakitangaza lockdown bila shaka tutapewa muda wa kujiandaa, mimi muda huo nafungasha virago nyumbaniii
Sent using Jamii Forums mobile app
AhsanteKwa wale mabachela
-Michele kilo 8
-Unga kilo 6
-Dagaa ½
-Tambi pakit 5
-Viazi visado 2
-Unga wa ngano kilo 3
-Mafuta ya kula ltr 5
-Vitunguu ½ kilo
-Tangawizi ½ kilo
-Maharagwe kilo 3
-Viazi vitamu kilo1
-Sukali 1½
Sabuni lazima Mche 1 unga 1kg tosha.Usisahau mishumaa 3.
Anza kula vinavyooza haraka.Maharage ni vizuri kuyachemsha weka kwenye Friji unachota kidogo kidogo.Chapati za maji zinasukuma siku.
Nishati kama mkaa uwepo kama back up gesi endapo itakata ghafla.
Maji usitumie kwa Fujo.Kama unavyombo jaza.
Bila kusahau movies zako za kutosha.Weka hela ya emergency.Watumie wazee hela pia.
Nitaomba niwe kipa wako wakati huoKwa kweli....me mwenyewe nitarudisha mpira kwa kipa
Bitter truth 😩baada ya kuona kwamba huku mitandaoni tunatishana sana sasa nasitisha kutembelea JF mana humu ni mwendo wa kupandishana presha tuu. Kama ebola ilipita, zika ilipita basi THIS TOO SHALL COME TO PASS, TUSITISHANE.
ni njia gani hizo za kuzingatia ambazo wenzetu hawazizingatii...?*Kwa wale tunaofikiri wagonjwa 19 wa Covid 19 kwa Tanzania bado SIO SERIOUS!![emoji848] Hebu tuangalie wenzengu wa nchi nyingine walikotoka wiki tatu zilizopita*
[emoji634] Italy
February 21 2020 - 21 cases
March 27 2020 - 86,498 cases
[emoji631] United States
February 21 2020 - 16 cases
March 27 2020 - 100,037 cases
[emoji632] France
February 26 2020 - 18 cases
March 27 2020 - 32,964 cases
[emoji629] Germany
February 25 2020 - 18 cases
March 27 2020 - 50,178 cases
[emoji633] Spain
February 27 2020 - 25 cases
March 27, 2020 - 64,059 cases
[emoji1130] Iran
February 19 2020 - 5 cases
March 27 2020 - 32,332 cases
South Africa [emoji1221]
March 1 2020 - 1 case
March 27 2020 - 1,170 cases
*Tupo pale wenzetu walipokuwepo wiki mbili tatu zilizopita.*
*Kama hatutajitahidi kujikinga nasi tutafika huko*.[emoji22]
*Watanzania wenzangu tujitahidi kuzuia muendelezo wa maambukizi ya Covid 19 kwa kuzingatia njia tunazoelekezwa na wizara.* .
*Ni jukumu lako wewe na mimi! Tuzingatie*[emoji1431]
Jr[emoji769]
Homelockdown haimaanishi hutoki nje kuona jua. Familia nying unakuta nyumba mbele shamba lipo nyuma au pembeni. Unashindwaje kwenda shambanEndapo utaamua kujifungia ndani wewe na familia yako, usibweteke tuu muda wote unaangalia TV au upo kwenye simu. Fanya mazoezi mara kwa mara. Au kwa wale wenye mashamba, nenda shambani panda hata mihogo.
Sasa HOME LOCKDOWN na SHAMBA wapi wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Huo muda wa kujiandaa ndyo unaitwa panic au rush hour. Kila m2 anahaha. Hata anayeuza chakula lazima apandishe bei na ajibakizie mwenyeweWakitangaza lockdown bila shaka tutapewa muda wa kujiandaa, mimi muda huo nafungasha virago nyumbaniii
Sent using Jamii Forums mobile app
Issue sio kupita mzee, issue ni kwamba itatuacha ktk hali gani itakaposepa.baada ya kuona kwamba huku mitandaoni tunatishana sana sasa nasitisha kutembelea JF mana humu ni mwendo wa kupandishana presha tuu. Kama ebola ilipita, zika ilipita basi THIS TOO SHALL COME TO PASS, TUSITISHANE.