Mtanzania mwenzangu, naomba niwape ushauri mapema juu ya hili janga la Corona linaloikumba Dunia nzima.
Kabla ya huu ugonjwa kufika Africa wengi tulitegemea kuwa utakuwa na impact ndogo sana kwa nchi za Africa tukijipa matumaini kuwa Waafrica tupo strong na ugonjwa wa aina hii (Mafua).
Jana nimeona taarifa ya habari Al Jazeera ikisema Africa ijiandaye kwa mripuko mkubwa wa hili gonjwa ndani ya wiki 2 hadi tatu zijazo.
Jana hiyo hiyo nikamsikia Spika wa Bunge la JMT kuwa Tanzania haiwezi kuweka watu wote home lockdown sababu kipato cha asilimia kubwa ya Watanzania ni cha kubangaiza kila siku. Maana yake hata serikali haiwezi wapa chakula kama baadhi ya nchi zilivyofanikiwa kufanya.
Ushauri wangu ni kufanya yafuatayo.
1. Tafuta kiasi cha pesa chochote kinachoendana na matumizi yako unachoweza kutumia hadi miezi mitatu bila kufanya kazi yoyote ya kukuingizia pesa.
Hata kama huna hiki kiasi, nakushauri tumia hata assets zako nenda kakope mapema. Kumbuka uhai ni muhimu kuliko assets. Hizi zitataftwa tu baadaye.
2. Nunua chakula kinachoweza kutunzika ambacho unaweza kutumia kati ya miezi mitatu hadi sita. Hii fanya mapema kabla serikali haijatangaza total home lockdown. Maana ikitokeaa ikatangazwa chakula kitapanda bei kwa kasi ya ajubu.
3. Tafuta mbadala wa kuweza kufanya shughuli zako nyumbani kama itawezekana mapema iwezekanavyo.
4. Usisubiri Serikali ikutangazie home lockdown. Ikiwezekana anza kujifungia mwenyewe mapema iwezekanavyo. Jikinge wewe na familia yako.
5. Hakikisha Afya yako ipo sawa wakati wote. Waafrica tunakatabia kabaya sana kwa kutojali afya zetu. Mara nying tunaishi na magonjwa mbalimbali. Sasa huu sio wakati wa kuishi na mgonjwa haya madogo madogo yanayoweza kutibika. Mfano malaria, Typhoid, UTI, Minyoo Mafua ya kawaida, vikohozi na mengineyo. Ni muhimu sana kuhakikisha umejitibu mapema magonjwa ya namna hii maana inavyoonekana COVID -19 ikikutana na combination ya magonjwa mengine, survival rate ni ndogo sana.
6. Endapo utaamua kujifungia ndani wewe na familia yako, usibweteke tuu muda wote unaangalia TV au upo kwenye simu. Fanya mazoezi mara kwa mara. Au kwa wale wenye mashamba, nenda shambani panda hata mihogo.
Huu sio muda wa kusubiri kila kitu serikali ikuambie. Tumia na wewe akili zako.
Mwaka juzi niliandika post humu nikishauri Wakulima wa korosho kuuza Mazao yao kwa bei wanayoona ingewelipa kuliko kusubiri ile iliyokuwa imependekezwa na serikali. Maana biashara na siasa ni vitu viwili tofauti. Hivyo hivyo wakati huu siasa na Majanga ni vitu viwili tofauti. Jiongeze mwenyewe.
Sent using
Jamii Forums mobile app