Ushauri: Nimepiga mtu kisa usaliti wa mapenzi

Ushauri: Nimepiga mtu kisa usaliti wa mapenzi

Karimu123

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2015
Posts
243
Reaction score
114
Habari wakuu kwema,

Miezi michache iliyopita kama 7 mpaka sasa nilipata dada mmoja hivi ila nilikuwa na wasiwasi maana niliona kama kanizidi akili maana kapitia vingi nilimkatalia akanilazimisha nikaona fresh so tukawa nae nikampa moyo wangu wote maana nilikuwa sitaki kubanduka kwake nilimpenda kuliko kawaida.

Lakini nilikujagungua mimi ni daraja lake mafanikio maana kitandani honestly nilikuwa siko vizuri nikamwambia ok nitafind tiba ila usifanyie makusudi lakini hakusikia, nikawa nasikia kwa watu mara yupo na nani, sijui anamsindikiza nani nikaona ok sina haja kujibizana nikawa kimya.

Sasa boss wake alisafiri kumbe alikuwa anatembea nae nilishajua hilo ndo maana nikataka kuachana kwa amani hakuelewa akaja kwangu analia sana nikamwambia nenda mana machozi hayasaidii akaenda akarudi na kilio mara mbili nikaona isiwe shida nimsamehe atajirekebisha.

Ila nikasema nitamfuatilia nikamfuatilia nikamuona boss wake anakuja kwako kama saa nne akalala mpaka asubuhi sikutaka kuleta varangati nikachukuka malapa yake nikatupa, sasa huyu msichana anakejeli anajaribu ili kunisumbua nilishauadi nikamuambia ukifanya kitu mbaya nitakufanyia kitu kibaya hutakaa unisahau.

Leo nilipiga pombe kidogo nikamfuta kwako nikampiga simu nikaona anajibu nusu nusu nikaingia mlangoni nikagonga alivyotoka nilimpa kibao moja nikamsukuma nikamwambia kesho nikiona simu yako kwako kwangu nitamuua nikasepa, niambieni wakuu kama nimekosea.

NOTE; I hate being cheated maana sijawahi hata kumsaliti nampa chance kibao kwanini afanye hivyo sasahivi hasira 0%.

Nawasilisha wakuu
 
Mkuu kama unajitambua kutokuwa viziri kitandani, ni sababu tosha ya yeye kuachia nje! Maliza tatizo lako kwanza mambo yatakuwa safi. Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulikuwa huko vzuri ki aje?, yaan ulikuwa na upungufu wa nguvu za kiume? na kwa nn ustafute tiba.
maana kama haya mapungufu
madogo madogo yalihitaji kusaidiana tu, au kuingia jogging na kuongeza uzoefu.
kwanza shugulikia hayo matatzo hapo utakuwa na haki ya kupiga mtu, na kama bado huko vzuri bas usi ingie kwenye mahusiano mpakaa umeona uko vzuri maana utapiga watu kila sku kwa mtindo huo
 
Habari wakuu kwema,,, Miezi michache iliyopita kama 7 mpk sasa nilipta dada mmoja iv ila nilikuwa na wasi wasi maana niliona kama kanizid akil mana kapitia ving nilimkatalia akanilazimisha nikaona fresh so tukawa nae nikampa moyo wangu wote man nilikuwa sitak kubanduka kwake nilimpenda kuliko kawaida.

Lakin nilikuja gungua mim ni daraja lake mafanikio maana kitandani honestly nilikuwa siko vzr nikamwambia ok ntafind tiba ila usifanyie maksudi lakin hakusikia, nikawa nasikia kwa watu mara yupo na nan sijui anamsindikiza nani nikaona ok sina haja kujibizana nikawa kimya sas boss wake alisafiri kumbe alikuwa anatembea nae nilishajua hilo ndo maana nikataka kuachana kwa aman hakuelewa akaja kwangu analia sana nikamwambia nenda mana machoz hayasaidii akaenda akarud na kilio mara mbil nikaona isiwe shida nimsamehe atajirekebisha ila nikasema nitamfuatilia nikamfuatilia nikamuona boss wake anakuja kwako kama saa nne akalala mpk asubuh sikutaka kuleta varangati nikachukuka malapa ya nikatupa sasa huyu demu anakejel anajaribu ili kunisumbua nilishauadi nikamuambia ukifanya kitu mbya ntakufanyia kitu kibaya hutakaa unisahau....

Leo nipiga pombe kdg nikamfuta kwako nikampiga simu nikaona anajibu nusu nusu nikaingia mlangoni nikagonga alivyotoka nilimpa kibao moja nikamsukuma nikamwambia kesho nikiona simu yako kwako kwangu ntamuuua nikasepa niambien wakuu kama nimekosea.....

NOTE; I Hate being cheated mana sijawah hata kumsalit nampa chance kibao kwanin afanye ivyo asaiv hasira 0%......

Nawasilisha Wakuu


Umekosea sana
 
pole sana mkuu!kwanza nafurahi umejua una matatizo na ukakiri!hilo litakusaidia upone!nadhan umempiga wifi kwa hiyo

inferior ya shida yako!kakosea kwakweli!majitu yanapendwa hayajitambui!..na ww umekosea jitahidi umwache AENDE!
 
hongera kwanza kujitambua una tatizo!nadhan umeumia kumuona anaruka ruka na ulishamwambia!amekukosea sana!jitahd upate tiba!hilo li dada we liache liende na maisha yake! bora ww unamjali ....again pole tena
 
sijaongeza ttz mana huyu demu naye ttz heri nibaki na ttz lang kuliko kuwa na yangu na mwingine mkuu sijui kama unaelewa....
Mzee huyo hajakusaliti kwakua hauko vizuri kitandani kwakua hata tunaojiona tupo vizuri tunasalitiwa pia.
Humu kuna uzi wa mdada akielezea mumewe alipata ajali kiuno kikawa hovyo lakini hakuwahi kumsaliti (kwa maelezo ya uzi).

Huyo binti hiyo ni tabia yake tu ndiyo inampelekesha kwakua kama shida ingekua ni wewe angekucheat na mwanaume mmoja ila shida siyo wewe ni yeye ndiyo maana ulikua unasikia anatoka na watu wengi.

Unauliza kama umekosea kumpiga mwanamke, ni kweli umekosea. Dawa siyo kipigo, ni msimamo wako juu ya uhusiano wenu. Kama unataka aende muache aende kama huwezi (umepuuzia na kusamehe mara nyingi) baki naye.

Now fanya kutafuta tiba ya ishu yako bob.
Kuna uzi ulitaja miaka yako, kama ni kweli maana yake sasa hivi wewe una 23.
Huu umri unaendana na maamuzi yako katika huu uhusiano lakini hauendani na mwanamke uliye naye wala na kunywa serengeti tatu/ tano mpaka ukamfumania demu wako akiingizwa gheto.

Demu uliyemfumania mwanzo unasema uliyemtoimba bora liende, siku uliyomtoimba ndiyo siku ukamfumania.

Nahisi kuna ishara unajaribu kutoa, tafuta mtu uongee naye bob.
 
Back
Top Bottom