Ushauri: Nimeoa lakini simpendi mke wangu

Ushauri: Nimeoa lakini simpendi mke wangu

BIG THINKER

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2018
Posts
699
Reaction score
1,516
Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza,

Nikiwa kahama nilifanikiwa kukutana na mfanya biashara mwenzangu yeye amejikita zaidi kwenye Madini, katika kuzungumza ikafika usiku mimi nikamwambia ndugu yangu uende kwako tutaonana kesho akasema haendi kulala kwakwe nikapotezea mimi nikaenda zangu.

Ilipofika usiku wa saa Tisa Shemeji akanipia simu akauliza "Rafiki yako Bado yuko huko mbona hapokei simu!?" Nikamwambia Subil nakupigia lengo nimuulize jamaa aliko.

Kweli nikapiga simu nikamuuliza uko wapi akasema kuna sehemu amelala nikamwambia Shemeji ananiuliza uliko Sasa inakuwaje hujaenda kwako!? Majibu aliyonipa ndiyo yamenifanya nilete huu Uzi hapa.

Jamaa akasema "Kaka sikufichi Niko na mke wangu mwaka wa Tisa huu lakini SIMPENDI," nilishituka nikawaza amelewa au! Nikamwambia aje pale nilipofikia tuzungumze, kwel daika chache nasikia horn za gar nikatoka nje mlinzi akawa amefungua geti akaingiza gari ndani tukakaa nje kuzungumza.

Akasema tena kaka "SIMPENDI MKE WANGU" nataka unisaidie Sina aman ya kuwa nae nikawaza Cha kumshauri lakin nikasema Subil, nikachukua sim nikampigia Shemeji nikamwambia Niko na mme wako hapa ongea nae akaongea kidogo kwamba Kuna vitu Bado tunafatilia atakuja mke akasema Haina shida, hapo nawaza Cha kumshauri sipati.

Kwa kifupi huyu bwana ni tajiri tu mkubwa anaish kahama hapa Wana mtoto Mmoja na mke wake, nitaelezea muonekano wa mke wake, mke wake ni mfupi, katika kuzungumza akasema anataka atafute mwanamke mweupe mrefu mzuri anasema hapo roho yake itatulia.

Mimi nikamuuliza unauhakika ukipata mwanamke mweupe roho itatulia? Kwa kwel tumeongea mengi.

Sasa wazee wenzangu wenye busara nimshauri nn Rafiki yangu make mimi nilimwambia ukwel swla lako ni zito mbaya Zaid hata mwanamke huyo mweupe wa kuoa Hana Hadi atafute.

Sasa wataalam wa mahusiano nipeni Cha kumwambia mshikaji make anatia huruma Kuna muda unaongea nae mpaka machozi yanamtoka.
 
Alaaaaah sasa mbona umevunja Ndoa tayari?.

Matajiri wa Kahama wanjulikana.. zaidi ya yote, umeelezea Mke wake alivyoo .

Duuhh !!.
Muulize huo weupe na urefu atautumiaje katika maisha yake? Utamuongezea nini?

Otherwise huwa ni tamaa tu za kimwili. Mwambia atulie maisha yaendelee.
 
Alaaaaah sasa mbona umevunja Ndoa tayari?.

Matajiri wa Kahama wanjulikana.. zaidi ya yote, umeelezea Mke wake alivyoo .

Duuhh !!.
Hana utajiri wowote, anayemuongelea kahama hamna mbuzi mjinga kama huyo. Sasa kama ana taka mwanamke mweupe si akajipakulie tu wapo wengi na wenye heshima, amjengee kama tajiri. Mtu yupo kwenye ndoa achukue mchepuko ampe mimba tajiri au mjinga huyo.
Mpe mimba, mkeo utamueleza Baadae, mbona kuna maswala mepesi tu.
 
Kwanza hakuna uhusiano kati ya mapenzi ya kweli na utajiri, isipokuwa upo uhusiano wa utajiri na ukahaba....

Msaidie jamaa yako kwa kumweleza kuwa hawala huleta mikosi, mke huleta baraka na kuwa dhambi kubwa isiyosameheka kwenye ndoa ni uzinzi!
 
Kwanza hakuna uhusiano kati ya mapenzi ya kweli na utajiri, isipokuwa upo uhusiano wa utajiri na ukahaba....

Msaidie jamaa yako kwa kumweleza kuwa hawala huleta mikosi, mke huleta baraka na kuwa dhambi kubwa isiyosameheka kwenye ndoa ni uzinzi!
Ahsante Twilimbwa
 
Ila wanaume mkishapata hela sijui huwa mnakuwa vipiii kabla hajawa tajiri alimpenda akamuoa sasa hivi kimebadilika nini
Na sifa alimpa kuwa amempenda kwa sababu ya rangi yake! Ghafla rangi imebadilika....
 
Back
Top Bottom