Kiti Chema
JF-Expert Member
- Oct 18, 2017
- 1,793
- 1,941
Nawasabahi ndugu zangu mlio wazima na wale wenye shida kidogo Mungu atatia wepesi.
Niende kwenye kusudi maalumu, mimi ni kijana ambaye nikitazama idadi ya namba ya miaka yangu naona inakimbia.
Leo linalonifanya niandike uzi huu ni hii hofu ya kuoa niliyo nayo. Nimekuwa na tabia ya kuogopa kuoa na kujihi kuwa kama nikioa nahisi ndo nitajiongezea mizigo zaidi, maana kuna muda huwa najitathimini na kuwaza kwa sauti ikiwa marafiki zangu waliooa huwa wananisimulia changamoto wanazokumbana nazo katika ndoa au familia.
Je mimi nitaziweza hapo tu ndo swala la kuoa hukata na hamu inaniishia tena yapo mambo mengi huwa nawazaga.
Kwa wanasaikolojia hii hali inatokana na nini ikiwa kama ni habari ya uzinzi mimi huko siko maana nimelelewa katika misingi ya dini na ninaye mchumba mmoja tu ingawa nimepitia changamoto mbali mbali kupitia huyo binti lakini sikutaka kuwa leo nipo na huyu na kesho nipo na huyu.
Nitashukuru kwa mawazo yenu.